Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu
1. Dawa hii kwa kawaida usaidia kupambana na maambukizi ya bakteria kwenye sehemu mbalimbali za mwili kama vile maambukizi kwenye sehemu ya ndani na ya nje ya sikio, matibabu ya nimonia, kuzuia maambukizi kwenye mkojo kwa lugha inayoeleweka ni UTI kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mfumo wa upumuaji, maambukizi kwenye mifupa ambayo Kwa kitaamu huiitwa osteomyelitis, matibabu kwenye vidonda vilivyoungua, matibabu ya gonorrhea na pia kwenye tumbo kama Kuna maambukizi ya bakteria.
2. Pia dawa hii ufanya Kazi kwa kupitiakwenye mmengenyo wa chakula na pia uingia kwenye mzunguko wa damu na kufanya kazi ya kutibu au kupambana na bakteria,Inapambana na bakteria kwa kuzuia kuzaliana kwa bakteria na wale waliokwishazaliana Wana dumaa na hawaendelea kukua hali inayosababisha matibabu yake kufanikiwa zaidi na pia bakteria hao hawawezi kuzaliana tena na pia dawa hii uingilia kwenye nuklia ya bakteria na kuharibu Kila kitu ndani ya seli ya ya bakteria.
3.Dawa hii mara nyingi huwa kwenye mfumo wa vidonge kwa hiyo matumizi yake utegemea wataalamu wa afya , vile vile dawa hii utumiwa na watu mbalimbali ila Kuna watu ambao hawapaswi kuitumia hasa wale wenye aleji na dawa hii pamoja na wale wenye aleji na sulfa na wenyewe hawapaswi kutumia, pia Kuna wale wenye ugonjwa wa maumivu ya kichwa Wanaoaswa kuitumia kwa taahadhari kwa sababu dawa hii Ina maudhi ya kuwepo kwa maumivu ya kichwa kwa watumiaji kwa hiyo wakiendelea kuitumia itawafanya maumivu ya kichwa kuongezeka.
4. Vile vile dawa hii Ina maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea kwa watumiaji maudhi hayo ni kama kuwashwa kwenye mwili mzima na pengine kutokea kwa vi upele vidogo vidogo ambavyo uendelea kuwasha tu, pamoja na hayo Kuna hali ya kichefuchefu ujitokeza, kutapika na maumivu ya tumbo, pia Kuna upungufu w hamu ya kula uweza kujitokeza,na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara mpaka dawa itakapoisha mwilini.
5.kutokana na kuwepo kwa maudhi madogo madogo ni kawaida kwa watumiaji wa dawa ila maumivu hayo yakizidi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kubadilishiwaa dawa au kupewa dawa ya kutuliza hayo matokeo ya dawa, pia kwa wale ambao huwa na ugonjwa wa maumivu ya kichwa ni vizuri kabisa kuwepo kwenye uangalizi wa wataalamu wa afya Ili kuweza kuepuka madhara mengine ambayo yanaweza kujitokeza.
6. Pia dawa hii haipaswi kutumika kiholela inapaswa kutumiwa kulingana na wataalamu wa afya kwa sababu mda mwingine dawa hii Ina matokeo mbalimbali ambayo yakitokea kwa mtu akiwa nyumbani matatizo yanaweza kuwa magumu kidogo, kwa hiyo kuwaona wataalamu wa afya ni jambo la muhimu kwq sababu unakuwa na uhakika wa kutosha.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya phenoxy-methyl penicillin ambayo upambana na aina ya bakteria ambao utoa sumu Ili kuzuia dawa isifanye kazi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...Maumivu ya mgongo hutokea sana kwa wajawazito. Ijapokuwa ni hali ya usumbufu sana ila hakikisha hautumii madawa kiholela kutoka maduka ya dawa ama miti shamba. Kwani ukikisea kidogobinawezabhatarisha afya ya mtoto
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya hydralazine katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii imetoka kwenye kundi la vasodilators, na pia usaidia sana kwenye matibabu ya magonjwa ya moyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea dawa ya kuzuia kuathirika kwa watu walio hatarini kupata VVU
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya furosemide ni mojawapo ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la diuretics na kwa jina linguine huitwa lasix
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa na maambukizi na mashambulizi ya virusi na bakteria kwenye sehemu za siri ama via vya uzazi?. Posti hii inakwenda kuupa ushauri.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya loperamide ni dawa ambayo inazuia kuharisha ni dawa inayofanya kazi kuanzia kwenye utumbo na pia usaidia kutuliza maumivu ya tumbo
Soma Zaidi...