Tunahitaji kuwa na protini mwilini. Kuna baadhi ya makundi ya watu wanahitaji protini zaidi. Je unawajuwa hao ni kina nana?, na je unauwa kazi za protini mwilini na athari za upungufu wake? endelea na makala hii.
Katika viinilishe muhimu mwili unavyohitaji amabavyo ni fati, protini, vitamini na wanga na mafuta mwili unahitaji protini kwa kiasi kikubwa kila siku. mwili unaweza kuibadili protini kuwa fati lakini si fati kuwa protini. hivyo protini ni kiinilishe muhimu zaidi ndani ya miili yetu. Katika makala hii nimekuandalia mambo muhimu unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo. Makala hii imeandaliwa wa kufuata nukuu na makala kutoka kwa wataalamu wa Afya na lishe.
YALIYOMO
Katika makala hii tutakwenda kuona
MUKTASARI KUHUSU PROTINI.
Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki ”proteios” likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe “nutrients” ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 1838 na Mkemia kutoka Swedih Jöns Jacob Berzelius.
Protini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng’enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)
Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes
Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.
VYAKULA VYENYE PROTINI
Tunaweza kupata protini kwenye mimea jamii ya mikunde kama kunde na maharagwe. Pia kiasi kikubwa cha protini tunaweza kukipata kwa kula mayai, nyama, samaki, dagaa na maziwa. Pia tunaweza kupata protini kwa kula nafaka kama mchele na nafaka zingine. Ulaji wa mboga za majani unaweza pia kutupatia protini kwa kiasi kidogo. Wadudu kama kukbikukbi, senene na wengineo pia wanaweza kutupatia protini.
Kwa kifupi vyakula vinavyotupatia protini ni pamoja na :-
KAZI ZAPROTINI NA VYAKULA VYA PROTINI MWILINI
Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini.
Kazi za protini mwilini:-
UPUNGUFU WA VYAKULA VYA PROTINI
Kama tulizoona faida za protini ndani ya miili yetu basi pia itambulike kuwa kuna hasara kubwa za kiafya endapo mtu atashindwa kupata protini za kutosheleza ndani ya miili yetu. Hapo chini nitakuorodheshea tu baadhi ya madhara ya kukosa protini ya kutosha:
ULAJI WA PROTINI KUPITILIZA
Kwa upande wa pili ulaji wa protini nje ya kiwango unaweza kuleta athari hasi katika afya ya mlaji. Zifuatazo ni madhara ya kula vyakula vya protini kupitiliza
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 2113
Sponsored links
👉1
Simulizi za Hadithi Audio
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4
Kitabu cha Afya
👉5
Madrasa kiganjani
👉6
kitabu cha Simulizi
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa Soma Zaidi...
Huduma kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo
Post hii inahusu zaidi huduma
Kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo,ni huduma maalumu ya kumsaidia mgonjwa aliyepata maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo. Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia Soma Zaidi...
Mambo yanayopunguza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo yanayopunguza nguvu za kiume Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu vitamini K na kazi zake mwilini
vitamini k ni moja katika vitamini vinavyoitajika sana mwilini. Je unazijuwa athari za upungufu wa vitamini k mwilini? Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa aliyepatwa na presha ya kupanda
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kupanda Soma Zaidi...
Faida za minyoo
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za minyoo Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...
Yajue malengo ya kusafisha vidonda.
Posti hii inahusu zaidi malengo ya kusafisha vidonda, kwa sababu Kuna watu wengine huwa wanajiuliza kwa nini nisafishe kidonda hospitalini au kwenye kituo chochote Cha afya, yafuatayo ni majibu ya kwa Nini nisafishe kidonda. Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA
Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg. Soma Zaidi...