Dua ni moja ya ibada ambazo zinamfanya mja awe karibu na Mweznyezi Mungu. Allah amesisitiza tumuombe dua kwa shida zetu zote, pia akaahidi kuwa atatujibu maombi yetu muda wowote tutakao muomba. Sasa ni zipi nyakati nzuri zaidi kuomb adua?
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " يَنْزÙل٠رَبّÙنَا ÙƒÙلَّ لَيْلَة٠إÙÙ„ÙŽÙ‰ السَّمَاء٠الدّÙنْيَا ØÙينَ يَبْقَى Ø«ÙÙ„ÙØ«Ù Ø§Ù„Ù„Ù‘ÙŽÙŠÙ’Ù„Ù Ø§Ù„Ø¢Ø®ÙØ±Ù ÙÙŽÙŠÙŽÙ‚Ùول٠مَنْ يَدْعÙونÙÙŠ ÙَأَسْتَجÙيبَ لَه٠وَمَنْ يَسْأَلÙÙ†ÙÙŠ ÙÙŽØ£ÙØ¹Ù’Ø·Ùيَه٠وَمَنْ يَسْتَغْÙÙØ±ÙÙ†ÙÙŠ ÙَأَغْÙÙØ±ÙŽ Ù„ÙŽÙ‡Ù "
“anashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema ‘nani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsamehe”. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).
2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. عَنْ أَبÙÙŠ Ø£Ùمَامَةَ، قَالَ Ù‚Ùيلَ يَا رَسÙولَ Ø§Ù„Ù„Ù‘ÙŽÙ‡Ù Ø£ÙŽÙ‰Ù‘Ù Ø§Ù„Ø¯Ù‘ÙØ¹ÙŽØ§Ø¡Ù أَسْمَع٠قَالَ " جَوْÙÙ Ø§Ù„Ù„Ù‘ÙŽÙŠÙ’Ù„Ù Ø§Ù„Ø¢Ø®ÙØ±Ù ÙˆÙŽØ¯ÙØ¨Ùرَ الصَّلَوَات٠الْمَكْتÙوبَات٠"
Amesimulia Abuu Umama رضىالله عنه kuwa aliulizwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘dua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema:) usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhi’”. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).
3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqama”. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).
4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).
5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema: “hufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkaba”. (amepokea Tabrany).
6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-’asr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ukaupata.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Hapa nitakuletea baadhi tu ya adhkari ambazo ni muhimu kwa muislamu
Soma Zaidi...Dua ni moja ya Ibada ambazo tunatakiwa kuziganya kila siku. Kuna fadhila nyingi sana za kuomba dua. Post hiibitakwenda kukujuza fadhila za kuomba dua.
Soma Zaidi...Elimu, pamoja na ubora wake, hainufaishi bila ya kutumiwa kwa hekima.
Soma Zaidi...Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini
Soma Zaidi...عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى ?...
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha jinsi ya kumswalia mtume, pamoja na kuzijuwa fadhila unazopata kwa kumswalia Mtume
Soma Zaidi...Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...