Ijue dawa ya cephalosporin katika kupambana na bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya cephalosporin katika kupambana na bakteria, ni mojawapo ya kundi kati ya makundi ya kupambana na bakteria ambalo ufanya Kazi kama penicillin.

Fahamu kuhusu dawa ya cephalosporin .

1. Dawa hii ya cephalosporin katika kupambana na bakteria huwa kwenye magroup muhimu matatu ambayo ni kundi la kwanza Lina dawa ya cephalexin, Kundi la pili Lina dawa ya cefamandole na kundi la tatu Lina dawa ya ceftriaxone na celfdimir, makundi yote matatu ufanya Kazi kwa umoja na kuweza kupambana na bakteria na kutibu magonjwa mbalimbali kama tutakavyoona hapo mbeleni.

 

2. Magonjwa mbalimbali ambayo utibiwa na cephalosporin na makundi yake ni kuzuia maambukizi kwenye ngozi, yaani maambukizi yabayoambatana na viupele pamoja na miwasho, kuzuia maambukizi kwenye mifupa na kwennye joint, kuzuia maambukizi kwenye mfumo wa mkojo na maambukizi ya njia za mkojo kwa kitaamu huiitwa UTI, kuzuia maambukizi kwenye tumbo,pia kuzuia maambukizi kwenye sikio hasa ndani ya sikio.

 

3. Dawa hii inawezekana kupitia sehemu mbalimbali kama vile kwenye mdomo au sindano za matakoni na pajani au kwa wakati mwingine upitia kwenye mishipa ya damu , pia dawa hii ikishaingia kwenye mwili inawezekana kusambaa sehemu mbalimbali kama kwenye kondo la nyuma, kwenye maziwa kwa mama anayenyonyesha,na pia kweye maji maji ambayo yapo kwenye ubongo ambayo Kwa kitaamu huiitwa cerebral Spinal fluids.

 

4.pia dawa hii Kuna watu ambao hawapaswi kutumia na Kuna wale wanaopaswa kuitumia kwa taahadhari, ambao hawapaswi kutumia ni wale wenye alleji na cephalosporin na kwa  na wale wenye aleji Kali na penicillin, na wanaopaswa kuitumia kwa taahadhari ni wenye ugonjwa wa Figo wanapaswa kutumia china ya uangalizi maalumu au pengine wapunguziwe dozi, na wale wenye ugonjwa wa kisukari watumie chini ya uangalizi maalumu na kwa akina Mama wenye mimba na wanaonyonyesha wanapaswa kuitumia kwa taahadhari au kwa uangalizi Fulani.

 

5. Pia dawa hii Ina maudhi madogo madogo kwa watumiaji na maudhi hayo yakizidi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kubadilishiwaa dawa au kupewa huduma nyingine muhimu na maudhi hayo ni kama vile kizunguzungu na kutapika, maumivu ya tumbo na kichwa, upungufu wa damu kwa watumiaji.

 

6. Pia dawa hii haipaswi kutumiwa kiholela Bali utumika kulingana na wataalamu wa afya kwa sababu unaweza kutumia ukiwa nyumbani na hujui kama haipaswi kutumiwa atimaye unajiletea matatizo ya Bure.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/22/Thursday - 08:53:49 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 950


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-