SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.
SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.
Hapa tutaona dua iliyo katika sura ambayo Allah ataijibu. Dua zenye kujibia wakati mwingine zina sura yake na sifa zake katika maneno na matamshi. Hebu tuone sifa hizo.
1.Dua ya nabii Yunusi. Mwenye kuomba dua na akatumia maneno aliyoyasema nabii Yunusi (amani ishuke juu yake) dua hii ni yenye kujibiwa. Amesema mtume صلّي الله عليه وسلّم “dua ya nabii Yunus pindi alipokuwa kwenye tumbo la samaki (aliseme) ‘LAA LILAAHA ILLAA ANTA, SUBHAANAKA INII KUNTU MINADHWALIMIINA’ hakika hataomba mtu muislamu dua kwa kutumia maneno haya kitu chochote isipokuwa atajibiwa na Allah”. (amepokea tirmidh).
2.Kuomba dua kwa kutumia jina la Allah lililo kubwa. Allah ana majina mengi na mazuri. Lakini katika majina hayo lipo ambalo ni kubwa na ukiomba dua kwalo lakina utajibiwa. Kwa ufupi ni kuwa jina hili limefichwa na hakina yeyote anayelijuwa. Ila mtume ametowa ishara ya kuonesha wapi linapatikana na maneno gani mtu atumie kulipata jina hilo.
Amesema mtume صلّي الله عليه وسلّم “jina kubwa la Allah lipo kwenye aya sita za mwisho za surat hashri. (amepokea Dilamy kutoka kwa Ibn ‘Abas). Pia katika mapokezi mengine ya Tabrany kutoka kwa Ibn ‘Abas kuwa mtume amesema jina kubwa lipo kwenye aya ya 20 ya surat al-imran. Na pia zipo hadithi nyingi sana zinazoashiri wapi jina hilo lipo. Nitaleta chache tuu.
i) Aisha رضىالله عنها aliomba dua hii “ ALLAHUMMA INII AD’UKA LLAHA WA-AD’UKAR-RAHMANA, WA-AD’UKAL-BARRAR-RAHIIMA, WA-AD’UKA BIASMAAIKAL-HUSNAA KULLIHAA MAA ‘ALIMTU WAMAA LAM A’ALAM AN TAGHFIRA LII WATARHAMNII” Mtume akacheka kisha akasema “hakika jina kubwa lipo ndani ya dua hii. (amepokea Ibn Maajah kutoka kwa ‘Aisha) hadithi hii ni ndefu nimeikatisha na kuchukua hiyo dyua tu.
ii)hadithi ya Anasرضىالله عنهkuwa”
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم الْمَسْجِدَ وَرَجُلٌ قَدْ صَلَّى وَهُوَ يَدْعُو وَيَقُولُ فِي دُعَائِهِ اللَّهُمَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ الْمَنَّانُ بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ . فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " تَدْرُونَ بِمَ دَعَا اللَّهَ دَعَا اللَّهَ بِاسْمِهِ الأَعْظَمِ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ وَإِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى "amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa alikuwa amekaa na mtume صلّي الله عليه وسلّم wamekaa msikitini na kulikuwa na mtu mmoja anaswali kisha akaomba dua kwa kusema “ ALLAHUMMA ANNII AS-ALUKA BIANNALAKAL-HAMDA, LAA ILAAHA ILLA ANTAL-MANNAANU BADI’US-SAMAAWATI WAL-ARDH YAA DHALJALALI WAL-IKRAM YAA HAYYU YAA QAYYUUM” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo anapoombwa kwalo atajibu”. (amepokea tirmidh kwa isnad gharib).
iii)amesimulia Abdillah Ibn Buraydah رضىالله عنه kutoka kwa baba yake kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم alimsikia mtu mmoja akisema “ALLAHUMMA INNIASALUKA BIAN-ASHHADU ANNAKA ANTALLAHU LAA ILAAHA ILLA ANTA. AL-AHADUS-SWAMADUL-LADHII LAMYALID WALAM YUULAD, WALAM YAKUN LAHU KUFWAN AHAD” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم hakika umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo akiombwa hutoa na akiombwa dua hujibu. (amesimulia Abuu Daud,tirmidh,Ibn Maajah na Ibn Hiban).
Iv). Mtume amesema اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الآيَتَيْنِ {وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ} وَفَاتِحَةِ سُورَةِ آلِ عِمْرَانَ "Jina kubwa la Allah linapatikana kwenye aya hizi‘ waillahukum ilahu wahidu laa ilaaha illa huwar-rahmanir-rahiim’ na mwanzoni mwa surat al ‘Imran
3.dua ya Mtume صلّي الله عليه وسلّم ni yenye kujibiwa. " لِكُلِّ نَبِيٍّ دَعْوَةٌ مُسْتَجَابَةٌ وَإِنِّي اخْتَبَأْتُ دَعْوَتِي شَفَاعَةً لأُمَّتِي وَهِيَ نَائِلَةٌ إِنْ شَاءَ اللَّهُ مَنْ مَاتَ مِنْهُمْ لاَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا " Katika hadithisahihi mtume amesema Nabii yeyote ameomba dua yake na akajibiwa. Na nikaifanya dua yangu mimi ni shifaa kwa umati wangu sikku ya qiama. (amepokea Bukhari, Muslim na tirmidh kutoka kwa Anas).
4.Dua wakati wa raha hujibiwa wakati wa shida. Hii ni sifa ya dua yenye kujibiwa mbayo watu wengi hatujui. Nikuwa pindi unapopata neema na raha hapo ndipo pa kumuomba Allah na Allah atakujibu wakati unapopata matatizo kwa kukufariji na kukuondlea matatizo. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَسْتَجِيبَ اللَّهُ لَهُ عِنْدَ الشَّدَائِدِ وَالْكُرَبِ فَلْيُكْثِرِ الدُّعَاءَ فِي الرَّخَاءِ " “mwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa raha”. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib).
Na katika mapokezi mengine amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم
" مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَسْتَجِيبَ اللَّهُ لَهُ عِنْدَ الشَّدَائِدِ وَالْكُرَبِ فَلْيُكْثِرِ الدُّعَاءَ فِي الرَّخَاءِ " “Mwenye kupenda kujibiwa dua zake wakati wa shida na taabu basi na azidishe dua wakati wa raha” (amepokea tirmidh)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa.
Soma Zaidi...Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa.
Soma Zaidi...Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...Hapa utakwendabkuijuwabhistoria ya uandishi wa hadithi. Pia utaijuwa sababu iliyopelekea uandishi wa hadithi kuwa mdogo .
Soma Zaidi...Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu
Soma Zaidi...