NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA.
![]()
![]()
NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA.
Itambulike kuwa dua ambayo imefata vigezo na masharti ya dua itajibiwa tu. Ila pia itambulike kuwa dua hujibiwa katika njia kuu tatu ambazo ni kupewa alichoomba, kufutiwa madhambi au kulipwa siku ya qiama kwa kuingizwa peponi. Hivyo itambuluke kuwa mtu anaweza kuomba dua kisha asijibiwe huenda Allah anataka kumpa kheri zaidi au huenda ameshamjibu kwa kumfutia madhambi yake. Allah ndiye anaejua lile ambalo ni bora kwa wajawake katika wakati wowote ule.
Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema
مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْعُو بِدُعَاءٍ إِلاَّ آتَاهُ اللَّهُ مَا سَأَلَ أَوْ كَفَّ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهُ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ " “
“mtu yeyote anaeomba dua ila atajibiwa ima awahishiwe kujibiwa haphapa duniani, au acheleweshewe (kujibiwa hapa duniani na badala yake ) ajibiwe akhera au asamehewe madhambi yake kwa kiasi kile alichoomba, maadam hajaomba (jambo la) madhambi au kukata udugu aua hajafanya haraka ya kutaka kujibiwa hata akawa anasema ‘nimemuomba Mola wangu na hakunijibu’”. (amepokea tirmidh).
Umeionaje Makala hii.. ?
Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.
Soma Zaidi...Post hii itakueleza ni dua gani unatakiwa uzisome wakati unapokiwa na hasira ama pale unapokasirika.
Soma Zaidi...Download kitabu Hiki Bofya hapa KUINGIA KWA WAGENI Amina na Sadie walimuonea huruma wakamuomba Zubeid amruhusu abakie.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha dua ambazo itazitumia katika swala yako.
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَجُلًا قَالَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه و سلم أَوْصِنِي.
Soma Zaidi...