image

Kushuka na kuhifadhiwa kwa quran, hatua kwa hatua: mafunzo ya baadhi ya sura za quran

QUR’AN 5.

Kushuka na kuhifadhiwa kwa quran, hatua kwa hatua: mafunzo ya baadhi ya sura za quran

Kushuka na kuhifadhiwa kwa quran, hatua kwa hatua: mafunzo ya baadhi ya sura za quran

QUR’AN
5.1 Kushuka Qur’an.
Hatua mbili kuu za kushuka Qur’an;
i.Kushuka kwa jumla kutoka Lawhi-Mmahfuudh hadi mbingu ya Dunia.
ii.Kushuka kigodo kidogo kutoka mbingu ya Dunia kwenda kwa Mtume (s.a.w).- Qur’an ilianza kushuka mnamo mwaka 610 A.D, Mtume (s.a.w) akiwa na umri wa miaka 40.
- Qur’an ilikamilika kushuka kwa muda wa miaka 23 sehemu kidogo kidogo.
Rejea Qur’an (97:1), (2:185), (44:3).Hekima ya Qur’an kushuka hatua kwa hatua;
1. Ni kujibu hoja mbali mbali zilizotolewa na zilihitajia majibu ya kiwahyi.
2. Ni kuwezesha utekelezaji wa maamrisho yake kuwa rahisi au mwepesi.
3. Ili iwe rahisi kuhifadhika katika mioyo ya maswahaba.

5.2 Kuhifadhiwa kwa Qur’an.
- Mtume (s.a.w) aliwaamrisha maswahaba wake kujifunza na kuifahamu Qur’an na kuihifadhi moyoni.

-Mtume (s.a.w) aliteuwa baadhi ya maswahaba kuiandika Qur’an ilipokuwa inashuka.
-Kuhifadhiwa kwa kusomwa mara kwa mara.
-Qur’an pia ilihifadhika kwa kusomwa mara kwa mara katika ibada za swala.
5.3 Mafunzo ya sura zilizochaguliwa.
Suratul-Lahab (111): Imeteremshwa Makka; Ina Aya Tano.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1.Imeangamia mikono ya Abulahab naye amekwisha angamia.
2.Haitamfaa mali yake wala alivyovichuma (watoto).
3.(Atakapokufa) Ataingia moto wenye muwako (mkubwa kabisa).
4.Na mkewe (ni) mchukuzi wa kuni (za fitina).
5.(Kana kwamba) Shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa (anayechukulia kuni za fitina).


Mafunzo ya sura kwa ufupi.
1.Binaadamu siku zote huamua kumkanusha Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kibri na jeuri.
2.Mali na watoto havina msaada wowote pindi inapokuja adhabu ya Mwenyezi Mungu (s.w).
3.Watu waovu na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w) wana mwisho mbaya wa kuishia motoni.
4.Maadui wa Uislamu na waislamu siku zote hawakati tamaa katika kuzuilia watu kuingia na kuufuata Uislamu.
5.Uchochezi, fitina na uasi ni miongoni mwa makosa makubwa yenye kuangamiza.


Suratul-Nnasr (110): Imeteremshwa Madinah Ina Aya Tatu.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1.Itakapofika Nusura ya Mwenyezi Mungu na Kushinda.
2.Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi.
3.Basi (hapo) mtakase Mola wako pamoja na kumsifu na umuombe magh’fira (msamaha) hakika Yeye ndiye apokeaye toba.Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.
1.Nusura na mafanikio hutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.
2.Baada ya nusura na ushindi hatuna budi kumshukuru, kumtukuza na kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu (s.w) bila ya kujivuna.
3.Katika kufanya juhudi, hatuna budi kuchunga na kutii ipasavyo maarisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
4.Nusura na mafanikio ya kweli huja baada ya juhudi za dhati za kibinaadamu kufanyika na kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) vilivyo.
5.Mafanikio ya kweli sio kujilimbikizia mali na anasa za dunia tu, bali ni kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo.Suratul-Kaafiruun (109): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Sita.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1.Sema: Enyi Makafiri.
2.Siabudu mnachoabudu.
3.Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu.
4.Wala sitaabudu mnachoabudu.
5.Wala nyinyi hamtaabudu ninayemuabudu (mimi).
6.Nyinyi mna dini yenu na mimi nina dini yangu.


Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.
1.Dini ni utaratibu wowote ule wa maisha anaoufuata mtu.
2.Kuna dini nyingi hapa Ulimwenguni, Ukafiri nao ni dini.
3.Hakuna uwezekano wa mwanaadamu kufuata dini (utaratibu wa maisha) za ya moja kwa wakati moja, Uislamu na mifumo mingine.
4.Waislamu wa kweli ni wale wasiochanganya haki na batili kwa kuwahofia makafiri.
5.Ni wajibu kuitangaza haki kwa wengine bila kuhofia chuki na uadui wao dhidi ujumbe uliowapa.
Suraul-Kawthar (108): Imeteremshwa Makka, Ina Aya Tatu.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1.Hakika tumekupa kheri nyingi.
2.Basi swali kwa ajili ya Mola wako na uchinje (kwa ajili yake pia).
3.Hakika adui yako ndiye atakayekuwa mkiwa (atakatikiwa na kila kheri).Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.
1.Mafanikio hayapimwi kwa wingi wa mali na watoto, bali ni kuridhiwa na Mwenyezi Mungu (s.w).
2.Hakuna neema kubwa kama kujaaliwa kuupokea Uislamu, kuuelewa, kuufuata vilivyo na kuufikisha kwa wengine.
3.Hatuna budi kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake ipasavyo na kufanya kila jambo kwa ajili yake tu.
4.Maadui na Wapinzani wa Uislamu ndiyo wenye kupata khasara na kufedheheka duniani na Akhera pia.
5.Ushindi na mafanikio hupatikana kwa waislamu baada ya kutii na kufuata maamrisho ya Uislamu vilivyo.Suratul-Maaun (107): Imeteremshwa Makka, Ina Aya Saba.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1.Je, Unajua yule anayekadhibisha dini (asiyeamini malipo ya Akhera)?
2.Huyu ni yule anayemnyanyasa yatima.
3.Wala hajihimizi (yeye wala wengine katika) kuwalisha maskini.
4.Basi adhabu kali itawathubutikia wanaoswali.
5.Ambao wanapuuza (maamrisho ya) swala zao.
6.Ambao hufanya riyaa (ya kujionyesha kwa watu).
7.Nao hunyima misaada (midogomidogo kwa wanaohitajia).Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.
1.Imani katika Uislamu hudhihirishwa katika matendo ya mtu na sio kauli au maneno tu.
2.Kuwadhulumu, kuwasimanga au kuwatendea uovu wowote mayatima na wenye shida ni katika makosa makubwa.
3.Swala ni lazima itekelezwe kwa kuzingatia ipasavyo nguzo, sharti zake pamoja na khushui (unyenyekevu).
4.Kutenda jambo lolote kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu (s.w) ndio uhai wa ibada ya muumini.
5.Maisha ni jambo la kijamii ambalo linahitajia watu kuishi pamoja kwa kusaidiana inapobidi.
6.Muumini wa kweli ni yule aliyemwepesi kutoa misaada kwa wanaadamu wenzie na mwenye kujali matatizo ya wengine yanapowapata.Suratul - Qureish (106): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Nne.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1.Ili kuwafanya Maqureish waendelee.
2.Waendelee na safari zao za wakati wa kusi (kwenda Yemen) na wakati wa kaskazi (kwenda Sham ndiyo maana tukajaalia jeshi la ndovu kushindwa).
3.Basi na wa muabudu Bwana wa Nyumba hii (Al-Kaaba).
4.Ambaye amewalisha (wakati wa) katika njaa na anawapa amani (wakati wa) katika khofu.Mafunzo kwa Ufupi.
1.Kwa hakika anayelisha na kulinda ni Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake.
2.Amani, Usalama na Ustawi wa kweli wa jamii hutokana na kushikamana na amri za Mwenyezi Mungu (s.w).
3.Shukrani za kweli kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni kumuabudu ipasavyo.
4.Maingiliano ya Mataifa kibiashara ni katika neema za Mwenyezi Mungu (s.w).                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 772


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Je Qur-an ilikusanywa na kuandikwa katika msahafu wakati wa uongozi wa Abu-Bakr(r.a)
Je Qur-an ilikusanywa na kuandikwa katika msahafu wakati wa uongozi wa Abu-Bakr(r. Soma Zaidi...

Hoja juu ya kukubalika hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sababu za kushuka sural Masad (tabat haraka)
Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al bayyinah
Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane. Soma Zaidi...

Saratul-humaza
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al qadir
Asbab nuzul surat al qadi. Hii ni sura ya 97 katika mpangilio wa mashaf. Surat al qadir imeteremshwa Madina na ina aya 5. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat al qariah
Surat Al qariah, ni moja katika sura zilizochuka miaka ya mwanzoni mwa utume. Soma Zaidi...

Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia
Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya id-gham katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake. Soma Zaidi...

quran na sayansi
2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio. Soma Zaidi...