Posti hii inahusu zaidi dawa ya lsoniazid nA kazi zake, ni dawa ambayo inasaidia kutibu kifua kikuu kati ya madawa yaliyoteuliwa na kuwa na sifa ya kutibu kifua kikuu.
Dawa ya Isoniazid na kazi zake.
1.Dawa ya Isoniazid ni dawa ambayo utumika katika vipindi vyote vya kutibu kifua kikuu yaanza kwenye kipindi cha kwanza na cha pili kwa hiyo dawa hii usaidia kufubaza bakteria ambao wanasababisha kifua kikuu na bakteria ushindwa kukua, dawa hii tunaweza kuikuta kwenye mfumo wa vidonge kwa mara nyingi na kwenye mfumo wa maji maji kwa watoto na pengine inaweza kutolewa kwa njia ya kulishwa kwenye mishipa ya damu au kwenye nyama.
2.Katika matumizi ya dawa hii tunapaswa kuwa makini hasa kwa akina Mama wanaotumia njia za uzazi wa mpango kwa sababu hii dawa umaliza nguvu kwa baadhi ya njia za uzazi wa mpango kwa hiyo unaweza kukuta Mama anatumia dawa hizi na njia za uzazi wa mpango akapata mimba kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii ni vizuri wakaonana na wataalamu wa afya ili kuchaguliwa njia sahihi na muhimu ambazo haziingilian na dawa hii.
3 Katika matumizi ya dawa hii ya Isoniazid kuna maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea kama vile matatizo kwenye ini kwa sababu dawa hii upitia kwenye ini, kichefuchefu, kutapika na kuharisha kwa hiyo Mgonjwa akiona dalili za namna hizi anapaswa kujua kuwa ni kwa sababu ya dawa na ikiwa Dalili hizi zimezidi anapaswa kwenda hospitalini ili kuweza kupata ushauri zaidi katika matumizi ya dawa hizi.
4.Pia tunaona kuwa dawa hii inafubaza wadudu wanaosababisha ugonjwa wa kifua kikuu na wagonjwa uweza kupona kwa hiyo tunapaswa kuwaleta wagonjwa wetu hospitali ili waweze kupata dawa na kuepukana na hali ya kusambaa kwa ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine maana ndio Tabia yake kama haujatibiwa uweza kusambaa kwa hiyo jamii inapaswa kujua madhara ya ugonjwa huu wa kifua kikuu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa aina ya expectorant katika matibabu ya kikohozi,ni dawa ambayo usaidia au uzuia kikohozi kuendelea kutokea.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa e quinine katika kutibu Malaria ni dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ikiwa dawa nyingine zimeshindwa kufanya kazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za dawa za NMN maana yake ni Nicotinamide mononucleotide ni dawa ambazo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya cephalosporin katika kupambana na bakteria, ni mojawapo ya kundi kati ya makundi ya kupambana na bakteria ambalo ufanya Kazi kama penicillin.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dawa ya Rifampicin na kazi zake, hii ni dawa mojawapo inayotibu kifua kikuu kati ya Dawa zilizoteuliwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi aina mojawapo ya dawa ya penicillin ambayo ufanya kazi kwa mda mrefu, dawa hii kwa kitaamu huiitwa procaine benzyl penicillin.
Soma Zaidi...kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka
Soma Zaidi...