Fahamu kuhusu dawa ya ALU au kwa lugha nyingine ni dawa ya mseto
Post hii inahusu zaidi dawa ya ALU ila kwa jina jingine huitwa dawa ya mseto,ni aina ya dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida.
Fahamu kuhusu dawa ya mseto au ALU.
1. Dawa hii ya ALU ni dawa ambayo utumika kutibu malaria ya kawaida, dawa hii ni muunganiko wa dawa mbili ambazo kwa kirefu zinaitwa Artemether lumefantrine, Artemether usimama kama A, na lumefantrine usimama kama LU kwa hiyo kwa ujumla utengeneza jina la ALU ambapo Artemether ina miligramu ishirini na lumefantrine ina miligramu mia ishirini kwa ujumla dawa hii huwa na jumla ya milligrams mia arobaini.
2. Kama tulivyotangulia kusema kwamba dawa hii utumika kutibu malaria ya kawaida, tunasema utibu malaria ya kawaida kwa sababu ya dalili zake kuwa za kawaida, dalili za malaria ya kawaida ni kama ifuatavyo maumivu kwenye jointi, maumivu ya kichwa, mwili kukosa nguvu, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo la kawaida, kuhisi baridi au kwa watu wengine kutetemeka , dalili hizi hazimfanyi mtu kushindwa kutembea na kufika hospitali na akipata vipimo na kukutwa na malaria ya kawaida anapatiwa vidonge vya ALU au mseto na anapona kabisa na kurudia hali yake ya kawaida.
3. Matumizi ya dawa hii utegemeza umri wa mtu na kilo za mtu, watu wenye kilo kuanzia tano mpaka kumi na tano utumia kidonge kimoja, kidonge cha kwanza ukitumia siku ya kwanza , kidogo cha pili baada ya masaa manane na vidonge vifuatavyo utumika asubuhi na jioni kwa kawaida dozi hiyo utumia siku tatu kama mtu anatumia vidonge kwa mda na kwa wakati.
4. Watu wenye kilo kuanzia kumi na tano mpaka ishirini na tano utumia vidonge viwili, yaani siku ya kuanza anameza vidonda viwili, baada ya masaa nane anameza vidonge vingine viwili na siku zifuatazo anameza vidonge viwili asubuhi na jioni mpaka siku tatu zinaisha. Yaani asubuhi viwili na jioni viwili.
5. Watu kuanzia kilo ishirini na tano mpaka thelathini na tano kwa kawaida umeza vidonge vitatu, yaani siku ya kwanza anameza vidonge vitatu, baada ya masaa manane vidonge vitatu, na anaanza kumeza asubuhi na jioni yaani asubuhi vidonge vitatu na jioni vidonge vitatu mpaka dozi inaisha.
6. Watu wenye kilo kuanzia thelathini na tano na kuendelea kwa kawaida umeza vidonge vinne, yaani siku ya kuanza kutumia dawa anameza vidonge vinne na baada ya masaa manane anameza vidonge vingine vinne na akimaliza hapo anameza vidonge asubuhi na jioni yaani asubuhi vinne na jioni vinne mpaka dozi inaisha , kwa kawa wakati wa kutumia dawa hizi ni vizuri kutumia maji mengi ya kunywa pamoja na kula kushiba kwa sababu kama mtu hajashiba dawa hizi hazifanyi kazi vizuri na uweza kumsumbua mtumiaji kwa hiyo ni vizuri kula na kushiba wakati wa kutumia dawa hizi.
7. Pia dawa hizi uweza juwa na maudhi madogo madogo kama vile kizunguzungu, kutapika, kuishiwa nguvu na pia kupenda kulala mda mwingi, hasa hasa maudhi haya uwapata watu wale ambao hawako na kushiba kabla ya kutumia dawa ni vizuri kabisa kula na kushiba ndipo utumia dawa, pia wakati wa kutumia dawa hizi ni vizuri na ni lazima kutumia dawa za kupunguza maumivu hasa hasa panadol na dawa nyingine ambazo ufanya kazi kama paracetamol.
8. Dawa hizi ya ALU haipaswi kutumiwa na akina mama wenye mimba na pia wale wenye mzio au aleji na dawa hizi , na pia ikiwa mtu anatumia dawa hizi na akatapika baada ya nusu saa kutumia anapaswa kurudia tena kwa sababu dawa haijafanya kazi.
9. Katika matumizi ya dawa hii ni vizuri kabisa kufuata taratibu za wataalamu wa afya ili kupata maelekezo sio kutumia kiholela kwa sababu unaweza kupata matatizo kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizi ya ALU.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 ai web app 👉3 web hosting 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Fahamu dawa ya kutibu maumivu ya mgongo (back none pain) na kiuno
Fahamu dawa ya back bone pain kwa matibabu ya mgongo, ni mojawapo ya dawa ambayo imependekezwa kutuliza maumivu ya mgongo.
Soma Zaidi...Dawa ya Isoniazid na kazi zake
Posti hii inahusu zaidi dawa ya lsoniazid nA kazi zake, ni dawa ambayo inasaidia kutibu kifua kikuu kati ya madawa yaliyoteuliwa na kuwa na sifa ya kutibu kifua kikuu.
Soma Zaidi...Kazi ya Dawa ya salbutamol
Posti hii inahusu dawa ya salbutamol na kazi yake ya kutibu ugonjwa wa Asthma, ni dawa mojawapo ambayo imetumia na watu wengi na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo zifuatazo ni kazi ya Dawa hii ya salbutamol katika kutibu Asthma.
Soma Zaidi...Dawa ya kuzuia kuathirika kwa watu walio hatarini kupata VVU
Somo hili linakwenda kukuletea dawa ya kuzuia kuathirika kwa watu walio hatarini kupata VVU
Soma Zaidi...Dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria
Posti hii inahusu zaidi dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ,ni dawa ambayo utumiwa na watu wengi kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria.
Soma Zaidi...