DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA.
DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA.
Hashira ni katika matendo ambayo shetani anayapenda sana yatokee kwa mwadadamu. Kwa sababu ya hasira maovu mengine huenda yakatokea kama matusi, kupigana, vifo na mengineyo mengi. Uislamu kama dini iliyokamilika imetowa muongozo mzima juu ya namna ya kukabiliana na hali ya hasira pindi inapotokea. Katika makala hii tunakwenda kuona njia za kukabiliana na hali ya hasira pindi inapotokea.
Njia za kuzuia Hasira
1.Kumlani shetani kwa kusema ‘’a’udhubillahi minashaytwanir- rajiim”:
Katika hadithi iliyosimuliwa na Sulayman Ibn Sard amesema: “nilikuwa nimekaa na Mtume (s.a.w), na kulikuwa na watu wawili wanagombana. Mmoja uso umekuwa mwekundu kwa hasira na mishipa ya shingo imemsimama. Mtume (s.a.s) akasema, ‘ninayajuwa maneno ambayo kama atayasema, hasira zote alizo nazo zitaondoka. Kama atasema “a’udhubillahi minash-shaytwaanir- rajiim” hasira zake zote zitaondoka. (amepokea BUkhari)
2.kubakia kimya
Kubakia kimya wakati wa kuwa na hasira ni jambo la busara, kwani ukiendelea kubakia kimya ndio hasira zitatulia. Amesema Mtume (s.a.s) “kama mmoja wenu atapatwa na hasira na abakie kimya (Amepokea Ahmad).
3.Kutokutembea:
Hasira zikitokea kama umesimama usiendelee kwenda au kusimama kwanza kaa chini. Amesema Mtume (s.a.s) “kama mmoja wenu amepatwa na hasira na akiwa amesimama basi na akae chini, hasira zake zitaondoka, na kama hazitaondoka basi na alale” (Amepokea Ahmad).
Kwa ufupi zipo njia nyingi ila hizi tatu ndio nitaishia kwenye makala hii. Tufahamu kuwa kumlani shetani ni njia ya kumkimbiza kwani yeye ndie anayesababisha hasira. Ni vyema ukachukuwa Udhu unapokuwa na hasira na kumlani shetani kwa wingi. Kubakia kimya wakati wa hasira, kukaa kama umesiamama ama kulala ni katika njia za kuondoa hasira
Umeionaje Makala hii.. ?
huu ni mwanzo wa kitabu hiki cha Matn arbaina Naway
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukufundisha dua za kuomba wakati wa kuwa na maumivu kwenye mwili wako.
Soma Zaidi...Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...