ADABU ZA KUOMBA DUA.
ADABU ZA KUOMBA DUA.
1.kuelekea qibla. Amesimulia Abdallah Ibn Zayd رضىالله عنه kuwa “alitoka Mtume صلّي الله عليه وسلّم kwenda kuomba dua ya mvua akaelekea kibla”. (amepokea Bukhari).
2.Kunyanyua mikono miwili juu. Amesimulia Abuu Musa رضىالله عنه kuwa “aliomba Mtume صلّي الله عليه وسلّم dua akanyanyua mikono yake mpaka nikaona weupe wa kwapa lake” (amepokea Bukhari). Na amesimulia Ibn ‘Abas kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " إِذَا دَعَوْتَ اللَّهَ فَادْعُ بِبُطُونِ كَفَّيْكَ وَلاَ تَدْعُ بِظُهُورِهِمَا فَإِذَا فَرَغْتَ فَامْسَحْ بِهِمَا وَجْهَكَ “muombeni Allah kwa matumbo ya viganya vyenu, wala msimuombe kwa migongo ya viganja vyenu.…”. (amepokea Abuu Daud na Bayhaqiy).
3.Kuanza dua kwa kwa kumsifu Allah na kumshukuru (kama kusema alhamdu lillah ….) na kumswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم. Amesimulia ‘Abdullah Ibn Mas’ud رضىالله عنه kuwa nilikuwa nikiswali, wakati Mtume yupo na Abuubakar na ‘Umar, basi nilipokaa nikaanza kumshukuru Allah na kumsifu na nikamswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha nikajiombea dua, akasema mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘omba utapewa, omba utapewa’”. (amepokea tirmidh kwa isnad sahih). Na katika masimulizi ya Fudailah Ibn ‘Ubayd رضىالله عنه amesema “hakika amefundisha mtume صلّي الله عليه وسلّم uma wake jinsi ya kuomba dua akasema ‘pindi anapoomba dua mmoja wenu basi aanze na tahmid (kumshukuru Allah) na thanaai (kumsifu Allah) kisha amswalie Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha aombe chochote anachotaka’” " إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ اللَّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ثُمَّ لِيُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ لِيَدْعُ بَعْدُ بِمَا شَاءَ " (amepokea Abuu Daud, tirmidh, Ibn Hiban na baihaqy).
4.Kuanza kuomba dua kwa kujiombea mwenyewe. Kwa anayetaka kumuombea mtu mwingine dua anatakiwa aanze na kujiombea mwenyewe. Amesimulia Ubaiya Ibn K’ab رضىالله عنه kuwa عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا ذَكَرَ أَحَدًا فَدَعَا لَهُ بَدَأَ بِنَفْسِهِ “alikuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم anapomkumbuka mtu na akataka kumuombea dua huanza kwa kujiombea mwenyewe kwanza.” (amepokea tirmidh kwa isnad sahih).
5.Kurudia rudia katika kuomba na kusisitiza maombi yako. Ila usiharakishe majibu kutaka kujibiwa haraka hata ukawa unamlaumu Allah. Amesimulia Abdallah ibn Ms’ud رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم anapenda kuomba mara tatutatu na (akawa) anaomba istighfar (msamaha) mara tatutatu. (amepokea Abu Daud kwa isnad salih).
6.Kuwa na yaqini juu ya kujibiwa na kujiepusha na yaliyo haramu. Mtu anatakiwa asiwe na shaka juu ya kujibiwa dua yake. Amesimulia Abuu Hurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " ادْعُوا اللَّهَ وَأَنْتُمْ مُوقِنُونَ بِالإِجَابَةِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ لاَ يَسْتَجِيبُ دُعَاءً مِنْ قَلْبٍ غَافِلٍ لاَهٍ "
“muombeni Allah mkiwa na yakini juu ya kujibiwa na jueni kuwa Allah hakubali dua ya mtu ambaye moyo wake umeghafilika naye. (amepokea Tirmidh na Alhaakim).
7.Usiharakishe kujibiwa. Isitokee mtu akawa na haraka ya kutaka maombi yake yajibiwe kama anavyotaka yeye kwa haraka hata akawa analaumu. Amesemulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema
" يُسْتَجَابُ لأَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ يَقُولُ دَعَوْتُ فَلَمْ يُسْتَجَبْ لِي " “atajibiwa (dua yake ) mmoja wenu maadam hajaharakisha (kujibiwa) akawa anasema nimeomba na wala sijajibiwa”. (amepokea Bukhari na Muslim). Na katika masimulizi mengine ya Abuuhrairah kuwa mtume amesema “hataacha mja kujibiwa dua yake maadam hajaomba madhamdhi au kukata udugu”. (amepokea Muslim na Abuu Daud). Hii ina maana dua itajibiwa tu ila isiwe ya kuomba madhambi au kukata udugu.
8.Kuitikia “aamiin”. Mwenye kuomba dua basi aitikie “aamiin” eidha awe mwenyewe pekee au yupo na kundi la watu. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم “atakapoomba dua mmoja wenu basi na aitikie ‘aamiin’ mwenyewe’”. (amepokea Ibn ‘Adiy).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 660
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Kitau cha Fiqh
Uislamu ni Nasaha (kunasihiana) kwa Mwenyezi Mungu, Kitabu chake Mtume wake , Viongozi na waislamu wote
عَنْ أَبِي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بْنِ أَوْسٍ الدَّارِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: "الدِّينُ النَّصِ?... Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...
Nafasi ya Sunnah (suna) katika Uislamu.
Hapa utajifunza nafasi ya kufuata suna katika Uislamu Soma Zaidi...
ni nyakati zipi ambazo dua hukubaliwa kwa haraka?
Dua ni moja ya ibada ambazo zinamfanya mja awe karibu na Mweznyezi Mungu. Allah amesisitiza tumuombe dua kwa shida zetu zote, pia akaahidi kuwa atatujibu maombi yetu muda wowote tutakao muomba. Sasa ni zipi nyakati nzuri zaidi kuomb adua? Soma Zaidi...
kuwa muaminifu na kuchunga Amana
Uaminifu ni uchungaji wa amana. Soma Zaidi...
DUA 94 - 114
DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 94. Soma Zaidi...
Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 6: ubainifu wa halali na haramu
Post hii inakwenda kukupa tahadhari juu ya mambo ya halali na mambo ya haramu. Soma Zaidi...
Hadithi Ya 39: Allaah Amewasamehe Umma Wake Kukosea Na Kusahau Kwa Ajili Yake ( Mtume صلى الله عليه وسلم )
Soma Zaidi...
KATU USITAMANI MAUTI (KIFO) YAANI KUFA, HATA UKIWA NA MARADHI AMA UKIWA MCHAMUNGU UKIWA NI MUOVU MTENDA MADHAMBI MAKUBWA NA MADOGO
Soma Zaidi...
kujiepusha na uongo na sifa za uongo
Uwongo ni kinyume cha ukweli. Soma Zaidi...