Post hii inahusu zaidi dawa ya Nystatin ni mojawapo ya dawa ambayo utumika kwenye ngozi.
1. Ni mojawapo ya dawa inayotumika kutibu fungasi za kwenye ngozi tu, pia iko kwenye mfumo wa mafuta mafuta hivi, au oil, cream kwa hiyo upakwa kwa mafuta.ni vizuri kabisa kutumiwa kwenye ngozi tu ikitumia kwa namna nyingine ni hatari kwa hiyo ni vizuri kuwaambia watumiaji kwamba makini katika kutumia dawa hii kwa sababu ikitumiwa vinginevyo tofauti na kwenye ngozi ni hatari sana.
2.pia dawa hii haiwezi kumengenywa kama dawa nyingine ambazo umengenywa kwenye mfumo wa chakula ndio maana ni hatari sana ikitumika kwenye system ya chakula, pia dawa hii usaidia kwenye kandida za sehemu mbalimbali kwa mfano dawa hii inaweza kutibu kandida ya kwenye sehemu za siri kwa kupaka dawa hiyo kwenye sehemu za siri.
3. Namna ya kutumia dawa hizi, unanawa mikono kwanza ili kuepuka kuingiza wadudu kwenye dawa , unakuwa tayari umeshasafisha sehemu ambayo unataka kupaka dawa hiyo ,unakaushaa sehemu hiyo vizuri kwa kitambaa kizuri,unapaka dawa yako kadri ya maelekezo ya wataalamu wa afya, kama ni sehemu za siri ni vizuri kabisa kutumia dawa hiyo wakati wa kupumzika au wakati wa usiku ili kuruhusu dawa ifanye kazi yake vizuri.
4. Pengine anayetumia dawa ni mgonjwa ambaye hajiwezi ni vizuri kabisa kumpaka au pengine ni mtoto ambaye hawezi kujihudumia mwenyewe ni vizuri kumpaka na kuzingatia kwamba hakuna kusambaza ugonjwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, pia kabla ya kutumia dawa nyingine baada ya kujipaka ni vizuri kabisa kuoga dawa ile ya kwanza na hakikisha unazingatia usafi katika matumizi ya dawa hii.
5. Katika matumizi ya dawa hii zingatia kwamba dawa hii utumika kwenye ngozi ya nje tu na ikitumiwa kwa njia yoyote ni hatari kwa afya kwa hiyo ni vizuri kabisa kuweka dawa hii mbali na watoto ili kuepuka hatari ya kutumia dawa hii kama mafuta au pengine wanaweza Kulamba au kula na mambo kama hayo, kwa hiyo ni vizuri kabisa kutumia dawa hizi kwa ushauri wa wataalamu wa afya kwa sababu bila ushauri wao matumizi mengine yanaweza kuwa sio sahihi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali za kutibu minyoo, tunafahamu kabisa minyoo ni ugonjwa ambao uwapata watu mbalimbali hasa watoto.
Soma Zaidi...Fangasi wanaweza kushambulia uke, kwa juu kwenye mashhav ya uke ama kwa ndani. Hali hii inaweza kusababisha miwasho na maumivu pia. Inaweza kusababisha michubuko na kutofurahia tendo la ndoa. Makala hii inakwenda kukujuza dawa na matibabu ya fangasi ukeni
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya ALU ila kwa jina jingine huitwa dawa ya mseto,ni aina ya dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ,ni dawa ambayo utumiwa na watu wengi kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo,dawa maalum ambayo imo kwenye kundi hili la cardiac glycoside ni digoxin, ni dawa muhimu ambayo utumika kwenye mfumo wa vidonge mara nyingi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa aina ya expectorant katika matibabu ya kikohozi,ni dawa ambayo usaidia au uzuia kikohozi kuendelea kutokea.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia dawa za ARV kwa wathirika wa virusi vya ukimwi .pia tutangalia kwa undani mambo ya kuzingatia kwa wathirika wanaotumia ARV .pamoja na kujali watu wanaotumia dawa hizo .
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya Tiba mionzi kwa wagonjwa wa saratani, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wanaotumia mionzi katika matibabu ya saratani.
Soma Zaidi...Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote
Soma Zaidi...