image

Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua, nguzo na sunnah za josho la maiti

1.

Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua, nguzo na sunnah za josho la maiti

Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua

1.Kuoshwa (Kukoshwa).
Mazingatio kabla ya kuosha maiti.
(a)Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake pia.
- Maiti ya mtoto yaweza kuoshwa na yeyote.
- Ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia



(b)Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa ajili ya kumpa msaada inapobidi.


(c)Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti muislamu kama vile;
1. Muoshaji awe muislamu.
2. Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
3. Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
4. Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa ‘gloves’.
5. Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi, pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.



(d)Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:
1. Nia
2. Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi kwa idadi ya witiri.


Namna ya Kuosha Maiti hatua kwa hatua.
i.Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
ii.Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu unaotoka kwa maiti.
- Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye karo liliotengenezwa
kwa kazi hiyo.



iii.Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji wakati wa kuosha.



iv.Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo (ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.



v.Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.



vi.Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama ilivyo mara ya kwanza.



vii.Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi.
- Kama hapaja takata, basi na avae gloves safi na ile chafu aitupe kwenye
ufuo na asafishe tena kama mara ya kwanza mpaka patakate.



viii.Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha akitupe ufuoni.



ix.Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.



x.Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.



xi.Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu za kawaida za kutia udhu (kutawadha).



xii.Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa ameinamishwa mbele kidogo.
- Kama nywele au ndevu ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na
maji mpaka zitakate.
- Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizong’oka
ziambatanishwe na sanda.



xiii.Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni na maji safi mpaka itakate.



xiv.Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyooshwa wa kulia.



xv.Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.



xvi.Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu baada ya kufa.



xvii.Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari kuvalishwa sanda (kukafiniwa).



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1684


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Hadithi Ya 30: Allaah Amefaridhisha Mambo Ya Dini Tusiyapuuze
Soma Zaidi...

HADITHI YA 34 YEYOTE ATAKAYEONA KITENDO KIOVU AKIONDOE KWA MKONO WAKE
Soma Zaidi...

Dua ambazo hutumiwa katika swala
Post hii inakwenda kukugundisha dua ambazo itazitumia katika swala yako. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 29: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote
Soma Zaidi...

Hadithi Ya 42: Ewe Mwana Wa Adam, Utakaponiomba Na Kuweka Matumaini Kwangu Basi Nitakusamehe
Soma Zaidi...

ZIJUWE NAMNA ZA KUZUIA HASIRA, NA MADHARA YA HASIRA
28. Soma Zaidi...

Dua 10 ambazo ni muhimu kuziomba kwa kila siku.
Posti hii inakwenda kukupa orodha ya dua 10 ambazo unaweza kuziomba kila siku. Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Darsa za Dua
Download kitabu hiki na upate kusoma zaidi ya dua 120, pamoja na darsa mbalimbali za dini ya kiislamu. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 37: Allaah Kaviandika Vitendo Vyema Na Vibaya
Soma Zaidi...

DUA 41 - 50
41. Soma Zaidi...

MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...