Kama tunavyojifunza katika surat ‘Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s.
Kama tunavyojifunza katika surat ‘Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s.w). Allah (s.w) huwasiliana na binadamu na kuwaelimisha kwa kutumia mojawapo ya njia zifuatazo zilizoainishwa katika aya ifuatayo:
Na haikuwa kwa mtu kwamba Mwenyezi Mungu anasema naye ila kwa il-hamu (anayetiwa moyoni mwake) au kwa nyuma ya pazia au humtuma mjumbe (Malaika) naye humfunulia kiasi anachotaka kwa idhini yake (Allah), bila shaka yeye ndiye aliye juu mwenye hekima.” (42:51). Aya hii inatufahamisha kuwa binaadamu hupata habari kutoka kwa Allah (s.w) kwa njia tatu zifuatazo:
(a) Il-hamu(Intution).
(b) Nyuma ya pazia.
(c) Kutumwa Malaika na kufikisha ujumbe kama alivyotumwa. Pia katika Qur-an tunafahamishwa njia mbili nyingine anazozitumia Allah (s.w) katika kumfikishia binaadamu ujumbe kutoka kwake:
(d) Ndoto za kweli (ndoto za Mitume).
(e) Maandishi (mbao zilizoandikwa tayari).
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza nafasi ya kufuata suna katika Uislamu
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.
Soma Zaidi...DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu “LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU.
Soma Zaidi...As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, nauliza inajuzu wanawake kuzuru makaburi?
Soma Zaidi...