Dua za kuomba wakati unapokuwa na hasira ama ukiwa umekasirika
Post hii itakueleza ni dua gani unatakiwa uzisome wakati unapokiwa na hasira ama pale unapokasirika.
DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA.
Hashira ni katika matendo ambayo shetani anayapenda sana yatokee kwa mwadadamu. Kwa sababu ya hasira maovu mengine huenda yakatokea kama matusi, kupigana, vifo na mengineyo mengi. Uislamu kama dini iliyokamilika imetowa muongozo mzima juu ya namna ya kukabiliana na hali ya hasira pindi inapotokea. Katika makala hii tunakwenda kuona njia za kukabiliana na hali ya hasira pindi inapotokea.
Njia za kuzuia Hasira
1.Kumlani shetani kwa kusema ‘’a’udhubillahi minashaytwanir- rajiim”: Katika hadithi iliyosimuliwa na Sulayman Ibn Sard amesema: “nilikuwa nimekaa na Mtume (s.a.w), na kulikuwa na watu wawili wanagombana. Mmoja uso umekuwa mwekundu kwa hasira na mishipa ya shingo imemsimama. Mtume (s.a.s) akasema, ‘ninayajuwa maneno ambayo kama atayasema, hasira zote alizo nazo zitaondoka. Kama atasema “a’udhubillahi minash-shaytwaanir- rajiim” hasira zake zote zitaondoka. (amepokea BUkhari)
2.kubakia kimya
Kubakia kimya wakati wa kuwa na hasira ni jambo la busara, kwani ukiendelea kubakia kimya ndio hasira zitatulia. Amesema Mtume (s.a.s) “kama mmoja wenu atapatwa na hasira na abakie kimya (Amepokea Ahmad).
3.Kutokutembea:
Hasira zikitokea kama umesimama usiendelee kwenda au kusimama kwanza kaa chini. Amesema Mtume (s.a.s) “kama mmoja wenu amepatwa na hasira na akiwa amesimama basi na akae chini, hasira zake zitaondoka, na kama hazitaondoka basi na alale” (Amepokea Ahmad).
Kwa ufupi zipo njia nyingi ila hizi tatu ndio nitaishia kwenye makala hii. Tufahamu kuwa kumlani shetani ni njia ya kumkimbiza kwani yeye ndie anayesababisha hasira. Ni vyema ukachukuwa Udhu unapokuwa na hasira na kumlani shetani kwa wingi. Kubakia kimya wakati wa hasira, kukaa kama umesiamama ama kulala ni katika njia za kuondoa hasira
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 web hosting π2 Dua za Mitume na Manabii π3 Bongolite - Game zone - Play free game π4 Kitabu cha Afya π5 Kitau cha Fiqh π6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Dua 10 ambazo ni muhimu kuziomba kwa kila siku.
Posti hii inakwenda kukupa orodha ya dua 10 ambazo unaweza kuziomba kila siku.
Soma Zaidi...Vyanzo vitano vya elimu zote duniani: Chanzo cha Elimu ni Allah (s.w)
Kama tunavyojifunza katika surat βAlaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s.
Soma Zaidi...Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.
Soma Zaidi...Faida za Kusoma Surat Al-Mulk
Surat Al-Mulk (Sura ya 67 katika Qurβan) inajulikana kama sura yenye baraka nyingi na kinga kubwa kwa msomaji wake. Katika makala hii, tunaangazia siri za kiroho, faida za kusoma sura hii kila usiku, na jinsi inavyomkinga Muislamu na adhabu za kaburi. Pamoja na hayo, tutaangazia mafunzo ya kimaadili yanayopatikana ndani ya sura hii yenye aya 30.
Soma Zaidi...