image

Utaratibu wa kutekeleza hija, matendo hatua kwa hatua, pamoja na kusherehekea sikuku baada ya hija

4.

Utaratibu wa kutekeleza hija, matendo hatua kwa hatua, pamoja na kusherehekea sikuku baada ya hija

Utaratibu wa kutekeleza hija, matendo hatua kwa hatua, pamoja na kusherehekea sikuku baada ya hija

4.5Hijja na Umrah.
?Maana ya Hijja
Kilugha: Kuzuru au kutembelea mahali kwa lengo maalum.
Kisheria: Ni kuizuru Ka’abah, nyumba tukufu ya Makkah katika mwezi na siku
maalum kwa kuzingatia masharti na nguzo zote za Hija.



Maana ya Umrah
Kilugha: Ni kutembelea.
Kisheria: Ni kutembelea nyumba tukufu ya Ka’abah katika mwezi na siku yeyote
kwa kuzingatia sharti na nguzo za Umrah.



Tofauti kati ya Hijjah na Umrah.
Na. Hijjah Umrah
1. Hijjah ni faradh kwa muislamu mwenye uwezo mara moja kwa maisha yake yote. Umrah ni Sunnah iliyokokotezwa.
2. Hijjah ina muda maalum, hufanywa katika mwezi na siku maalum. Umrah haina muda maalum, hufanywa mwezi na siku yeyote.
3. Hijjah huchukua muda mrefu na hufanyikia ndani na nje ya Makka – Muzdalifa, Arafa na Mina. Umrah huchukua muda mfupi na hufanyikia ndani ya Makka kwa Kutufu, Kusai na Kunyoa tu.
4. Ibada ya Hijjah ina matendo mengi Ibada ya Umrah ina matendo machache.




Umuhimu na Nafasi ya Hijjah katika Uislamu.
i.Hijjah ni nguzo ya tano katika Uislamu iliyofaradhishwa kwa waumini.
Rejea Qur’an (3:97).

ii.Hijjah na Umrah ni ibada za hali ya juu na zenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w).

iii.Kuacha ibada ya Hijjah kwa mwenye uwezo kwa kukusudia anastahiki adhabu mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (3:97).

iv.Kuhiji ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa waumini wenye uwezo wa kimali na afya.



Wanaowajibika kuhiji.
- Waislamu wenye sifa zifuatazo wanalazimika kuhiji;
a)Waliobaleghe – Watoto wadogo hawawajibiki kuhiji hata kama wana uwezo,
hata hivyo wanaruhusiwa chini ya uangalizi wa wazazi wao.
b)Wenye Akili timamu – Asiye na akili timamu hawajibikiwi kwa ibada yeyote
ile katika Uislamu.



c)Waungwana – Wafungwa au watumwa hawawajibiki kwa Hijja mkapa
watakapokuwa huru.



d)Wenye uwezo – Waislamu wote wenye uwezo kimali na afya njema ni wajibu
kutekeleza ibada ya Hijjah.



e)Wasio katika kizuizi – Waliowekewa kizuizi au kuzuiliwa kwa sababu za
kiusalama sio wajibu kwao kuhiji muda huo.



f) Wanawake waongozane na maharimu wao.
–Mwanamke mwenye uwezo atawajibika kuhiji iwapo ataongozana na
maharimu wake.



Mwenendo wa mwenye kunuia Hijja au Umrah.
- Ajiepushe na kauli na vitendo viovu na vichafu.
- Azidishe kusoma Qur’an na kusimamisha swala za faradh kwa jamaa na kusimamisha swala za sunnah kwa wingi.
- Kuomba msamaha na kutubu kikweli kweli kwa Allah (s.w).
- Kujitahidi kujipamba na kila tabia njema na kuamiliana kwa wema na wanahajj wengine.
- Ajitahidi kujumuika na wanahajj kutoka sehemu mbali mbali Ulimwenguni.
- Ajiepushe na matamanio wanapokuwa katika mchanganyiko wa wanaume na wanawake katika Hijja.



