Fahamu dawa ya Prednisone katika kupambana na aleji
Post hii inahusu zaidi dawa ya Prednisone ambayo usaidia katika kupambana na aleji.
Ifahamu dawa ya Prednisone katika kupambana na aleji
1. Prednisone ni mojawapo ya dawa ambayo imependekezwa kutuliza aleji kwa watu wenye tatizo hili kwa sababu Kuna wale ambao Wana tatizo la aleji lakini hawawezi kutumia dawa ya hydrocortisone kwa hiyo dawa nyingine ambayo upendekezwa ni Prednisone.
2. Pamoja na kutuliza aleji ambazo zimesababishwa na dawa pamoja na vyakula dawa hii pia ufanya Kazi kwa wagonjwa wa asthma na pia kwa watu wanabanwa na kifua kwa sababu mbalimbali kwa hiyo dawa hii ni nzuri na pia imesaidia watu wengi sana.
3. Dawa hii utumika kwa mdomo mara nyingi na pia milligrams ubadilika kulingana na hali ya mgonjwa, hali ikiwa mbaya au aleji imekuwa kubwa kuzidi kiasi ya milligrams sitini inaweza kutumika na pia kadri aleji inavyopungua milligrams thelathini mpaka arobaini zinaweza kutumika, na ushauri wa wataalamu wa afya ni muhimu sana.
4. Dawa hii inapaswa kutumiwa na watu mbalimbali ila wale wenye tatizo la presha ya kupanda wanapaswa kuitumia kwa taahadhari na pia kwa wale ambao wametumia ila hawakupata nafuu wanapaswa kubadilishiwaa dawa hii na kutumia dawa nyingine ambayo inafaaa kabisa. Na kwa upande wa wagonjwa wa asthma ni vizuri kuitumia kwa uangalifu sio Mda wote kukaa wanaitumia kwa sababu inaweza kuwaletea shida kwenye mapafu.
5. Vile vile dawa hii Ina maudhi madogo madogo kama vile mapigo ya moyo kwenda mbio, matatizo kwenye mapafu iwapo kama imetumika mara nyingi na kwa kiasi kikubwa na pia baada ya kupona mgonjwa anaweza kuhisi Hana nguvu na maumivu ya kichwa pia yanaweza kutokea.
6. Dawa hii inapaswa kutumiwa kulingana na wataalamu wa afya sio kuitumia kiholela.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Fahamu kuhusu dawa ya parental Artusnate dawa ya kutibu malaria sugu
Post hii inahusu zaidi dawa ya Parental Artusnate ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria sugu kama tutakavyoona hapo baadaye.
Soma Zaidi...Dawa ya kutibu maumivu ya jino
Utaijuwa Dawa ya maumivu ya jino, sababu za maumivu ya jino na njia za kujikinga na maumivu ya jino
Soma Zaidi...Namna ya kutumia tiba ya jino.
Posti hii inahusu zaidi namna au njia ya kufanya Ili kuweza kutumia tiba hii ya jino, kwa sababu ya mchanganyiko ambao umekwisha kuwepo kwa hiyo unachumua mchanganyiko unafanya kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Faida za vidonge vya zamiconal
Posti hii inahusu zaidi faida za vidonge vya zamiconal, ni baadhi ya faida ambazo upatikana kutokana na vidonge vya zamiconal,ni vidonge ambavyo utibu au kusaidia kwenye matatizo ya viungo vya uzazi.
Soma Zaidi...Mgawanyo wa tiba ya kifua kikuu
Post hii inahusu zaidi mgawanyiko wa tiba ya kifua kikuu, kwa kawaida tiba hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Soma Zaidi...