Dhamana ya Kuchunga Ahadi Katika Uislamu

Kuchunga'au kutekeleza'ahadi'ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli.

Dhamana ya Kuchunga Ahadi Katika Uislamu

  1. Kuchunga Ahadi

Kuchunga au kutekeleza ahadi ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli. Utekelezaji wa ahadi pia ni matunda ya ukweli na uaminifu. Mtu mkweli na mwaminifu ni lazima awe ni mwenye kutekeleza ahadi. Tumeona katika hadith kuwa ukosefu wa uaminifu, uwongo na uvunjaji wa ahadi ni alama kuu tatu za unafiki.

Muislam hana budi kujizatiti katika kutekeleza ahadi zote alizozitoa katika kutekeleza mambo mema. Muislamu akiahidi kutekeleza jambo jema au akiapa kufanya jambo fulani jema analazimika kutekeleza ahadi hiyo au kiapo hicho. Ama kiapo au ahadi ya kufanya mambo maovu si jambo lililosahihi mbele ya Allah(sw). Kwa hiyo ahadi au kiapo cha kufanya mambo yaliyokinyume na sharia ya Allah (sw) si ahadi au kiapo kinacho tambulika mbele ya Allah na atakapodhihirika kuwa ahadi yake au kiapo chake kilikuwa nicha kutenda maovu akivunjemara moja. Vinginevyo kila ahadi njema ni lazima itekelezwe na kuna adhabu kali mbele ya Allah kwa wavunjao ahadi. Hebu tuone msisitizo wa Allah (s.w) juu ya utekelezaji wa ahadi:“...Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa (siku ya Kiyama). (1 7:34)“Na tim izeni ahadi m nazozitoa kw a jina la Mw enyezi Mungu m napoahidi, wala msivunje hizo ahadi baada ya kuzithubutisha , hali mume kweisha mfanya Mw enyezi Mungu kuw a shahidi kw enu. Hakika Mw enyezi Mungu anayajua yote mnayoyafanya. (16:91)“Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi yao, tuliwalaani na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. (5:13)

Aya hizi zinatosha kutuonesha umuhimu wa kuchunga ahadi katika Uislamu. Aya zinabainisha kuwa utekelezaji wa ahadi ni amri kama amri nyingine za Allah (sw) ambazo mja akizitekeleza hupata mafanikio mema hapa duniani na malipo makubwa humngojea huko akhera na akizivunja huhasirika katika maisha yake hapa duniani na huko akhera. Tunafahamishwa pia katika Qur’an kuwa miongoni mwa watu wema watakaofuzu mbele ya Allah ni wale watekelezao ahadi zao

kama tunavyohamiswa katika aya zifuatazo:

“Hakika wamefuzu Waislamu…ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia (wanazitekeleza). (23:1,8)Wema ni (wale)… watekelezao ahadi zao wanapo ahidi. (2:1 77)

Pia Uislamu unaitazama ahadi kwa upeo mpana zaidi kuliko ahadi za kawaida tunazotoa kwa wanaadamu wenzetu.

Ahadi kuu tunayoitoa mbele ya Allah (s.w) ni kuwa tutamuabudu na kumtegemea yeye pekee. Ahadi hii ameitoa kila mtu hata kabla ya kuja hapa duniani kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Na kumbuka Mola wako alipowaleta katika wanaadamu miongoni mwao kizazi chao na kuw ashuhudisha juu ya nafsi zao (akawaambia): Je, mimi siye Mola wenu? Wakasema: Ndiye, tunashuhudia.(Akawaambia) “Msije mkasema siku ya Kiyama kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo. (7:1 72).

Aya hii inatupa mwanga kuwa kumuamini Allah (sw) na kumuabubu inavyostahiki katika maisha ya kila siku ni ahadi ya asili iliyofungamana na umbile la binaadamu. Hivyo ni wazi kuwa kumuamini Allah (sw) na kumuabudu inavyostahiki ni jambo jepesi linalolandana na asili ya umbile la mwanadamu mwenyewe. Hata hivyo kwa kuwa binaadamu ameumbwa na udhaifu mwingi; Allah (sw) hakumuacha binadamu hivyo hivyo na ahadi yake ya asili, bali ameweka utaratibu madhubuti wa kumkumbusha binaadamu ahadi yake hii mara kwa mara katika maisha yake yote. Allah (sw) ameleta mitume pamoja na vitabu ili kuwakumbusha wanaadamu wa kila ummah na kila zama juu ya ahadi hii kuu. Waislamu wanajikumbusha mara kwa mara juu ya ahadi hii katika swala kila wanaposoma Suratul-Fatiha.

 “Ni Wewe tu tunayekuabudu na ni wewe tu tunayekuomba msaada”. (1:5).Pia tunapotoa shahada:

“Nashuhudia kuwa hapana mola ila Allah na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah”.

