Posti hii inahusu zaidi dawa ya Carvedilol na kazi yake, ni dawa inayotibu au kuzuia mapigo ya moyo ambayo yako juu na kusababisha kulegeza kwa mishipa ya moyo.
Kazi ya Carvedilol.
1. Dawa ya Carvedilol ni mojawapo ya Dawa ambazo usaidia kushusha presha kama iko juu , ufanya kazi hii kwa kuhakikisha kwamba mishipa ya moyo imelegezwa kwa sababu mishipa ya moyo kama imebana usababisha presha kuwa juu kwa hiyo dawa hii ikitumika usababisha mishipa kuregea na mapigo ya moyo kuwa kawaida.
2.pia dawa hii inatabia ya kushusha sukari, kwa hiyo mgonjwa wa matatizo ya moyo kabla ya kutumia Dawa hii anapaswa kupima kiwango cha sukari mwilini, kama iko chini hapaswi kutumia kwa sababu anaweza kushusha zaidi, kwa hiyo watu wenye matatizo ya sukari kushuka wanapaswa kuwa makini.
3.Dawa hii pia usaidia kuzuia kupatwa kwa ghafla ugonjwa wa moyo ambao kwa kitaalamu huitwa heart attack, ambapo mgonjwa uwea kuzimia ghafla na pengine kupoteza fahamu, pamoja na kuwepo kwa dawa hii ya Carvedilol kuna dawa Ambazo ufanya kazi kama ya Carvedilol ambazo ni Atenolo, propanol and labetalo, kwa hiyo dawa hizi zisitumike kiholela zinapaswa kutumika kwa ushauri wa daktari na wataalamu wengine wa afya.
4. Katika kutumia dawa hizi kuna maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea kama vile kizungu Zungu, mwili mzima kuchoka, kushuka sana kwa mapigo ya moyo, kuharisha kuongezeka kwa uzito, na kushusha sukari, kwa hiyo Mgonjwa akihisi dalili kama hizi anapaswa kujua kuwa ni kwa sababu ya dawa anazozitumia kwa hiyo maudhi mengine ni ya hatari yanapaswa kufanyiwa kazi mapema kama vile presha kushuka kuzidi kiasi kwa sababu hii ni hali ya hatari kwa mgonjwa.
5. Dawa hii haipaswi kutumiwa na watu mbalimbali kama vile wenye Asthma kali kwa sababu inaweza kupasua sehemu mbalimbali ambazo zinahusika kwenye mfumo wa hewa, kwa hiyo mwenye presha anapaswa kujua hili kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo kwenye upumuaji, hata mgonjwa anapaswa kuwa wazi pindi hawapo hospitali na inabidi ajieleze wazi ili kuepuka matatizo mengine na jamii inapaswa kujua matumizi mazuri ya Dawa hii.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu zaidi njia ya kupitisha dawa kwenye mdomo na vipengele vyake, hii njia dawa umengenywa kwenye tumbo na kupitia kwenye utumbo mdogo na baadae kwenye damu,
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya loperamide ni dawa ambayo inazuia kuharisha ni dawa inayofanya kazi kuanzia kwenye utumbo na pia usaidia kutuliza maumivu ya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ,ni dawa ambayo utumiwa na watu wengi kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya aminophylline katika kutuliza maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Soma Zaidi...Zipo dawa nyingi ambazo hufahamika katika kutibu fangasi kwenye mdomo ama kinywa. Miongoni mwa dawa hizo hapa nitakuletea baadhi yao. kama wewe pia unasumbuliwa na fangasi wa mdomo basi post hii itakusaidi sana.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...