picha

DUA 113 - 126

DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu “LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU.

DUA 113 - 126


DUA ZA WAKATI WA SHIDA
Dua ya wakati wa taabu
“LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU. LAA ILAAHA ILLA LLAHU RABBULS-SAMAAWATI WARABBUL-ARDHI WARABBUL-’ARSHIL-’KARIIM” (Bukhari)

.Dua pindi uonaposhetani au unapotishwa na shetani
115.Ikitokea Mtu ameona shetani au ametishwa na shetani anatakiwa kuleta isti’adha na asema “A’UDHU BILLAHI MINKA” mara tatu kisha aseme “AL’ANUKA BILA’ANATIL-LLAHI TAAMMAH” mara tatu. Hakika shetani anakimbia ukisema maneno hayo. Hatika mapokezi ukimuona shetani akikutisha au hakukutisha soma adhana hakika shetani hukimbia adhana. Katika hadithi alopokea muslim mtume (s.a.w) amesema “hakika shetani hukimbia pindi adhana ya swala inaposomwa”

pindi muislamu anapokutana na jambo ambalo halitaki. 116.Pindi Muislamu anapoutana na jambo ambalo halitaki au jambo baya litakalomuhuzunisha anatakiwa aseme: “QADDARALLAHU WAMAA SHAA-A FA’ALA” na katu asiseme lau.… Yaani lau nisingelifanya hivi lisingenikuta au mifano kama haya. Kwani kusema hivi hufungua milango ya shetani (Muslim na Nisai)

pindi muislamu anapopatwa na shaka
117.Itakapotokea Mtu anashaka katika nafsi yake juu ya jambo anatakiwa aseme: “HUWAL-AWALU WAL-AKHIRU WADHAHIRU WAL BAATWINU WAHUWA BIKULLI SHAY-IN ‘ALIIM” (Abu Daud amepokea adithi hii na sanadi yake ni sahihi)

Anapopata Muislamu msiba
118.Msiba ni katika mambo yanayohuzunisha moyo. Msiba sio pekeake kifo hata ukipotelewa na kitu pia ni msiba. Hivyo inapotokea hali kama hii ya kuhuzunisha moyo useme:”INNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHIR-RAJI’UUN” Allah amesema kuwa “wape habari njema za furaha wenye subira, ambao wanapopata msiba husema ”INNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHIR-RAJI’UUN”

Dua pindi unapokasirika.
119.Mtume (s.a.w) amekataza sana kuwa na tabia ya kukasirika na ni katika usia alokuwa akiwaba masahaba zake. Pindi mtu anapokasirika Mtume amesema anatakiwa aseme: “A’UDHU BILLAHI MINASH-SHAITWAANIR-RAJIIM” hadithi hii ni sahihi.(Bukhari na Muslim).

Dua unapokutana na adui
120.Pindi unapokutana na adui wako kama kwenye vita ama sehemu nyingine iwe usiku ama mchana unatakiwa useme: “ALLAAHUMMA MUNZILAL-KITAABI WA MUJRISAHAABI WAHAAZIMAL-AHZAABI IHZIMHUM WANSUUNAA ‘ALAYHIM” hii dua aliiomba mtume alipokutana na Maadui zake kwenye vita vya Ahzab (Bukhari na Muslim)

Dua pindi unapohofia kiongozi
121.Ikitokea mtu anajambo na anataka kukutana na kiongozi, au amewekwa chini ya ulinzi na kiongozi jabari, muovu ama kwa namna ingine na akawa anahofu kukabiliana na kiongozi huyo anatakiwa aseme: “LAA ILAAHA ILLAAHUWAL-HALIIMUL-KARIIM,,SUBHAANALLAHI RABBIA-SAMAAWATIS-SAB-’I WARABBIL-’ARSHIL-’ADHIIMI. LAA ILAAHA ILLAA ANTA, ‘AZZA JAARUKA WAJALLA THANAAUKA” amesimulia hadithi hii Ibn “Umar.

DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI
122.Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Hakuna haja ya kumeza dawa za kupunguza maumivu kwa mwenye kumuamini Allah. Ila watu wasielewe vibaya maneno haya, maaana Mtume (s.a.w) amesisitiza watu wajitibu, ila pia ieleweke Allah amejaalia kuwa qurani ni dawa na ni ponyo kwa maradhi na mabo mengine. Leo hapa nimewaandalia dawa ya kuondowa maumivu katika sunnah nayo ni dua ambayo mtume (s.a.w) alikuwa akiwafundisha masahaba waombe pindi wakiwa na maumivu na maradhi.

123.Mtume (s.a.w) alimwambia swahaba kuwa: “weka mkono wako pale unaposikia maumivu katika mwili wako kisha sema “BISMILLAHI” mara tatu kisha useme mara saba (maneno haya): “A’UDHU BILLAHI WAQUDRATIHI MIN-SHARI MAA AJIDU WA-UHAADHIRU”. Hadithi hii ni sahihi na amepokea Muslim, Abu Daud na Ibn Maajah kutokana na masimulizi ya ‘Uthman Ibn Abil-”As.

124.Mtume (s.a.w) alimwambia Mainuna bint Abi Ubay kuwa :”weka mkono wako wa kulia pale panapokupatia maudhi (maumivu) kisha sema “BISMILLAHI ALLAHUMMA DAAWINI BIDAWAAIKA WASHFINII BISHAAIKA WAGHANII BIFADHLIKA ‘AN-MAN SIWAAKA WAHDHUR ‘ANII ADHAAKA” (Amepokea Tabrany)

125.Mume (s.a.w) alimwambia Asmaa bint AbuBakar kuwa: “weka mkono wako (pende maumivu) na useme mara tatu “BISMILLAHI ALLAHUMMA ADH-HAB ‘ANNI SHARRA MAA AJIDU BIDA’AWATIKA NABIYYIKA TWAYYIBIL-MUBAARAKIL-MAKIIN ‘INDAKA. BISMILLAHI “ (Amepokea ibn “Asakir)

126..amesimulia Ibn ‘Abas (r.a) kuwa : “alikuwa Mtume (s.a.w) akitufundisha dua kwa ajili ya maradhi na maumivu yote tunayoyapata kuwa Mtu aseme: ‘BISMILLAHI, A’UDHUBILLAHIL-’ADHIIM MINSHARRI KULLI ‘ARQIN-NA’AARI, WAMINSHARRI HARRIN-NAHAARI” (Amepokea Ahmad, tirmidh na Alhaakim).


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 1501

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Hadithi ya pili: sifa za muumini wa kweli

Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
DUA DHIDI YA WASIWASI, UCHAWI NA MASHETANI

DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 1.

Soma Zaidi...
Dua za wakati wa shida na taabu

Hizi ni Dua ambazo unatakiwa uziombe wakati wa shida na taabu

Soma Zaidi...
Dua za kumuomba Allah wakati wa shida na tabu ama matatizo

Post hii inakwenda kukufundisha dua ambazo ni muhimu kuzisoma wakayi wa shida na taabu.

Soma Zaidi...
TANZU ZA HADITHI

Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihi (b) Hasan/Nzuri.

Soma Zaidi...
SHUGHULI ZA KILA SIKU

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Masharti ya kukubaliwa kwa dua

Post hii itakwenda kukugundisha masharti yanayofungamana na kukubaliwa kwa dua.

Soma Zaidi...
ADHKAR NA DUA

ADHKARI MBALIMBALI NA DUA Hapa tutajifunza dua mbalimbali ambazo ni adhkari.

Soma Zaidi...
DUA ZA WAKATI WA SHIDA

DUA ZA WAKATI WA SHIDA 1.

Soma Zaidi...