HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
1.Dua ya kumuombea aliye mbali. Chukulia mfano una ndugu yako yupo nchi nyingine ama mji mwingine kisha ukamkumbuka na ukataka kumuombea dua, basi dua hii itajibiwa tu. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua iliyo nyepesi (na haraka ) kujibiwa ni dua ya mtu kumuombea aliye mbali” (amepokea Abuu Daud na Tirmidh kwa isnad sahihi). Pia amesimulia Abuu Dardaa رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “dua ya mtu muislamu ni yenye kujibiwa anapomuombea ndugu yake aliye mbali. Juu ya kichwa chake kuna Malaika anaitikia ‘aamiin’ na wewe upate mfano wa wake”. (amepokea Ahmd na Muslim).
2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa. Hali za watu watatu hawa wakiomba dua Allah atajibu dua zao bila ya shaka. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema
" ثَلاَثُ دَعَوَاتٍ يُسْتَجَابُ لَهُنَّ لاَ شَكَّ فِيهِنَّ دَعْوَةُ الْمَظْلُومِ وَدَعْوَةُ الْمُسَافِرِ وَدَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ
3.“dua za watu watatu (hawa) ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa”. (amepokea Abuu Daud, Ahmad na Tirmidh kwa sanad sahihi).
4.Dua ya mwenye swaum (funga), imamu muadilifu, na mwenye kudhulumiwa. Watu hawa dua zao zitajibiwa tu, kingozi muadilifu, mtu aliyekuwa kwenye funga na kabla hajafuturu na mtu aliyedhulumiwa. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم watu watatu dua zao hazirudi: mwenye funga mpaka afutauru, imamu muadilifu (kiongozi muadilifu), na mwenye kudhulumiwa.…….” (amepokea tirmidh kwa isnad sahihi).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 385
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Kitabu cha Afya
Hadithi Ya 25: Wenye Mali Wameondoka Na Fungu (jaza) Kubwa
Soma Zaidi...
AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...
AINA ZA HADITHI
Aina za HadithKuna aina kuu mbili za Hadith- (a) Hadith Nabawiyyi. Soma Zaidi...
DUA 113 - 126
DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu “LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU. Soma Zaidi...
Hadithi Ya 23: Tohara Ni Nusu Ya Imaan
Soma Zaidi...
Vyanzo vitano vya elimu zote duniani: Chanzo cha Elimu ni Allah (s.w)
Kama tunavyojifunza katika surat ‘Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s. Soma Zaidi...
Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 3: Nguzo za uislamu
Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu Soma Zaidi...
kujiepusha na uongo na sifa za uongo
Uwongo ni kinyume cha ukweli. Soma Zaidi...
Hadithi Ya 29: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote
Soma Zaidi...
NYAKATI AMBAZO DUA HUJIBIWA
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA. Soma Zaidi...
Hadithi Ya 22: Je, Nikiswali Swalah Za Fardhi, Nikafunga Ramadhaan
Soma Zaidi...