Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki.
Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Utamjuaje kama ana aleji na nyuki?. ni pale utakapomuona aliyeng’atwa na nyuki akivimba mwili, na anaweza pia kupoteza fahamu. Pia hali hizi zinategemea ni kiasi gani cha nyuki wamemg’ata mtu.
Utakapomuona mtu ameng’atwa na nyuki usimkimbie, kwanza msaidie, kuhakikisha kuwa nyuki hawamng’ati tena. Unaweza kuchukuwa blanketi ama shuka uakmfunika vyema. Hakikisha na wewe umefunika pua, mgomo na masikio. Kama nyuki wanaendelea kuja mmwagie maji mgonjwa ili kupoteza harufu ya nyuki.
Hakikisha kabla hujaanza kutoa huduma ya kwanza, kwanza unaangalia hali ya aliyeng’atwa, kama hali ni ya kawaida na hahitaji kwenda hospitali. Kama anahitaji kwenda hospitali haraka wasiliana na kituo kilicho jirani ama tafuta msaada, kwa watu walio karibu. Hakikisha maamuzi haya hayaathiri hali ya mgonjwa. Ili kumpa huduma ya kwanza aliyeng’atwa na nyuki:-
1.kwa upole tumia kitu chenye wembamba kisha toa miiba ya nyuki kwenye ngozi ya mgonjwa. Katu usitukie kucha zako, maana zitaipasua miipa na sumu itaingia ndani na katu hutaweza kuitoa tena.
2.Unaweza kutuia kisu, ama kituchenye ncha, ila hakikisha kuwa miiba ya nyuki haikatiki kwa ndani. Kwa mfano unapotumia kiwembe kuna uwezekano mkubwa ukaikata miib kwa ndani.
3.Muweke mgonjwa mahali pa ubaridi kama inawezekana
4.Osha maeneo aliyong’atwa kwa sabuni na maji
5.Unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu.
6.Zipo dawa kama losheni (calamine lotion) ila ni maalumu kwa aliyeng’atwa na nyuki, kama zipo mgonjwa apakwe.
7.Hakikisha unamtuliza moyo mgonjwa.
8.Kama hali ni mbaya bado mgonjwa apelekwe kituo cha afya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na kumsaidia mwenye aliyeumwa na nyuki.nyuki na wadudu ambao wakikushambulia Sana na ukikosa msaada unaweza kufa au kuwa katika Hali mbaya.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kupoteza fahamu, ni sababu ambazo umfanya mtu kupoteza fahamu kwa sababu mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa fizi ambapo fizi huweza kuwa na maumivu, kuambukizwa, kuvuja damu kwenye fizi na Vidonda.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mzunguko wa mwezi kwa mwanamke, ni mzunguko ambao huchukua siku ishilini na nane kwa kawaida Ila lla ubadilika kulingana na mtu, Ila ngoja tuangalie siku ishilini na nane tu.
Soma Zaidi...Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa alieye ingiwa na uchafu puani (foreign body)
Soma Zaidi...