Vituo vya Kunuia Hijja au Umrah.
- Miiqaat, ni vituo vya kunuia Hijjah na Umrah.
- Vituo vitano alivyoviweka Mtume (s.a.w) ni;
(a)Zul-Hulaifa (Bir-‘Ali).
- Ni cha watu watokao Madinah, kiko kilometa 450 kutoka Makkah.

(b)Juhfah (Rabigh).
- Ni cha watu watokao Misri na Syria, kiko kilometa 187 kaskazini-magharibi ya Makkah.

(c)Qurnul-Manaazil (Sail).
- Ni kituo cha watu watokao Najd, kiko kilometa 94 mashariki ya Makkah.

(d)Makkah.
- Ni kituo cha wakazi wa Makkah na wale wanao nuia Hija mwezi 8, Dhul-Hijah.

(e)Yalamlam.
- Ni kituo cha watu watokao Yemen, Afrika Mashaiki na Afrika Kusini, kiko kilometa 54 kusini-magharibi ya Makkah.

(f)Dhaaru-Iraq.
- Ni kituo cha watu kutoka Iraq, Iran, n.k., alichokiweka Khalifah Umar Ibn Khatwaab (r.a) wakati wa ukhalifah wake.
- Kiko kilometa 94 kaskazini –mashariki ya Makkah.

(g)Jiddah.
- Ni kituo cha wasafiri wa ndege, kiko kilometa 72 kusini ya Makkah.



Yaliyoharamishwa kwa mwenye kuwa katika Ihram.
-Kufanya jimai (tendo la ndoa), kubusu, kukumbatiana au kufanya ushawishi wowote wa kimapenzi kati ya mume na mke.

-Kusema au kutenda mambo machafu na maovu.
Rejea Qur’an (2:197).

-Kunyoa nywele, kukata kucha, au kupunguza sehemu yeyote ya mwili isipokuwa kwa udhuru, kama matibabu, n.k.

-Kuoa, kuolewa, kutoa posa au kufanya mipango ya ndoa.
-Kujipaka manukato au kuvaa nguo zenye kuvutia.
-Kuvaa nguo iliyoshonwa na kufunika kichwa kwa wanaume.
-Kufunika uso na viganja vya mikono kwa wanawake kwa kuvaa gloves.
-Kuvaa viatu vya kufunika miguu na kuvaa soksi.
-Kuwinda au kusaidia kuwinda hata kwa kuonyesha mnyama anayewindwa.
-Kula nyama iliyowindwa au iliyopatikana kwa msaada wa mtu aliyekuwa katika Ihram.
-Kula mayai ya ndege waliopatikana kwa kuwindwa.



Aina za Hijjah.
-Kuna aina kuu tatu za Hijah ambazo Hajj ana uhuru wa kuchagua kulingana na uwezo wake.

a)Ifraad.
- Ni aina ya Hijja amapo Hajj anavaa Ihram kwa nia ya kufanya Hijjah tu bila ya Umrah.
- Huanza kwa Talbiya; “Allaahumma labbaykal-Hijja” – ‘Nimeitika kwa Hijjah’
- Hajj huvaa Ihram mpaka amalize matendo yote ya Hija mwezi 10, Dhul-Hijjah.
- Hajj halazimiki kuchinja siku ya mwezi 10, Dhul-Hijah.

b)Qiran.
- Ni aina ya Hija ambapo Hajj hunuia kufanya Hija na Umrah pamoja.
- Hajj huitika kwa Talbiya; “Allaahumma labbaykal-Hijja wal-Umrata” – ‘Nimeitika kwa Hijjah na Umrah.’

- Hajj huwa katika Ihram mpaka alenge mawe minara mitatu, atufu Tawaful-Ifaadha na kunyoa mwezi 10, Dhul-Hijjah.

- Hajj analazimika kuchinja mnyama.
- Aina hii ya Hija hufanywa na wakazi wa Makka na wale waliokuja na wanyama.

c)Tamattu.
- Ni aina ya Hijah ambapo Hajj hunuia kufanya Umrah tu, kwa kuitika; “Allaahumma labbaykal-Umrah” – ‘Nimeitika kwa Umrah.’

- Hajj huvua Ihram baada ya kufanya matendo yote ya Umrah na kunyoa na kuwa huru na miiko ya Ihram.

