Nafasi ya Sunnah (suna) katika Uislamu.


image


Hapa utajifunza nafasi ya kufuata suna katika Uislamu


Nafasi ya Sunnah katika Uislamu
Mtume Muhammad (s.a.w) kama ilivyokuwa kwa Mitume waliomtangulia, alikuwa ni mjumbe wa Allah (s.w) aliyeteuliwa ili aufundishe Uislamu na kuusimamisha katika jamii, yeye mwenyewe akiwa ni kiigizo chema. Hivyo ili watu waweze kuufahamu Uislamu vilivyo na kuweza kuusimamisha katika jamii hawana budi, pamoja na kuisoma Qur-an kwa mazingatio, kumfuata Mtume, kumtii na kumfanya kuwa kiigizo chao kitabia na kimwenendo. Qur-an inasisitiza jambo hili katika aya nyingi na baadhi ya hizo ni hizi zifuatazo:

Amri ya Kumtii Mtume (s.a.w)
Utii kwa Allah (sw) umesisitizwa sambamba na utii kwa Mtume (s.a.w) kama tunavyojfinza katika aya zifuatazo: “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa." (3:132) 

 

“Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu nyenu, walio katika nyie (Waislamu wenzenu). Na kama mkikhitalifiana juu ya jambo lo lote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hiyo ndiyo kheri, nayo ina matokeo bora kabisa." (4:59) Na mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na tahadharini (na kukhalifu amri zao). Na mkikengeuka basi jueni ya kwamba juu ya Mtume wetu ni kufikisha tu (ujumbe) waziwazi. (Na akishafikisha hana lawama; lawama juu yenu). (5:92) ................Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni katika wanaoamini (kweli). (8:1)

“Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msijiepushe naye na hali mnasikia." (8:20)

 

Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume, na kama mkikengeuka, basi ni juu yake huo (mzigo) aliotwika; (kazi aliyopewa kufikisha ujumbe). Na juu yenu (huo mzigo) mliotwikwa (kutii). Na mkimtii mtaongoka; hapana juu ya Mtume ila kufikisha (ujumbe wake) wazi wazi. (24:54)

 

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu. ( 47:33)

 

Na mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume. Mkipuuza (hapana lawama juu yake). Juu ya Mtume wetu ni kufikisha tu kuliko wazi wazi. (Naye amekwisha kukufikishieni). (64:12)

Amri ya Kumfuata Mtume (s.a.w)
Sema, "Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni, (hapo) Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye maghufira (na) mwenye rehema." (3:31)

 

"Na anachokupeni Mtume basi pokeeni na anachokukatazeni jiepusheni nacho". (57:7)

 

Amri ya Kumfanya Mtume (s.a.w) Kiigizo "Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana." (33:21)

 

Kutomfuata Mtume (s.a.w) ni Uasi Na anayemwasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuiruka mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamwingiza Motoni, humo atakaa milele, na atapata adhabu zifedheheshazo. (4:14)

Siku hiyo wale waliokufuru na kumwasi Mtume watatamani ardhi isawazishwe juu yao (yaani lau kuwa wamefukiwa tu kaburini bila ya kufufuliwa). Wala hawataweza kumficha Allah Hadith yo yote (katika ammbo waliyoyafanya). (4:42)

 

“Je, hawajui ya kwamba anayeshindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa yeye atapata moto wa Jahannam kukaa humo daima? Hiyo ndiyo hizaya kubwa." (9:63)  “…

 

Na watakao muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi bila shaka watapata moto wa Jahanam, wakae humo milele." (72:23)



Aya hizi zote kwa ujumla zinatuonyesha wazi kuwa kufuata sunnah, ya Mtume (s.w) si jambo la hiari kwa Muislamu. Hivyo ule uoni walionao baadhi ya Waislamu kuwa sunnah ni jambo la hiari, ukilifanya unapata thawabu na ukiliacha hupati dhambi ni uoni potofu kama tutaizingatia pia aya ifuatayo: "Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika wamepotea upotofu ulio wazi (kabisa). (33:36)

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    2 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    3 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Uandishi wa Hadithi wakati wa Matabiina
Historia ya uandishi wa hadithibwakati wa Matabiina, yaani wafuasi wa maswahaba Soma Zaidi...

image Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe
Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio. Soma Zaidi...

image Je waislamu walishindwa vita vya Uhudi?
Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri? Soma Zaidi...

image Fadhila za kujenga msikiti
Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah. Soma Zaidi...

image Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba
Nini kilichangia ongezeko la uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba. Soma Zaidi...

image Mda wa mwisho wa kula daku mwezi wa ramadhani
Post hii fupi itakwenda kukujulisha utaratibu wa kula daku. Soma Zaidi...

image Mzazi na msafiri na mwenye kudhulumiwa dua zao hujibiwa kwa haraka
Wapo watu kadhaa ambao waliomba dua hazirudi. Hapa nitakueleza wawili ambao ni mzazi na msafiri. Soma Zaidi...

image Usitamani kifo hata ukiwa mchamungu mno ama muovu mno
Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana. Soma Zaidi...

image Uandishi wa hadithi wakati wa Matabii tabiina (tabiitabiina)
Hii ni historia ya uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina. Yaani wafuasi wa wale wafuasi wa Masahaba Soma Zaidi...

image Nafasi ya Sunnah (suna) katika Uislamu.
Hapa utajifunza nafasi ya kufuata suna katika Uislamu Soma Zaidi...