DUA 61 - 84

DUA 61 - 84

61.

Download Post hii hapa

DUA 61 - 84


61.Mtume (s.a.w) amesema, amali njema ya kudumu ni kusema: “Sub-haanallahi, wal-hamdulillaahi, walaailaha illallaahu walaahu akbaru walaahawla walaaquwwata illaabillaahi." Utukufu ni wa Allah na shukurani zote anastahiki Allah, na Hapana Mola ila Allah na Allah ni mkubwa. Hapana uwezo wala nguvu ila kutoka kwa Allah."

62.Dhikri ya kuleta wakati wa kulala Alikuwa Mtume (s.a.w) akienda kulala usiku, akiweka pamoja viganja vyake kisha akivipulizia na akivisomea suratul-Ikhlas, suratul Falaq na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani, usoni na mbele (akifanya hivyo mara tatu.) (Bukhari na Muslimu)

63.Mtume (s.a.w) amesema: "Ukienda kulala soma Ayatulkursiyyu kwani Allah ataendelea kukuhifadhi, wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi." (Al-Bukhari)

64.Mwenyezi Mungu, hakuna Mola ila yeye, ndiye mwenye uhai wa milele, msimamia kila jambo. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni vyake (peke yake vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na (yaliyo) nyuma yao; wala (hao viumbe) hawalijui lolote katika ilimu yake ila kwa alipendalo. Enzi yake imeenea mbinguni na ardhini, wala kuvilinda hivyo hakumshindi; Na yeye (pekee) ndiye aliye juu na ndiye aliye mkuu." (2:255)

65.Alikuwa Mtume (s.a.w) akitaka kulala, anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake, kisha anasema: "Allahumma qiniy a'dhaabaka yaumatab-a'thu i'baadaka." "Ee! Allah nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakapowafufua waja wako."

66.Pia Mtume (s.a.w) wakati wa kulala alikuwa akisema: “Allahumma Bismika amuutu wa-ahyaa. “Kwa jina lako, Ee Allah ninakufa na nina kuwa hai." uzi na ndiye Mwenye hikima (2:32)

Dua ya kufungulia swala (Duau al-iftitah)
67.Kusoma dua ya kufungulia swala ni sunnah. Katika Hadithi ya Bukhari na Muslim iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), baada ya kuhirimia swala Mtume (s.a.w) alikuwa akileta dua ifuatayo:

68.“wajahtu wajhi lilladhi fatwaras-samaawat wal-ardha hanifam-muslima wamaa kaana minal-mushrikina. Inna swalatiy wanusukii, wamah-haya, wamaamatiy, lillahi rabil-alamiina laa sharikalahu wabidhalika umirtu wa-ana minal-mushrikiina.”

Tafsiri:
“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Nimeacha dini za upotovu. Mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika swala yangu (na ibada zangu zote) na uzima wangu na kufa kwangu (yote) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bwana (Rabbi) wa walimwengu wote. Hana mshirika wake. Na haya ndio niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza walio jisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu. (6:79, 162-163)

Kusoma al-hamdu (surat al-fatiha) 69.Baada ya kusoma dua ya kufungulia swala mtu atasoma alhamdu. Na kusoma al-hamdu ni nguzo ya swala.Tunasoma suratul-Fatiha kama ifuatavyo:-

70.Bismillahir Rahmaanir Rahiim (1) Alhamdu liLLahi rabbil-’Aalamiin (2). Rrahmaanir Rahiim (3) Maaliki yaumiddiin (4) Iyyaakana‘abudu waiyyaaka nasta‘iin (5) Ih dinasw-swiraatwal mustaqiim (6) Swiraatwa lladhiina an ‘amta ‘alaihim; ghairil maghdhuubi ‘alaihim wala dhw-dhwaaliin (7)

Tafsri:
71.(1) Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu: (2) Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu wote: (3) Mwingi wa Rehema mwenye kurehemu (4) Mwenye kumiliki siku ya malipo: (5) Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunaye kuomba msaada: (6) Tuongoze njia iliyonyooka: (7) Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale ) waliokasirikiwa, wala ya wale waliopotea.

