Post hii itakufundisha maana ya neno sunnah katika Uislamu. Pia utajifunza maana ya neno hadithi katika uislamu
Maana ya Sunnah:
Kilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Hivyo ukisema "Sunnat Muhammad (s.a.w)" ina maana ya mwenendo au tabia au mila aliyokuwa akiifuata Mtume Muhammad (s.a.w) katika maisha yake ya kila siku. Na ikisemwa, "Sunnatullah" kama ilivyotumika katika Quran, ina maana ya desturi au kawaida au mila ya Allah (s.w) katika kufanya mambo ya Uungu wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: “Hii ni kawaida (sunnah) ya Allah (ya kuwaadhibu wakorofi) iliyokuwa kwa waliopita zamani, hutapata mabadiliko katika kawaida (sunnah) ya Allah." (33:62).
Kisheria, sunnah ni mwenendo au matendo ya Mtume (s.a.w) ambayo ni sehemu ya Utume wake. Waislamu wanalazimika kuyaiga na kuyafuata katika uendeshaji wa maisha yao ya kila siku ili kupata radhi za Allah (s.w). Mwenendo wa Mtume (s.a.w) haukutokana na matashi yake bali ulikuwa ni wahyi kutoka kwa Allah (s.w) kama inavyothibitika katika Qur-an: “Na hazungumzi (Muhammad) kwa matamanio ya nafsi yake.Isipokuwa (anayozungumza ni) wahyi uliofunuliwa kwake." (53:3-4)
Kiutendaji, sunnah ya Mtume (s.a.w) ni yale matendo ya msingi aliyoyafanya, aliyoyaagiza na yaliyofanywa mbele yake asiyakemee au kuyakataza.
Maana ya Hadith:
Kilugha: maana ya Hadith katika lugha ya Kiarabu ni jambo jipya au kitu kipya", hutuba, taarifa, maelezo au mapokezi. Katika Qur-an neno "Hadith" limetumiwa kwa maana hizi kama ilivyo katika aya ifuatayo: Basi simulizi gani baada ya hizi (simulizi za Qur-an) wataziamini?" (77:50) Kisheria, Hadith za Mtume (s.a.w) ni simulizi (mapokeo) au taarifa juu ya yale yote aliyoyafanya Mtume (s.a.w) katika kuufundisha Uislamu kinadharia na kimatendo au juu ya yale yaliyotendwa mbele yake akayakataza au akayaridhia au maelezo juu ya mwenendo na tabia ya Mtume (s.a.w). Ifuatayo ni mifano ya Hadith za Mtume (s.a.w):
(i)Maelezo au maelekezo ya Mtume (s.a.w)
Amesema Mtume (s.a.w) "Mwenye kumueleza mwenzake jambo la kheri anapata malipo sawa na mtendaji wa kheri hiyo."
(ii)Vitendo vya Mtume (s.a.w).
Amesema Bibi Aysha (r.a): "Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali swala ya Dhuha rakaa nne na mara nyingine huzidisha atakazo."
(iii) Kukubali (kuridhia)
Amesema Bibi Aysha (r.a): "Mtume (s.a.w) aliwapeleka askari kwenye vita, kiongozi wao alikuwa akipendelea sana kusoma suratul- Ikhlasi katika swala. Waliporejea waliripoti kwa Mtume (s.a.w) jinsi Imamu wao alivyokuwa anafanya, Mtume (s.a.w) akasema: "Muulizeni kwanini alifanya hivyo." Wakamuuliza naye akajibu kwamba suratul- Ikhlas ni sifa za Mwenyezi Mungu na yeye anapenda kuzisema. Mtume (s.a.w) akasema: "Mwambieni kwamba na yeye Mwenyezi Mungu anampenda."
(iv) Sifa au Mwenendo wa Mtume (s.a.w)
"Amesema Sayidna Ali (r.a), Mtume (s.a.w) alikuwa mwenye elimu, mpole na mkarimu. Mwenye kumuona Mtume (s.a.w) huvutiwa naye na kumfuata."
Umeionaje Makala hii.. ?
Dua ni moja ya ibada ambazo zinamfanya mja awe karibu na Mweznyezi Mungu. Allah amesisitiza tumuombe dua kwa shida zetu zote, pia akaahidi kuwa atatujibu maombi yetu muda wowote tutakao muomba. Sasa ni zipi nyakati nzuri zaidi kuomb adua?
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha umuhimu wa nasaha katika dini
Soma Zaidi...Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihi (b) Hasan/Nzuri.
Soma Zaidi...Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.
Soma Zaidi...