KUKUSANYIKA KATIKA DUA. Ni jambo la kupendeza kuomba dua mkiwa kwenye kundi. Zipo dua ambazo siku zote zinaombwa watu wakikusanyika kama dua ya kuomba mvua. Kukusanyika kwenye dua ni sunnah katika sunnah zingine. Ijulikane kuwa pindi mtu akiomba dua kisha wengine wakaitikia aamiin huenda katika waloitikia akawepo walii wa Allah ambae ikawa sababu ya dua kujibiwa. Pia watu waliokuwepo kwenye kundi aombe mmoja na wengine waitikie aamiin na wanyanyue mikono yao. Maswahaba Allah awaridhie walikiwa wakiombeana dua na walikuwa pia wakikusanyika kayika kuomba dua. Mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa pia akiwahimiza maswahaba wake kuwa katika kundi wanapoomba dua na wengine waitikie aamiin. Amesimulia Habiib Ibn Salamah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “halikusanyiki kundi la watu na wakaomba dua wengine na wengine wakaitikia ‘aamiin’ isipokuwa Allah ataijibu dua hiyo”. (amepokea tbrany, Bayhaqy na Alhaakim).