Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu
DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO
Dawa za vidonda vya tumbo zinategemea aina za vidonda alivyo navyo, mahala vilipo na sababu za vidonda hivyo. Kitu cha kwanza kuangalia ni sababu gani zilizopelekea vidonda hivyo?. kisha baada ya kuijuwa sababu ndipo maibabu yatafuata. Kama tulivyokwisha jifunza kuwa sababu kuu za vidonda vya tumbo ni bakteria aina ya Hypylori. Hivyo kama sababu ni hii mgonjwa atapewa dawa ya kuwauwa hawa bakteria. Pia kama sabau ni asidi tumboni atapewa dawa za kupunguza uzalishwaji wa hizi asidi. Dawa za vidonda vya tumbo ni kama zifuatazo:-
1.Dawa kwa ajili ya kuuwa bakteria. Hapa mgonjwa atapewa dawa kama:-
A.Amoxicillin (amoxil)
B.Clarithromycin (Biaxin)
C.Metronidazole (flagyl)
D.Tinidazole (tindamax)
E.Tetracyline
F.Levolaxacin
2.Dawa za kuzuia uzalishwaji wa asidi mwilini (proton pump inhibitors (PPIs))
A.Omeprazole (Prilosec)
B.Lansoprazole (Prevacid)
C.Rabeprazole (Aciphex)
D.Esomeprazole (Nexium)
E.Panztoprazole (Protonix)
3.Dawa za kupunguza uzalishwaji wa asidi tumboni (Acid blockers (histamine (H-2))
A.Famoditine (Pepcid AC)
B.Cimetidine (Tagamet HB)
C.Nizatidine (Axid AR)
4.Dawa zinzzolinda ukuta wa utumbo na tumbo
A.Cytoprotective agents
B.Sucralfate (Carafate)
C.Misoprostol (Cytotec)
TIBA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO.
Wataalamu wa afya pia wanakubali uwepo wa tiba mbadala katika kutibi vidonda vya tumbo. Zipo nyingi sana, miongoni mwazo ni:-
A.Bamia
B.Kitunguu thaumu
C.Asali
Kwa nini vidonda haviponi hata baada ya kutumia dawa?
Hii hutokea endapo:-
A.Kama mgonjwa hakutumia dawa kwa kufuata masharti vyema
B.Haswa kuna baadhi ya bakteria wa vidonda vya tumbo wana usugu wa kufa na dawa
C.Kama unatumia tumbaku
D.Kama unatumia dawa za NSAIDs
Pia mara chache vidonda vya tumbo vinaweza kusababishwa na:-
A.Uzalishwaji wa asidi kupitiliza
B.Mashambulizi mengie yasiyo ya H.pylori
C.Saratani ya tumbo
D.Kuwa na maradhi mengine
Umeionaje Makala hii.. ?
Zipo dawa nyingi ambazo hufahamika katika kutibu fangasi kwenye mdomo ama kinywa. Miongoni mwa dawa hizo hapa nitakuletea baadhi yao. kama wewe pia unasumbuliwa na fangasi wa mdomo basi post hii itakusaidi sana.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa zinazosaidis katika kutuliza magonjwa ya akili, dawa hii kwa kitaamu huiitwa chlorpromazine ni dawa ambayo utumiwa na watu wenye tatizo la magonjwa ya akili na kwa kiasi kikubwa huwa sawa.
Soma Zaidi...Nitakujuza dalili za UTI na dawa za kutibu UTI. Pia tutaona njia za kujikinga na UTI pamoja na dalili za UTI
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu,ni dawa ambayo upunguz maumivu ya Kawaida, kushusha homa na pia usaidia kwenye magonjwa ya moyo hasa kuzuia stroke kama imetokea mda ndani ya masaa ishilini na manne
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya macrolide ni mojawapo ya dawa ya kutibu au kupambana na bakteria na upambana na bakteria wafuatao streptococcus pyogenes, staphylococcus aureus na haihusiki na haemophilia influenza ambao usababisha maambukizi kwenye mfumo w
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole ni mojawapo ya dawa ambazo usaidia kutibu minyoo, na pia imefanikiwa sana kadri ya watumiaji wa dawa hiyo.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na maumivu ya hedhi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu ambao wana uwezo wa kutumia vidonge vya zamiconal, ni baadhi ya watu au makundi yanayoweza kutumia vidonge hivi.
Soma Zaidi...