Kurukuu.
72.Katika rukuu ni sunnah kusoma dua hii Katika rukuu ni sunnah kumsabihi Allah (s.w) kwa kusema kimya kimya mara tatu au zaidi

73.“Subhana Rabbiyal’Adhiim”
Tafsiri:
74.“Utukufu ni wako Ee Bwana (Mlezi) wangu Uliye mkuu”

Kuitidali (kusimama wima kutoka kwenye rukuu) 75.wakati wa kunyanyuka maneno haya:“sami’a llahu liman hamidahu” Mwenyezi Mungu anamsikia kila mwenye kumhimidi. Na baada ya kusimama sawa ni sunnah kusema “rabbanaa walakal-hamdu”ewe mola wetu sifa zote za ukamilifu ni zako. Pia ni sunnah kusema maneno haya

76.“rabbanaa walakal-hamdu mil-as-samaawati wamil-al-ardhi wamil-amashi-ita minshai-in ba’adah”
Tafsiri:
77.Ewe Mola wetu sifa zote za ukamilifu ni za kwako, kutoka mbinguni, kutoka ardhini na katika vitu vyote vilivyo baina yao (mbingu na ardhi) na kutoka katika vinginevyo unavyo viridhia

Kusujudi
78.utasema kwenye sijda:-

79.“subhaana rabbiyal-a’alaa” Tafsiri:
80.utukufu ni wa kwako Mola uliye tukuka. (mara tatu au zaidi)

Kukaa kati ya sijida mbili.
Katika kikao hiki utasema:-
81.“rabbigh-firliy warhamnii wa’afinii warzuqniy”
Tafsiri: Ewe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya na uniruzuku

Tahiyyatu (maamkizi)
Haya ni maneno yanayosemwa katika kikao cha tahiyatu. Maneno haya ni:-

82.“Attahiyyaatu lillaah, wasw-swalawaatu, watwa-yyibaatu, assalaamu ‘alaika ayyuhannabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuhu, assalaamu ‘alay-naa wa-’alaa ‘ibaadillaahi swswaalihiina. Ash-hadu an-llaailaaha illallaahu wa-ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhuu warasuuluhu”.

Tafsiri:
83.“Maamkizi yote ni ya Allah, na swala zote na yote mazuri, Amani iwe juu yako, ewe Mtume na Rehma na Baraka za Allah. Na amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah. Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mja na, ni Mtume wake”. (Muslim).

Kumswalia Mtume (s.a.w) kwenye tahiyyatu ya mwisho. Zipo aina nyingi za kumswalia Mtume (s.a.w). Hapa utasema maneno yafuatayo:-

84.“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka hamiidum-majid”

Tafsiri: Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.


                   

Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 758

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Muangalie aliye chini yako na usimuangalie aliye juu
Muangalie aliye chini yako na usimuangalie aliye juu

Katika hadithi hii utakwenda kujifunza hekma ya kuangalia watu walio chini yako na sio walio juu yako

Soma Zaidi...
UHAKIKI WA HADITHI
UHAKIKI WA HADITHI

Uhakiki wa Hadith za Mtume (s.

Soma Zaidi...
DUA ZA WAKATI WA HASIRA
DUA ZA WAKATI WA HASIRA

DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA.

Soma Zaidi...
Ni  zipi hadithi sahihi na hadithi Quds
Ni zipi hadithi sahihi na hadithi Quds

Hapa tutajifunza maana ya hadithi sahihi na hadithi Quds na tofaiti zao.

Soma Zaidi...
Dua za kuwaombea wazazi
Dua za kuwaombea wazazi

Kwenye Quran kuna duaambazo Allah ametufundisha tuziombe kwa ajili ya wazazi, familia na kwa ajili yetu wenyewe.

Soma Zaidi...
kuwa muaminifu na kuchunga Amana
kuwa muaminifu na kuchunga Amana

Uaminifu ni uchungaji wa amana.

Soma Zaidi...
BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU
BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU

BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU.

Soma Zaidi...
Dua za kuondoa wasiwasi,  woga na kujikinga na uchawi, na mashetani
Dua za kuondoa wasiwasi, woga na kujikinga na uchawi, na mashetani

Post hii itakufundisha dua za kuomba wakati wa woga, wasiwasi na kujikinga na wachawi na mashetani

Soma Zaidi...