Posti hii inakwenda kukufundisha dua za kuomba wakati wa kuwa na maumivu kwenye mwili wako.
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI
Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Hakuna haja ya kumeza dawa za kupunguza maumivu kwa mwenye kumuamini Allah. Ila watu wasielewe vibaya maneno haya, maaana Mtume (s.a.w) amesisitiza watu wajitibu, ila pia ieleweke Allah amejaalia kuwa qurani ni dawa na ni ponyo kwa maradhi na mabo mengine. Leo hapa nimewaandalia dawa ya kuondowa maumivu katika sunnah nayo ni dua ambayo mtume (s.a.w) alikuwa akiwafundisha masahaba waombe pindi wakiwa na maumivu na maradhi.
1.Mtume (s.a.w) alimwambia swahaba kuwa: “weka mkono wako pale unaposikia maumivu katika mwili wako kisha sema “BISMILLAHI” mara tatu kisha useme mara saba (maneno haya): “A’UDHU BILLAHI WAQUDRATIHI MIN-SHARI MAA AJIDU WA-UHAADHIRU”. Hadithi hii ni sahihi na amepokea Muslim, Abu Daud na Ibn Maajah kutokana na masimulizi ya ‘Uthman Ibn Abil-”As.
2.Mtume (s.a.w) alimwambia Mainuna bint Abi Ubay kuwa :”weka mkono wako wa kulia pale panapokupatia maudhi (maumivu) kisha sema “BISMILLAHI ALLAHUMMA DAAWINI BIDAWAAIKA WASHFINII BISHAAIKA WAGHANII BIFADHLIKA ‘AN-MAN SIWAAKA WAHDHUR ‘ANII ADHAAKA” (Amepokea Tabrany)
3.Mume (s.a.w) alimwambia Asmaa bint AbuBakar kuwa: “weka mkono wako (pende maumivu) na useme mara tatu “BISMILLAHI ALLAHUMMA ADH-HAB ‘ANNI SHARRA MAA AJIDU BIDA’AWATIKA NABIYYIKA TWAYYIBIL-MUBAARAKIL-MAKIIN ‘INDAKA. BISMILLAHI “ (Amepokea ibn “Asakir)
4.amesimulia Ibn ‘Abas (r.a) kuwa : “alikuwa Mtume (s.a.w) akitufundisha dua kwa ajili ya maradhi na maumivu yote tunayoyapata kuwa Mtu aseme: ‘BISMILLAHI, A’UDHUBILLAHIL-’ADHIIM MINSHARRI KULLI ‘ARQIN-NA’AARI, WAMINSHARRI HARRIN-NAHAARI” (Amepokea Ahmad, tirmidh na Alhaakim).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ الْحَسَنِ بْنِ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ سِبْطِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم وَرَيْحَانَتِهِ رَضِيَ اللَ...
Soma Zaidi...Hapa nitakuletea baadhi tu ya adhkari ambazo ni muhimu kwa muislamu
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha jinsi ya kumswalia mtume, pamoja na kuzijuwa fadhila unazopata kwa kumswalia Mtume
Soma Zaidi...hii ni orodha ya dua mbalimbali kutoka kwenye quran. Unaweza kuzitumia dua hizi kujipendekeza kwa Allah na kupata msamaha, neema na mengineyo.
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...