Post hii inahusu huduma ya kwanza kwa mtu aliyeingiwa na uchafu au kitu chochote sikioni. Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu ambapo hutumika kusikia, Kuna wakati vitu uingia ndani yake na kuleta madhara
Dalili za mtu aliyeingiza kitu chochote sikioni inawezekana kuwa maharage, mahindi, wadudu na vitu vingine kama hivyo ambavyo hupendelewa na watoto.
Dalili za mtu aliyeingiza kitu sikioni
1. Maumivu makali
2. Maambukizi kwenye sikio
3. Kuvimba ndani ya sikio
4. Sikio kuwa jekundu
5. Kushindwa kusikia vizuri
6. Kutoka uchafu sikioni
Vifuatavyo ni vitu vinavyoweza kuingia sikioni
1. Maharage
2. Mahindi
3. Wadudu
4. Mchanga
5. Toyi
6. Makaratasi madogo madogo
Tufanyeje Ili kuepusha Hali ya kuingia maharage, mahindi na vitu vingine kwenye sikio?
1. Watoto wanapaswa kuwa na mwangalizi wakati wa kucheza
2. Watoto wadichezee vitu kama maharage na mahindi
3. Watoto na watu wazima wawe na tahadhari hasa sehemu zile zenye wadudu kama vile nyuki na wadudu wengine wanaoweza kuingia masikio.
Huduma ya kwanza
1. Usitumie vitu kama msumari, ama kijitu kuchokoa sikio ili kutoa kitu kilichoingia, kufanya hivi kunaweza kuingiza zaidi hicho kitu
2. Kama kitu kinaonekana kitoe kwa upole kwa kukishika, kama kwa kutumia vipanio maalumu vidogovidogo kama tweezers
3. inamisha sikio kwa hali ambayo tundu iliyoingiwa na kitu itaelekea chini
4. kama aliyeingia ni mdudu tumia mafuta yaliyo na uvuguvugu, yaingize sikioni kisha inamisha kichwa kama ulivyofanya hapo juu. Usitumie njia hii kwa kitua ambacho kio mdudu.
5. tumia maji, ingiza sikioni ili hicho kitu kitoke pamoja na maji. Unaweza kutumia bomba la sindano kufanya hivi.
6. mpeleke mmgonjwa kituo cha afya kama kitu kitashindikana kutoka.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha hii ni chanjo wanayopewa watoto wadogo chini ya miaka mitano kwa lengo la kuzuia kuharisha chanjo hiyo kwa kitaalamu huitwa Rotarix.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya roghage
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuondoa sumu mwilini, ni njia mbalimbali ambazo uweza kutumika ili kuondoa sumu mwilini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kupungukiwa damu mwilini, ni ugonjwa unaotokana sana hasa kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano ingawa na kwa watu wazima.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu Rangi za mkojo na maana zake na mkojo mchafu
Soma Zaidi...Kifafa hakiambukizi na ugonjwa wa ubongo lakini kifafa pia hakiathiri akili au ubongo Ila kikiwa kifafa Cha kudumu na Cha nguvu ndio huweza kuadhiri. Pia Kuna kifafa Cha mimba na kifafa Cha kawaida.kifafa Cha mimba ndio kinahatari Sana kuliko Cha Kawaid
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa vijana
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...maumivu ya kichwa ni moja ya dalili za kiafya ambazo huashiria hali isiyo ya kawaida. hata hivyo maumivu ya kichwa yanaweza kutokea hata kama sio mgonjwa. Hapa nitakuletea sababu zinazopelekea kuumwa na kichwa mara kwa mara.Maumivu
Soma Zaidi...