image

Dua za kuondoa wasiwasi, woga na kujikinga na uchawi, na mashetani

Post hii itakufundisha dua za kuomba wakati wa woga, wasiwasi na kujikinga na wachawi na mashetani


DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI
1.Kutaka hifadha dhidi ya vitimbi vya shetani na wasiwasi ni jambo ambalo Allah ametuamrisha kulifanya. Hivi pia ndivyo ambavyo mtume wetu alikuwa akifanya. Amesema Allah (s.w): “Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.” Quran surat al-an-muumin aya ya 97-98).

Hivyo hapa tunajifunza kuwa ukitaka kujikinga na wasiwasi na vitimbi vya shetani unatakiwa useme maneno haya aliyotufundisha Allah (s.w) ambayo ni kusema “RABBI A’UUDHUBIKA MIN-HAMAZAATISH-SHAYAATWIN, WA A-’UUDHUBIKA AN-YAHDUDUUN” katika dua hii herufi D hap utaona imepigiwa msitari. Hiyo ni herufi ض ambayo hainna mwenzie kwenye kiswahili. Fatilia kwa wasomi wakufundishe inavyosomwa. Kwa kiarabu dua hii ni hii chukua msahafu wako fungua surat al-muumin aya ya 97-98 وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ ﴿٩٧﴾ وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ ﴿٩٨﴾

2.mwenye kutaka kuikinga nyumba yake na mwili wake pamoja na ahali zake dhidi ya uchawi na majini masi asome surat al-baqara japo mara moja kila baada ya siku tatu, au asome ayat al-qursiy na aya mbili za mwisho za surat al-baqara japo mara moja kwa siku au asubhi na jioni. Au asome sura al-mu’awidhatayn yaani surat al-falaq na surat an-na sura hizi asome pamoja na surat al-ikhlas kwa utaratibu aloufanya Mtume (s.a.w), tutauzungumza hapa. Hebu tuone kwanza faida za sura hizi kwa mapokezi ya hadithi zilizo sahihi

1.Surat al-fatiha.
Amesimulia Ibn ‘Abas kuwa “wakati ambao jibril alikuwa amekaa na Mtume akasikia sauti ya mlango uliofunguliwa juu yake akanyanyu kichwa chake kisha akasema “hiyo ni nsauti ya mlango uliopo mbinguni umefunguliwa siku ya leo, na katu haujawahi kufunguliwa ila ni leo tu (ndio mara ya kwanza kufunguliwa).

Basi akashuka Malaika kutoka kwenye mlango huu akasema (Jibril) huyu ni malaika ameshuka duniani na hajawahi kushuka kamwe ila ni leo tu akatoa salamu (malaika huyo) kisha akasema (kumwambia mtume) tuo habari za furaha kwa nuru mbili ulizopewa na hakuwahi kupewa mtume yeyote kabla yako kamwe (ambazo ni) surat al-fatiha na aya za mwisho za surat al-baqarah hatusoma herufi yeyote isipokuwa utapewa” (amepokea Muslim). Amesema Mtume “surat al-fatiha ni dawa ya kila gonjwa” amepokea Bayhaqiy)

2.surat al-baqarah Amesema Mtume “…Mwenye kuisoma katika nyumba yake usiku hatoingia shetani nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu, na mwenye kuisoma mchana hatoingia shetani nyumba hiyo kwa michana mitatu” (amepokea Ibn hiban, tabrany na Bayhaqiy). 3.ayat al-qursiy.
Amesema Mtume “katika surat al-baqarah kuna aya iliyobora kuliko aya zote haitasomwa aya hiyo kwenye nyumba yenye shetani ila atatoka kwenye nyumba hiyo, (aya hiyo ni) ayat al-kursy) (amepokea Al-Haakim na Bayhaqiy)

3.aya za mwisho za surat al-baqarah
Amesema Mtume hakika Allah ameimalizia surat al-baqarah kwa aya zilizo tukufu (zilizotoka) kwenye hazina chini ya ‘arshi basi jifundisheni aya hizo na muwafundishe wake zenu na watoto wenu. Kwani mna ndani ya aya hizo dua, qiraa na dua” (amepokea Al-Haakim kutoka kwa Abuu Dhari).
Pia Amesema mtume “aya mbili za mwisho za surat al-baqarah mwenye kuzisoma usiku zitamtosheleza” (amepokea bukhari,Muslim,Ahmad na Ibn Maajah kutoka kwa ibnmas’ud)

4.Suratul ikhlas, nasi na falaq
Amesimulia ‘Abdallah Ibnhabib kuwa Mtume amesema “QUL HUWA LLAHU AHADU na mu’awadhatayn (qul a’udhu birabin-nasi na qul a’udhu birabil-falaq) (mwenye kuzisoma ) asubuhi na jioni zinatosheleza kwa kila kitu.(amepokea ahmad, Tirmidh na Nisai).