Katika shahada tunatoa ahadi kuwa katika kuendesha maisha yetu ya kila siku tutamtii na kumnyenyekea Allah (s.w). Pekee na tutafuata mwenendo wa Mtume wake. Hivyo, yule mwenye kumuasi Allah (s.w) na Mtume wake ni mwenye kuvunja ahadi.

Aidha, katika Qur-an tunaamrishwa kuchunga ahadi yoyote ya halali tuliyoitoa kwa mtu au kwa jamii:

“Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa ”. (17:34).

Kuvunja ahadi ya halali pasina dharura ni tabia ya unafiki.Katika mchakato wa maisha ya kila siku tuna weka ahadi za aina nyingi na hapa tutarejea baadhi ya aya za kuomba ahadi hizo:Deni ni Ahadi

Ahadi nyingine inayochukua nafasi ya juu ni ahadi ya kulipa deni. Kukopa katika Uislam pasina riba ni jambo la halali kwa mtu aliyetingwa na shida ya msingi. Kukopa kwa ajili tu ya kujistarehesha au kufanya mambo ambayo si ya lazima wakati huo ni jambo lisilopendelewa na Uislamu kwani kushindwa kulipa deni hilo itakuwa ni miongoni mwa mambo yatakayomhasirisha mja mbele ya Allah (sw) katika siku ya Hukumu. Mtume (saw) amesema:

Mkopaji akifa (na deni) atalazimishwa kulipa deni hilo siku ya Kiyama. Bali deni linaruhusiwa katika hali tatu;kwanza, wakati mja atakapo kuwa hana cha kumuwezesha kupigania katika njia ya Allah na akakopa ili ajitayarishe kupigana na adui yake na adui wa Allah(sw); Pili, wakati mtu atakapofiwa na Muislamu wa karibu yake na akakopa ili agharimie mazishi, na tatu, kwa manamume ambaye kwa kuhofia hatari za kuendelea kukaa bila kuoa kwa kusindwa kuchunga mipaka ya Dini, akakopa ili kugharimikia ndoa, Allah (sw) atawasamehe katika siku ya Hukumu(iwapo watakufa na madeni). (Ibn Majah).

Katika hadith nyingine tunafahamishwa kuwa Mtume wa Allah am e s em aSiku ya Kiyama Allah (sw) atamwita mkopaji na kumsimamisha mbele yake. Kisha ataulizwa; Ee mwana wa Adamu! Ni kwa shida gani ulijiingiza katika deni hili? Na kwa nini umechukua (umeharibu) haki za wengine? Atajibu: “Ee Bwana wetu! Yu w afahamu vema kile nilichokopa, siku (kila w ala kukinyw a w ala kukifuja, lakini w akati fulani ajali ya moto ilitokea, wakati mwingine palitokea wizi (mali hiyo) ilipotea au hasara ilitokea (juu yake). Allah (s.w.) atasema:”Ee mja wangu! Umesema kweli. Nina haki zaidi kulipa deni hili. Allah ataamuru ichukuliwe amali njema na ataipima katika mizani, na amali yake njema itakuwa nzito kuliko amali mbovu, ataingia peponi kw a Rehema ya Bw ana wake ”. (Ahmad).Hadith zinatufahamisha kuwa Allah (sw) atawalipia madeni wale tu ambao walilazimishwa na hali ikabidi wakope na kwa bahati mbaya wakakosa cha kulipa mpaka wakafa na madeni. Katika hali hii Allah (sw) atawalipia madeni hayo siku ya kiyama kwani ni lazima kila mwenye haki alipwe haki yake siku hiyo ya Kiyama kwani ni lazima kila mwenye haki alipwe haki yake siku hiyo. Lakini atakayekopa bila ya sababu ya msingi, halafu itokee asilipe deni lake mpaka akafa, ni lazima atalilipa mwenyewe deni hilo mbele ya Allah (sw). Pia Mtume (saw) amesema:

Mali ya wengine (kama mkopo) kwa nia ya kulipa (kisha asiweze kulipa) Allah (sw) atamlipia deni lake. Na mwenye kuchukua mkopo kwa nia ya kutolipa, basi Allah atamuangamiza na kumhilikisha. (Bukhari)Katika Hadith nyingine tunafahamishwa kuwa:

Abu Qatawa ameeleza kuwa mtu mmoja aliuliza: Ee Mtume wa Allah kama nitauaw a katika njia ya Allah, dhambi zangu zote zitasamehew a? Alijibu (Mtume): “Ndio, kama utaumwa, na kama ni mwenye subira na shukurani na mwenye kutafuta Radhi za Allah, kama umebakia katika mstari wa mbele na kuwashambulia maadui bila ya kurejea nyuma. “Kisha Mtume akamuuliza kuwa amesemaje. Muulizaji alirudia tena swali lake na kisha Mtume (saw) akasema: Dhambi zako zitasamehewa lakini deni lako halitasamehew a. Sasa hivi Jibril amenifahamis ha juu ya hili. (Muslim).

