51.
51.34.Dua ya kupanda mnyama/chombo cha usafiri โBismillah wal-hamdulillahi, sub-haanalladhiy sakhkharalanaa haadhaa wamaa kunnaalahu muq-riniyna wainna ilaa rabbinaa la mun-qalibuuna.โKwa jina la Allah na sifa zote ni za Allah. Utukufu ni wa yule aliyetutiishia kipando hiki, tusingeweza kukitumia kwa uwezo wetu wenyewe, na kwa Mola wetu ndio marejeo.
52.Dua ya Safari โAllahu akbaru, Allah akbaru, Allahu akbaru, sub-haana lladhiy sakh-kharalanaa hadhaa wamakunnaa lahu muqriniyna, wainnaailaa rabbinna lamunqalibuuna. Allahumma innaa nas-aluka fiy safarinaa hadhal-birri wa-ttaqwa, waminal-a'mali maatar-dhwaa, Allahumma hawwin a'laynaa safaranaa hadha wat-wi a'nnaa budahu, Allahuumma antasw-swaahibu fiy ssafari, wal-khaliyfatu fiyl-ahli. โAllah ni mkubwa, Allah ni mkubwa, Allah ni mkubwa, ametakasika ambaye ametudhalilishia sisi hiki (chombo au mnyama), na hatukuwa sisi kwako ni wenye uwezo, na sisi kwa Mola wetu tutarejeshwa. Ee Allah, hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na ucha Mungu, na katika matendo unayoridhia, Ee, Allah ifanye nyepesi safari yetu hii na ufupishe umbali wake. Ee Allah, wewe ndie mwenzangu katika safari na mchungaji wa familia yangu.
53.Dua ya kupokea habari ya kufurahisha โAl-hamdulillahilladhiy bina-a'matihi tatimmu sw-swaalihaatu." โShukurani zote anastahiki Allah ambaye kwa neema yake hizi nzuri imekamilika."
54.Dua ya kupokea habari za kuhuzunisha โAl-hamdulillahi a'laa kulli haali" โShukurani zote anastahiki Allah kwa hali zote."
55.Dua ya kuingia sokoni โLaa illaaha illa llaahu wah-dahu laashariikalahu, lahul-mulku walahul-hamdu, yuh-yi' wayumiitu wahuwa hayyun laa yamuutu wahuwa a'laa kullishay-in qadiiru." โHakuna Mola ila Allah aliye mpweke, hana mshirika, ni wake ufalme,na ni zake sifa njema, anahuisha na anafisha, naye ni hai asiyekufa, kheri iko mikononi mwake, na yeye juu ya kila kitu ni muweza."
56.Ubora wa kusalimiana Mtume (s.a.w) amesema โHamtoingia peponi mpaka muamini na hamtaweza kuamini mpaka mpendane. Je, nikufahamisheni jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Jambo hili ni kutoleana salaamu." (Muslim) Ukamilifu wa salaamu ya Kiislamu ni โAssalaamu a'laykumu Warahmatullahi wabarakaatuhu." โAmani ya Allah, Rehema zake na Baraka zake ziwe juu yenu." Anayesalimiwa analazimika kujibu kwa kusema: โWaa'laykumu ssalaamu warahmatullahi wabarakaatuhu." โNanyi pia amani ya Allah, Rehema zake na Baraka zake ziwe juu yenu."
57.Ubora wa kumkumbuka na Kumtukuza Allah wakati wa mapumziko A'bdullaah Ibn Qays (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alimuuliza: "Ee 'Abdullah Ibn Qays, ni kufahamishe hazina miongoni mwa hazina za Peponi? Kisha Mtume (s.a.w) akamwambia sema: โLaa haula walaaquwwata illaabillahi." "Hapana uwezo wala nguvu ila kutoka kwa Allah." (Bukhari na Muslimu)
58.Mtume (s.a.w) amesema, maneno anayopenda Allah kuliko yote ni manne โSub-hanallahi, Wal-hamdulillahi, Walaa ilaaha illallaahu, Wallaahu Akbaru." โUtukufu ni wa Allah, shukurani zote anastahiki Allah, Hapana Mola ila yeye, Allah ni Mkubwa." (Muslimu)
59.Abu Hurayrah (r.a) ameeleza kuwa: Mtume (s.a.w) amesema, "Kuna maneno mawili (2) ambayo ni mepesi katika ulimi na mazito katika mizani na anayopenda Allah, nayo ni: โSub-haanallahi wabihamdihi, wasubuhaana llaahila'dhiim." โUtukufu ni wa Allah na shukrani zote anastahiki yeye. Utukufu ni wa Allah aliye mkuu." (Bukhari na Muslimu)
60.Jabir Ibn Abdullah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Hakika dua kubwa ni kusema: โAl-hamdulillaahi" โShukurani zote anastahiki Allah." Na hakika namna bora ya kumkumbuka Allah (dhikri) ni kusema: โLaailahailla llaaha." โHapana Mola ila Allah." (Ahmad)
Umeionaje Makala hii.. ?
Hii ni historia ya uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina. Yaani wafuasi wa wale wafuasi wa Masahaba
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูู ูู ุงููู ูุคูู ูููููู ุฃูู ูู ุนูุจูุฏู ุงูููููู ุนูุงุฆูุดูุฉู ุฑูุถููู ุงูููููู ุนูููููุงุ ููุงููุชู: ููุงูู: ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู "...
Soma Zaidi...Dua ni moja ya ibada ambazo zinamfanya mja awe karibu na Mweznyezi Mungu. Allah amesisitiza tumuombe dua kwa shida zetu zote, pia akaahidi kuwa atatujibu maombi yetu muda wowote tutakao muomba. Sasa ni zipi nyakati nzuri zaidi kuomb adua?
Soma Zaidi...ุนููู ุนูุจูุฏู ุงูููููู ุจููู ุนูุจููุงุณู ุฑูุถููู ุงูููููู ุนูููููู ูุง ููุงูู: "ููููุช ุฎููููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููููู ูุงุ ููููุงูู: ู...
Soma Zaidi...