Posti hii inahusu zaidi matokeo ya maumivu makali , kuna wakati mwingine mgonjwa anapata maumivu makali ya viungo na dawa mbalimbali uweza kutolewa kwa mgonjwa huyo lakini matokeo yake huwa ni kuendelea kwa maumivu kwa hiyo yafuatayo ni matokeo ya maumivu
Matokeo ya maumivu makali.
1. Mgonjwa ubadilika kimtazamo na pengine anaweza kufanana kama amechanganyikiwa.
Hali hii utokea kwa mgonjwa mwenye maumivu makali kwa sababu mgonjwa anafilili kwamba hatapona na hivyo uanza kubadilika na pengine kuwa mkali, juwa na hasira na pengine kufanana kama amechanganyikiwa na kupoteza mwelekeo.
2. Pengine kwa sababu ya maumivu akilala ukosa usingizi na ulala macho kila siku kwa mda mwingine utasikia anaongea mwenyewe usiku au anaita wale ambao hawaumwi na wamelala na aliwalalamikia kuwa wamemwacha na hawamjali kwa hiyo tiba ni lazima ili kumfanya mgonjwa akaweza kupona na kuwa kawaida.
3. Pengine maumivu yakiwa makali sana na wengine ushindwa kabisa kushiriki tendo la ndoa kabisa na hamu kwa wengine uisha kabisa kwa hiyo maumivu yakiwa ya mda mrefu yanaweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa kwa hiyo ni vizuri kutibu maumivu mapema .
4. Maumivu pia yanaweza kusababisha kutengana kwa familia kwa sababu kama kutakuwepo na uzembe wa kutoshirikiana katika kuuguza Mgonjwa panaweza kuwepo na kutegeana na pia kama kipato ni kidogo na pia hiyo ni shida kubwa katika kumuuguza mwenye maumivu ya mda mrefu.
5.Kwa hiyo tunapaswa kutibu Magonjwa mapema kabisa ili kuepuka hatari ya kuwepo kwa maumivu ya mda mrefu kwa kufanya hivyo tutaweza kuwasaidia wagonjwa wetu pia na jamii iache tabia mbaya ya kuwanyanyapaa wagonjwa hasa wale walio kwenye maumivu makali.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowPosti hii inahusu zaidi mkojo wa kawaida kwa kila mwanadamu na unavyopaswakuwa, mkojo wa kawaida kwa binadamu huwa na sifa zifuatazo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi athari za mkojo mwilini, kwa kawaida tunafahamu kwamba mkojo ni matokeo ya mkusanyiko wa uchafu wa maji maji yanayokusanyika kutoka mwilini ikiwa mkojo umebaki mwilini usababisha madhara mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Unadhanivkufanya kazi kunaweza kukusababishia maradhi ama mwili kudhoofu, ama kukonda. Umeshawahivkujiuliza wanao nenepa huwa hawafanyi kazi?
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wagonjwa
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa mate mdomoni, mate ni majimaji ambayo hukaa mdomoni na husaidia katika kazi mbalimbali mdomoni.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Uvimbe au mashambulizi ya bacteria kwenye utando laini uliopo tumboni ambao kitaalamu hujulikana Kama peritonitis.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatua za kufuata unapohisi umeambukizwa na virus vya ukimwi. Kwa sababu watu wengi wanakuwa na kiwewe anapohisi ameambukizwa na virus vya ukimwi kwa hiyo wanapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...