DUA ZA WAKATI WA SHIDA 1.
DUA ZA WAKATI WA SHIDA
1.Dua ya wakati wa taabu
âLAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-âADHIMUL-HALIIMU. LAA ILAAHA ILLA LLAHU RABBULS-SAMAAWATI WARABBUL-ARDHI WARABBUL-âARSHIL-âKARIIMâ (Bukhari)
2.Dua pindi uonaposhetani au unapotishwa na shetani
Ikitokea Mtu ameona shetani au ametishwa na shetani anatakiwa kuleta istiâadha na asema âAâUDHU BILLAHI MINKAâ mara tatu kisha aseme âALâANUKA BILAâANATIL-LLAHI TAAMMAHâ mara tatu. Hakika shetani anakimbia ukisema maneno hayo. Hatika mapokezi ukimuona shetani akikutisha au hakukutisha soma adhana hakika shetani hukimbia adhana. Katika hadithi alopokea muslim mtume (s.a.w) amesema âhakika shetani hukimbia pindi adhana ya swala inaposomwaâ
3.pindi muislamu anapokutana na jambo ambalo halitaki.
Pindi Muislamu anapoutana na jambo ambalo halitaki au jambo baya litakalomuhuzunisha anatakiwa aseme: âQADDARALLAHU WAMAA SHAA-A FAâALAâ na katu asiseme lau.⌠Yaani lau nisingelifanya hivi lisingenikuta au mifano kama haya. Kwani kusema hivi hufungua milango ya shetani (Muslim na Nisai)
4.pindi muislamu anapopatwa na shaka
Itakapotokea Mtu anashaka katika nafsi yake juu ya jambo anatakiwa aseme: âHUWAL-AWALU WAL-AKHIRU WADHAHIRU WAL BAATWINU WAHUWA BIKULLI SHAY-IN âALIIMâ (Abu Daud amepokea adithi hii na sanadi yake ni sahihi)
5.anapopata Muislamu msiba
Msiba ni katika mambo yanayohuzunisha moyo. Msiba sio pekeake kifo hata ukipotelewa na kitu pia ni msiba. Hivyo inapotokea hali kama hii ya kuhuzunisha moyo useme:âINNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHIR-RAJIâUUNâ Allah amesema kuwa âwape habari njema za furaha wenye subira, ambao wanapopata msiba husema âINNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHIR-RAJIâUUNâ
6.Dua pindi unapokasirika.
Mtume (s.a.w) amekataza sana kuwa na tabia ya kukasirika na ni katika usia alokuwa akiwaba masahaba zake. Pindi mtu anapokasirika Mtume amesema anatakiwa aseme: âAâUDHU BILLAHI MINASH-SHAITWAANIR-RAJIIMâ hadithi hii ni sahihi.(Bukhari na Muslim).
7.Dua unapokutana na adui
Pindi unapokutana na adui wako kama kwenye vita ama sehemu nyingine iwe usiku ama mchana unatakiwa useme: âALLAAHUMMA MUNZILAL-KITAABI WA MUJRISAHAABI WAHAAZIMAL-AHZAABI IHZIMHUM WANSUUNAA âALAYHIMâ hii dua aliiomba mtume alipokutana na Maadui zake kwenye vita vya Ahzab (Bukhari na Muslim)
8.Dua pindi unapohofia kiongozi
Ikitokea mtu anajambo na anataka kukutana na kiongozi, au amewekwa chini ya ulinzi na kiongozi jabari, muovu ama kwa namna ingine na akawa anahofu kukabiliana na kiongozi huyo anatakiwa aseme: âLAA ILAAHA ILLAAHUWAL-HALIIMUL-KARIIM,,SUBHAANALLAHI RABBIA-SAMAAWATIS-SAB-âI WARABBIL-âARSHIL-âADHIIMI. LAA ILAAHA ILLAA ANTA, âAZZA JAARUKA WAJALLA THANAAUKAâ amesimulia hadithi hii Ibn âUmar.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya hadithi al Quds na Hadith an-Nabawiy
Soma Zaidi...