Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu Primary Key na Foreign Key
Katika MySQL, Primary Key na Foreign Key ni mihimili muhimu ya kuboresha usimamizi wa data na kuwezesha uhusiano kati ya jedwali tofauti. Mihimili hii inahakikisha kuwa data inabakia thabiti, safi, na inayohusiana kwa usahihi katika mfumo wa database.
Primary Key ni kitambulisho cha kipekee cha kila rekodi kwenye jedwali. Kila jedwali linaweza kuwa na Primary Key moja tu, na thamani za Primary Key haziwezi kujirudia wala kuwa na thamani tupu (NULL).
CREATE TABLE Wanafunzi (
mwanafunzi_id INT AUTO_INCREMENT PRIMARY KEY,
jina VARCHAR(50),
darasa VARCHAR(10)
);
Hapa, mwanafunzi_id
ni Primary Key inayotambulisha kila mwanafunzi kipekee.
Foreign Key ni sehemu ya jedwali moja inayohusiana na Primary Key ya jedwali lingine. Inaonyesha uhusiano kati ya rekodi za jedwali tofauti.
CREATE TABLE Madarasa (
darasa_id INT AUTO_INCREMENT PRIMARY KEY,
jina_la_darasa VARCHAR(20)
);
CREATE TABLE Wanafunzi (
mwanafunzi_id INT AUTO_INCREMENT PRIMARY KEY,
jina VARCHAR(50),
darasa_id INT,
FOREIGN KEY (darasa_id) REFERENCES Madarasa(darasa_id)
);
Hapa, darasa_id
kwenye jedwali la Wanafunzi
ni Foreign Key inayohusiana na Primary Key ya Madarasa
.