- Hajj huvaa tena Ihram siku ya mwezi 8, Dhul-Hija na kuitika; “Allaahumma labbaykal-Hijjah” – ‘Nimeitika kwa Hijjah.’

- Hajj atavua tena Ihram baada ya kutupa mawe na kunyoa mwezi 10, Dhul-Hija.
- Hajj atalazimika kuchinja mnyama siku ya mwezi 10, Dhul-Hija kwa kununua mnyama kama hakuja nayo. Qur’an (2:196).

- Aina hii ya Hija ni bora na nafuu kwa wanaotoka mbali na hawana wanyama wa kuchinja.



Matendo ya Hija na Umrah.
1.Ihram na Nia ya Hija na Umrah.
- Ihram huvaliwa nyumbani au katika vituo (miiqaat) vya kunuia Hija na Umrah.
- Nia ya Hija na Umrah hufanyika katika miiqaat baada ya kuswali rakaa mbili.
Rejea Qur’an (22:27-28).

2.Talbiya.
- Ni maneno ya kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (s.w) kulingana na aina ya Hija anayokusudia Hajj.
- Maneno haya huanzia miiqaat hadi kufikia Ka’abah.

3.Tawafu.
- Ni kitendo cha kuizunguka Ka’abah mara saba kuanzia kona ya jiwe jeusi (Hajaral-aswad) kwa kulibusu au kuligusa kwa kidole au kuashiria.

- Mzunguko hufanywa kwa mwelekeo wa kinyume na mwendo wa saa (Ant-clockwise direction).

- Tawafu hufanywa mtu akiwa katika twahara, Hajj akikatisha tawafu kwa udhuru wowote ule, ataanzia pale alipokatishia.



Aina za Tawafu.
a)Tawaful-Quduum.
- Ni tawafu (ya Umrah) inayofanywa mara tu baada ya kuingia Makkah kwa ajili ya Hija au Umrah.

- Wanaume huvalia vipande viwili vya shuka, moja kiunoni na nyingine hufungwa lubega kwa kuacha wazi bega la kushoto (Iztibaa).

- Wwanaume hutembea mwendo wa matiti (jogging) (kukimbia - Ramal) mizunguko ya tatu ya mwanzo na minne iliyobaki kawaida.

b)Tawaful – Ifadha (Tawafu ya Nguzo).
- Ni tawafu ya Hija inayofanywa siku ya mwezi 10, Dhul-Hija. Pia inaitwa Tawafuz-Ziyaara.
- Hakuna Iztibaa na Ramal katika tawafu hii.



c)Tawaful-Widaa.
- Ni tawafu ya kuaga inayofanyika baada ya kumaliza Umrah au Hija tayari kurejea majumbani mwao.



4.Kusa’i.
- Ni kitendo cha kutembea mara saba baina ya vilima viwili vya ‘Saffa’ na ‘Marwa’ kwa kuanzia ‘Saffa’ na kuishia ‘Marwa.’
Rejea Qur’an (2:158).

- Aliyenuia Umra tu, baada ya kusai atanyoa na kuwa huru na masharti ya Ihram.
- Walionuia Hija ya Qiran na Ifrad watabakia katika Ihram na hawatanyoa.



5.Siku ya Tarwiya (mwezi 8, Dhul-Hija).
- Ni siku ya mwezi 8, Dhul-Hija ambapo Mahujaji huondoka Makka kuelekea Mina kabla ya Adhuhuri.

- Swala zote tano huswaliwa Mina kwa wakati wake, Adhuhuri hadi Alfajir ya mwezi 9, Dhul-Hija kwa kuzifupisha lakini bila kuzikusanya mbili mbili.



6.Siku ya Arafa (mwezi 9, Dhul-Hija).
- Arafa ni bonde lililo baina ya vilima vitatu.
- Siku ya Arafa ni mwezi 9, Dhul-Hija ambapo Mahujaji husimama (hukaa) katika uwanja wa Arafa na kuomba dua mbali mbali na maghufira kuanzia Adhuhuri hadi kukaribia kuzama jua.

- Kabla ya maghribi kuingia, Mahujaji huondoka Arafa na kuelekea Muzdalifa.
Rejea Qur’an (2:199).