Hizi ni baadhi tu ya sura mahususi ambazo Mtume alikuwa akiwasisitiza masahaba zake wazisome. Sura nyingine ni kama al-imran, al-an’am, al-israa, al-kahaf, surat musabahat(sura zilizoanzwa na tasbih nnazo zipo saba), surat al-mulkk, surat ar-rahman, surat al-waqi’a, surat al-zalzala, surat at-takathur, surat al-fiyl, surat al-kafiruun, surat yasin n.k. Kupata faida zaidi ya sura hizi download App yetu iiitwayo darsa za quran, utafaidiza zaidi.

Sasa hebu tuone namna ambavyo Mtume (s.a.w) katika maisha yake tunapata mafunzo alivyokuwa akitumia sura hizi kama ni kinga na dawa kwa mambo mbalimbali:-

1.Mtume (s.a.w) amesema:”mwenye kusoma aya kumi nne za mwanzo katika surat al-baqarah, na ayat al-qursiy na aya mbili baada ya aya hii, na aya mbili zilizo mwishoni mwa surat al-baqarah hataingia katika nyumba hiyo shetani mpaka asubuhi” (amepokea hadithi tabrany na Alhakim akaisahihisha).

2.Mtume alikuwa anapokwenda kulala anasoma sura na aya hizi, kwa utaratibu huu:- Alikuwa Mtume (s.a.w) akienda kulala usiku, akiweka pamoja viganja vyake kisha akivipulizia na akivisomea suratul-Ikhlas, suratul Falaq na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani, usoni na mbele (akifanya hivyo mara tatu.) (Bukhari na Muslimu)

Mtume (s.a.w) amesema: "Ukienda kulala soma Ayatulkursiyyu kwani Allah ataendelea kukuhifadhi, wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi." (Al-Bukhari)

Mwenyezi Mungu, hakuna Mola ila yeye, ndiye mwenye uhai wa milele, msimamia kila jambo. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni vyake (peke yake vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na (yaliyo) nyuma yao; wala (hao viumbe) hawalijui lolote katika ilimu yake ila kwa alipendalo. Enzi yake imeenea mbinguni na ardhini, wala kuvilinda hivyo hakumshindi; Na yeye (pekee) ndiye aliye juu na ndiye aliye mkuu." (2:255)

Alikuwa Mtume (s.a.w) akitaka kulala, anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake, kisha anasema: "Allahumma qiniy a'dhaabaka yaumatab-a'thu i'baadaka." "Ee! Allah nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakapowafufua waja wako."

Pia Mtume (s.a.w) wakati wa kulala alikuwa akisema: “Allahumma Bismika amuutu wa-ahyaa. “Kwa jina lako, Ee Allah ninakufa na nina kuwa hai." uzi na ndiye Mwenye hikima (2:32)

3.Dua pindi uonaposhetani au unapotishwa na shetani
Ikitokea Mtu ameona shetani au ametishwa na shetani anatakiwa kuleta isti’adha na asema “A’UDHU BILLAHI MINKA” mara tatu kisha aseme “AL-’ANUKA BILA’ANATIL-LLAHI TAAMMAH” mara tatu. Hakika shetani anakimbia ukisema maneno hayo. Hatika mapokezi ukimuona shetani akikutisha au hakukutisha soma adhana hakika shetani hukimbia adhana. Katika hadithi alopokea muslim mtume (s.a.w) amesema “hakika shetani hukimbia pindi adhana ya swala inaposomwa”

Kwa ufupi zipo dua nyingi lakini qurani inatosha kabisa kufanya kila tunalolitaka. Qurani inatosha kuwa kinga ya wachawi, majini na vijicho. Dua zaidi tumeziwekakwenye App yetu iitwayo swala na dua. Tumeweka kule kwa kuhofia kuirefusha app ii kuwa ndefu zaidi. Tunasikiliza mawazo yenu wasomaji zaidi. Kuiboresha App hii. Darsa hii imewekwa kutegemea na michango na maoni ya masomaji wetu. Tutaendelea kufanya hivu zaidi.


 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 4464


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Historia ya uandishi wa Hadithi, na ni kwa nini wakati wa Mtunme hakukuwa na uandishibmkubwa wa hadithi
Hapa utakwendabkuijuwabhistoria ya uandishi wa hadithi. Pia utaijuwa sababu iliyopelekea uandishi wa hadithi kuwa mdogo . Soma Zaidi...

Fadhila za udhu yaani faida za udhu
Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu Soma Zaidi...

Dua za wakati wa shida na taabu
Hizi ni Dua ambazo unatakiwa uziombe wakati wa shida na taabu Soma Zaidi...

Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 42: Ewe Mwana Wa Adam, Utakaponiomba Na Kuweka Matumaini Kwangu Basi Nitakusamehe
Soma Zaidi...

DUA 120
Soma Zaidi...

Matendo ('amal) hulipwa kutokana na nia (makusudio)
Soma Zaidi...

DUA 120
Soma Zaidi...

DUA ZENYE MANENO HAYA HUJIBIWA
SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA. Soma Zaidi...

DUA YA 1 - 10
1. Soma Zaidi...

DUA 85 - 93
SWALA YA MTUME 85. Soma Zaidi...

Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 2: Ujio wa Jibril kwa Mtume (s.a.w)
Hii ni hadithi ya pili katika kitabu cha Arbain Nawawiy Soma Zaidi...