hukumu na taratibu za biashara ya ushirika na hisa katika uislamu
Mali yenye kuchangiwa mtaji kwa hisa
Mtu akishaamua kuuza hisa (share) kwa watu wengine kwa ajili ya mali fulani katika sheria ya Kiislamu anapoteza umilikaji wa mali wa mtu mmoja. Kuuza hisa kwa wengine kwa maana nyingine ni kukaribisha watu wengine kushiriki katika umilikaji wa mali ile. Nafasi ya mtu katika kumiliki mali hiyo itategemea idadi ya hisa alizonazo katika mali ile. Wenye hisa inabidi washirikiane katika faida na hasara pamoja na gharama za uendeshaji.
Faida anazopata atakayekuwa mwenye kumiliki mali
Zipo faida kadhaa ambazo atakayekuwa mwenye kumiliki mali huzipata kwa kufuata ushirika katika biashara, mtaji na faida (Shared Equity and rental) badala ya kupata mikopo ya biashara yenye riba. Faida kubwa atakayopata ni fadhila za Allah (s.w.) kwa kule kuepuka kwake kutoa riba kwa mkopo atakaopata. Tunajifunza katika Hadithi za Mtume (s.a.w.) kuwa laana ya Allah (s.w.) huwafikia wote wanaohusika na riba (mtoaji, mpokeaji, shahidi). Hata hivyo kuna faida nyingine ambazo anaweza kuzipata:
(i) Atakayekuwa mwenye kumiliki mali kwa kutochukuwa mkopo wenye masharti ya riba hujiepusha kabisa na hatari ya kunyangβanywa mali yake (aliyoweka rahani) akishindwa kutimiza masharti yake.
(ii)Fedha ambayo angeitoa kama riba kwa ajili ya mkopo atabaki nayo na kutumia kwa shughuli nyingine kuendeshea maisha yake.
(iii)Atakuwa na uhakika wa kupata sehemu halali ya faida inayotokana na mali hiyo (kama ipo). Kadhalika kama ikitokea hasara haitamlazimu kubeba mzigo wote wa hasara kwani ushirika katika biashara huhusisha vile vile umuhimu wa kugawana hasara itokeapo.
Faida kwa wenye kununua hisa
Mwenye kununua hisa huchangia katika mtaji. Naye huepuka ghadhabu za Allah (s.w.) za utoaji mkopo kwa riba. Zaidi ya haya hupata faida zifuatazo:
(i) Hupata sehemu ya faida itokanayo na mali hiyo kulingana na mchango wake kwenye biashara (idadi ya hisa alizonazo).
(ii) Huwa na sauti kwenye mali kwani naye pia ni mwenye kumiliki mali ile mpaka atakapouza hisa zake. Isitoshe hutoa kiwango kidogo kujipatia haki ya kumiliki ukilinganisha na mtaji mzima.
Kwa ujumla jamii nzima itanufaika kwa kuacha mfumo wa mikopo kwa riba na kuhimiza watu kufanya ushirika katika biashara. Ilivyo waliokopeshana kwa riba hawawi katika uhusiano mzuri kiroho. Aliyekopeshwa ilimbidi kufanya hivyo kutokana na shida aliyokuwa nayo. Kutoa kwake riba anakufanya kwa kuwa anafahamu hatari za kutofanya hivyo (kupoteza mali yake) ingawa kitendo hicho kinamuuma sana rohoni. Hivyo urafiki kati ya mkopeshaji na mkopeshwaji huwa ni wa kinafiki. Jambo hili ni wazi sana katika jamii ya dunia ya sasa. Hebu fikiria athari za mikopo hii kwa nchi masikini duniani. Ni mara nyingi nchi masikini zimekuwa zikipiga kelele aidha kupunguziwa au kufutiwa kabisa baadhi ya madeni yao. Sehemu kubwa ya madeni hayo ni limbikizo la riba la miaka mingi.
Hivyo Uislamu unapiga vita riba kutokana na madhara yake kibinafsi, kitaifa na kimataifa. Aidha Uislamu unahimiza ushirikiano katika biashara kama ufumbuzi wa tatizo la riba.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 Dua za Mitume na Manabii π3 ai web app π4 Madrasa kiganjani π5 Bongolite - Game zone - Play free game π6 web hosting
Post zinazofanana:
Namna ya kutawadha yaani kuchukuwa udhu
Kuchukuwavudhu ni ibada, lakini pia ni matendo ya kuufanya mwilivuwe safi. Katika post nitakwenda kukifundisha namna ya kutia udhu katika uislamu.
Soma Zaidi...Mafungu ya urithi katika uislamu
Hspa utajifunza viwango maalumu vya kutithi mirathi ys kiislamu.
Soma Zaidi...Mgawanyiko katika kuitumia mali unayomiliki
Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako.
Soma Zaidi...