7.Kulala Muzdalifa.
- Muzdalifa ni kitongoji kilichopo baina ya Arafa na Minah.
- Mahujaji huswali Magharib na Isha na kulala humo na kuswali Alfajir kabla ya kuelekea Minah.

- Wakiwa njiani kuelekea Minah, Mahujaji huokota vijiwe saba kwa ajili ya kulenga mnara mkubwa watakapofika Minah.
Rejea Qur’an (2:198).



8.Siku ya kuchinja (mwezi 10, Dhul-Hija).
- Matendo ya siku ya kuchinja ni pamoja na;
i.Kutupa mawe kwenye mnara mkubwa – Jamatul-Aqaba.
ii.Kuchinja mnyama kwa wenye kuhiji Hija ya Tamattu na Qiran.
iii.Kunyoa kichwa kwa wanaume na kupunguza kwa wanawake.
iv.Kutufu tawaful-ifadha (Tawafu ya Nguzo).



9.Siku za Tashriq (mwezi 11-13, Dhul-Hija).
- Ni siku za mwezi 11-13, Dhul-Hija.
- Mahujaji hukaa kambini Minah na kutupa vijiwe saba kila mnara katika minara mitatu pindi linapopinduka jua.

-Huswaliwa swala za faradh kwa wakati wake bila kuzikusanya, lakini kwa kuzipunguza rakaa.



10.Tawaful - Widaa.
- Ni tawafu ya kuaga baada ya Hajj kukamilisha matendo yote ya Hija au Umrah na tayari kurejea makwao.
- Tawafu hii haina ‘Ramal’ na ‘Iztibaa.’. Rejea Qur’an (2:203).

?Matendo (mambo) yanayobatilisha Hija pindi yasipotekelezwa.
i.Nia au Ihram isipotekelezwa kwa kufuata masharti yake ipasavyo.
ii.Sai (kati ya Saffa na Marwa).
iii.Kuhudhuria katika uwanja wa Arafa mwezi 9, Dhul-Hija.
iv.Tawaful-Ifadha (Tawafu ya Nguzo).



Umuhimu wa siku ya Iddil-Haj na Sunnah ya kuchinja.
-Ni siku ya kumshukuru na kumtaja sana Allah (s.w) kwani ndiye aliwezesha Ibada ya Hija kukamilika.
-Ni siku ya kujipumzisha baada ya ibada ngumu na misukosuko mingi.
-Ni siku ya kufurahi na kujumuika pamoja kutathmini utekelezaji wa ibada za Hija.
-Ni siku ya kuonyesha utayari wetu wa kujitoa muhanga kwa ajili ya kupigania Uislamu kwa kuchinja vile tulivyoruzukiwa.
-Ni kuiga na kufuata mila ya Baba yetu Nabii Ibrahim (a.s).



                   



           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 733


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Jinsi uislamu ulivyokomesha biashara ya utumwa wakati na baada ya mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzuru makaburi na dua zinazosomwa wakati wa kuzuru kaburi
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika katika kuzuru kaburi la muislamu. Soma Zaidi...

Tofauti ya uchumi wa kiislamu na uchumi wa kikafiri
Uchumi wa kiislamu unatofautiana sana na uchumi wa kikafiri. Hapa utajifunza tofauti hizo. Soma Zaidi...

Historia na asili ya kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango
Soma Zaidi...

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...

Hukumu na sherei zinazohusu ajira na kazi katika uislamu
Wajibu wa KufanyakaziUislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada. Soma Zaidi...

Warithi wasio na mafungu maalumu katika uislamu
Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi. Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti kabla ya kufa na baada ya kufa, mambo muhimu anayopasa kufanyiwa maiti wa kiislamu
3. Soma Zaidi...

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga
Soma Zaidi...

Mambo ambayo hayafunguzi funga
Hii ni orodha ya mambo ambayo hayawezi kuharimu funga yako endapo utayafanya. Soma Zaidi...

Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka
Soma Zaidi...

Yanayofaa kwa maamuma katika kumfata imamu kwenye swala ya jamaa
Soma Zaidi...