Huu ndio uzito wa deni na Muislam wa kweli atajitahidi kujiepu sha na madeni na ikibidi akope ajitahidi kulilipa katika muda aliouahidi au mapema zaidi pale atakapopata uwezo. Utashangaa leo hii waislamu wamefanya kukopa ndio mtindo wa maisha!Nadhiri ni ahadi

Mara nyingi mwanaadam anapokuwa na hali ngumu , humwomba Mola wake kuwa akimuondoa kwenye hali ile ya shida atamuabudu inavyostahiki na atatenda wema kwa waja wake. Lakini wanafiki huvunja ahadi hiyo na kusahau kabisa yale aliyoahidi baada ya kupata hali nzuri aliyoitamani. Katika historia tunafahamishwa mfano wa watu wa namna hii. Mtume (saw) alipokuwa Madina, mtu mmoja jina lake Sa’laba alihudhuria mkutano wa Ansar na mbele ya mkutano aliahidi kuwa kama Allah (sw) atamtajirisha, atatoa sadaqa na atawafanyia wema jamaa zake. Punde alitajirika kwa mali ya urithi. Lakini, kwa bahati mbaya hakutekeleza ahadi yake wala hakukumbuka yale aliyoyatamka mbele ya Allah (sw). kutokana na kisa hiki Allah anatukumbusha katika aya zifuatazo:“Na m iongoni mw ao w ako w aliom uahidi Mw enyezi Mungu kuw a :”akitupa katika fadhila zake tutatoa sadaqa na tutakuwa miongoni mwa watendao mema. Lakini alipowapa hizo fadhila zake walizifanyia ubakhili na wakakengeuka, nao (mpaka hivi sasa) wanakengeuka. Kwa hiyo atawalipa unafiki nyoyoni mwao mpaka siku ya kukutana Naye, kwa sababu ya kukhalifu kwao waliyomuahidi Mwenyezi Mungu na kwa sababu ya kusema kwao uwongo”. Je hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong’ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye mambo ya ghaibu ” (9:75-78).

Muislamu wa kweli anatakiwa kila mara akumbuke hali yake duni aliyonayo hapo awali kutokana na uchanga wake , ugonjwa, uhaba wa mali au kutokana na mazingira fulani ya dhiki na alinganishe hali nzuri na wasaa alionao hivi sasa kisha amshukuru Allah (sw) kwa kuzidishaunyenyekevu kwake na kutenda mema.Mikataba ni Ahadi

Waislamu wa kweli hawana budi kufuata masharti ya mikataba waliofunga na wengine kipindi ambapo haiendi kinyume na sharia ya Allah (sw). Katika historia tunaona jinsi Mtume (saw) alivyofuata masharti ya mikataba ya amani waliyowekeana na makabila au mataifa ya makafikiri. Kwa mfano, kutokana na mkataba wa amani wa Hudaybiyya, Mtume (saw) alimkatalia Muislamu kutoka mikononi mwa Makurayshi kujiunga na kundi la waislamu wenzake kwa vile ingalikuwa ni kinyume na makubaliano ya mkataba pamoja na kwamba mkataba kulikuwa haujawekwa sahihi. Uislam unatutaka tuwe wakweli katika mikataba yetu hata kama tumefunga mikataba hiyo na maadui zetu na maadui wa Mwenyezi Mungu. Tunatanabahishwa katika Qur’an:“…wala kule kuwachukia watu kwa kuwa walikuzuilieni kufika katika ms ikiti uliotukuzw a (Makka) kus ikuopelekeeni kutow afanyia uadilifu, Na saidianeni katika wema na ucha-Mungu, wala msisaidiane katika m aovu na uadui. Na Mcheni Mw enyezi Mungu ; hakika Mw enyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu”. (5:2)

Maelezo haya yanatosha kutupa mwanga wa uzito wa ahadi mbele ya Allah(sw). Muislamu wa kweli hana budi kujizatiti kuwa mkweli katika ahadi zake zote alizozitoa kwa Allah (s.w) na kwa wanaadaml wenziwe. Zote hizi zitakuwa ni zenye kuulizwa mbele ya Allah (sw) katika siku ya Hukumu.                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 295


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

UGONJWA WA MALARIA NA TAKWIMU ZA ATHARI YAKE KIDUNIA
Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles. Soma Zaidi...

Simu au Kompyuta inastak? (inasumbua)
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

dharura
14. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah
Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Soma Zaidi...

Matendo ('amal) hulipwa kutokana na nia (makusudio)
Soma Zaidi...

HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA HUJIBIWA
HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA. Soma Zaidi...

Taqwa (Hofu ya kumuogopa Allah) ni popote ulipo
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '... Soma Zaidi...

Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya 'Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki katika quran
Soma Zaidi...

Maana ya swala
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno 'Swalaat' lina maana ya 'ombi au 'dua. Soma Zaidi...

Husaidia wenye matatizo katika jam ii
Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada. Soma Zaidi...

Khalifa 'Umar bin Abdul Aziz
Soma Zaidi...