DART somola 42: Asynchronous programming

Katika somo hili tutakwenda kujifunza concept nyingine ya asynchronous programming.

Asynchronous programming hii ni njia ya kuandika code ambazo zinaruhusu program kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Kama vile kusoma na kuandika taarifa za database kutoka kwenye internet, kusoma faili na kudownload. Hizi ni baadhi ya task ambazo hazihitaji kuw ainterrupted.

 

Synchronous programming hapa program ita run mstari baada ya mstari mara moja tu. ni kwa sababu hapa inahitaji shughuli zote zikamilike ndipo program ielekee kwenye shughuli inayofuata.

Mfano:

void main() {

 print("mwanzo");

 print("kati");

 print("mwisho");

}

Hapo program itaanza na mstari mw akwanza kisha itaprint unaofuata kisha unaofuata mpaka mwisho. Hii ni tofauti na asynchronous ambapo program itaendelea ku print mstari unaofuata bila ya kupoteza muda mapaka imalize shughuli za mstari uliotangulia.

 

Hivyo tunasema synchronous programming inahitaji kusubiria lakini asynchronous programming  haihitaji kusubiria. Hivyo basi asynchronous programming huboresha program.

Mfano  wa asynchronous:

void main() {

 print("mwanzo");

 Future.delayed(Duration(seconds:3),()=>print('kati'));

 print("mwisho");

}

 

Utaona hapo mstari unaoandika kati umetangulia lakini program imeprint mwisho. Hivyo iliendelea mstari unaofuata bila hata ya kusubiria mstari wa nyuma u print.

Kwa nini tunahitaji asynchronous

  1. Kwa ajili ya kusoma data kwenye insternet
  2. Kwa ajili ya kuandika data kwenye database
  3. Ku run program ambazo zinatumia uda mrefefu
  4. Kusoma data kwenye faili
  5. Ku download
  6. Na mengineyo mengi

 

Ili uweze kutumia asynchronous unatakiw akutumia class inayoitwa future pamoja na keyword kama async na wait. Tutajifunza zaidi kwenye somo linalofuata.

 

Baadhi ya misemo muhimu ambayo hutumika:

  1. Synchronous operation hizi ni zile operation (shuguli za program) ambazo huzuia program kufanya shughuli nyingine kabla ya kukamilisha shughuli za nyuma.
  2. Synchronous function hizi ni function ambazo hufanya synchronous operation
  3. Asynchronous operation ni operation ambazo zinaruhusu shuguli nyingine kufanyika kabla ya nyingine
  4. Asynchronous function ni function zinazofanya kazi kwenye asynchronous operation

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata utakwenda kujifunza kuhusu future  class kwenye dart.

 

 Future class

Katika somo hili utakwenda ujifunza kuhusu future class na jinsi ambavyo itakavyotumika kwenye dart.

 

Katika dart future huwakilisha value (thamani) ama error (tatizo) ambalo bado halijatokea, ila hutarajiwa kutokea wakati ujao.

 

Kwenye dart future hutengenezwa kwa kutumia future class. Hapa mwenyewe utachaguwa je itakee muda gani hiyo operation. Unaweza kuandika itokee baada ya sekunde ngapi ama dakika ngapi, unaweza kuchaguwa hata baada ya lisaa.

 

Mfano hapa nitakuletea mfano wa future ambazo operation itafanya kazi baada ya sekunde 2.

 

Kwanza utaanza kuandika keyword future ikifuatiwa na aina ya data ambayo unatarajia ku return kwenye hiyo ascynchronous operation fano kama ni string utaand">...

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: DART Main: ICT File: Download PDF Views 574

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

DART somo la 35: Enum kwenye Dart:

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu enum na inavyotumika kwenye Dart.

Soma Zaidi...
DART somo la 24: Jinsi ya kutengeneza faili, folda na kuingiza data

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika data kwenye faili. Kwanza utajifunza kutengeneza folda, kisha faili na kuweka data, kisha utajifunza kufuta fali.

Soma Zaidi...
DART somo la 34: Static variable kwenye Dart

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu static property na jinsi ambavyo inavyotumika.

Soma Zaidi...
DART somo la 43: Stream kwenye Dart

Katika somo hili utakwenda ujifunz akuhusu concept ya stream kwenye Dart. pia ttaona kwa namna gani strean inaweza kutofautiana na future wakati zote mbili zipo kwenye asychronous programming.

Soma Zaidi...
DART somo la 29: Dart encapsulation

Katika somo hili tutawenda kujifunza kuhusu encapsulatio kwenye Dart OOP na jinsi inavyoweza kutumika.

Soma Zaidi...
DART somo la 37: Class interface

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu class interface na inavyotofautiana na class abstract

Soma Zaidi...
DART somo la 3: Aina za Data

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data zinazotumika kwenye Dart.

Soma Zaidi...
DART somo la 20: method zinazotumika kwenye map data type kwenye Dart

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu method ambazo hutumika kwenye map data type

Soma Zaidi...
DART somo la 19: method zinazotumika kwenye set data type kwenye Dart

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.

Soma Zaidi...
DART somo la 44: Jinsi ya ku install mysql kwenye program ya dart

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuunganisha databse na Dart. Pia utajifunza jinsi ya kuset environment kwenye kompyuta ili kuweza kutumia Dart sdk kwenye CMD.

Soma Zaidi...