picha

Swala ya kuomba mvua swalat istiqaa na jinsi ya kuiswali.

Hapa nitakujulisha kuhusu swala ya kuomba mvia, na taratibu za kuiswali.

12. Swala ya Kuomba Mvua - (Swalatul Istisqaa)’

Istisqaa ina maana ya kuomba maji. Uislamu unatuhimiza kumuelekea Allah kwa msaada wakati wa matatizo na dhiki. Kwa hiyo panapokuwa na ukame Waislamu wanahimizwa kumuomba Allah(s.w)kwa unyenyekevu katika jamaa. Maombi haya yanajulikana kama “Swalatul Istisqaa”. Kutokana na Hadithi mbali mbali maombi haya yanaweza kuombwa katika namna tatu zifuatazo:

 


(a)Kuomba Dua bila ya swala.
(b)Kuomba dua katika khutuba ya Ijumaa au mwisho wa swala za faradhi.
(c)Namna ya tatu ambayo ni muhimu sana ni ile ya kuswali rakaa mbili zinazofuatiwa na khutuba na kumalizia na Dua.
Maombi haya hapana budi yaombwe kwa unyenyekevu mkubwa ukiambatana na imani kamili juu ya uwezo waAllah usio mipaka.

 


Swalatul Istisqaa Inavyoswaliwa

 


Swala hii ni sunnah iliyokokotezwa wakati wa ukame na huswaliwa katika jamaa uwanjani kama inavyo swaliwa swala ya Idd. Kama swala ya Idd katika rakaa ya kwanza kuna takbira saba baada ya Takbira ya kuhirimia na kuna Takbira tano kabla ya kuanza Suratul Fatiha katika rakaa ya pili. Ni sunnah katika rakaa ya kwanza, baada ya Al-fatiha kusoma Surat-Qaf au Al-A’laa na katika rakaa ya pili kusoma baada ya Alfatiha. suratul-Qamar au Al-Ghashiyah. Imamu ni sharti awe kiongozi wa ngazi ya juu au naibu wake anayeshughulikia mambo ya Waislamu.

 


Swala hii hufuatiwa na khutuba mbili kama ilivyo katika khutuba za Idd. Ni sunnah Imamu kuleta istighf'aari mara tisa kabla hajaanza khutuba ya kwanza na ya pill.

 

Istighfaari hii ni kusema
"Astaghafirullahil-aladhim alladhii laa ilaaha illa huwal-hayyul-qayyuum-almudabbiru kullu-shayin wa-atubu ilaihi"

 

Ni sunnah wakati wa kuomba dua kugeuza mikono au kuelekeza mbinguni migongo ya viganja vya mikono . Tunafahamishwa hill katika Hadith za Mtume (s.a.w) zifuatazo kuwa:
Abduilah blrs 7.aid Al-Arrsarl (r.a) amesimuiia kuwa Mtume (s.aw) aWaaenda rye ya rryi Qi Iwswali swaIatu1-IsiisgaaAUpotaka. kuorrtba dua, alielekea Qibia nra alaageura. kiiemba choke. (Muslim).
Arras bin MaWc (r.a) amestmuIia kuu~a Mturne (s.a w) katika kuomba dua ya mvua alielekaezaJuu mtgongo yaviganfa uyake vya miknno. (Muslim).

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 2326

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 ai web app     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Mifumo ya benki na kazi zake

Hapa utajifunza kazi za benki.

Soma Zaidi...
Mambo yaliyo haramu kwa mwenye hedhi na nifasi

Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi

Soma Zaidi...
Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu

Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?

Soma Zaidi...