image

Kulaaniwa Bani Israil

Pamoja na kuteuliwa na Allah(s.

Kulaaniwa Bani Israil

Kulaaniwa Bani Israil


Pamoja na kuteuliwa na Allah(s.w) kuwa taifa bora kuliko mataifa yote ya wakati huo, Allah(s.w) aliwaghadhibikia Mayahudi na kuwalaani kutokana na matendo yao yafuatayo:

(i)Walikuwa ni wezi wa fadhila

- Allah(s.w) aliwatunukia neema mbali mbali ili wasimamishe
Ufalme wake katika ardhi na wamuabudu ipasavyo.

- Wengi wao walivitumia vipawa hivi kwa maslahi ya dunia na wakawa miongoni mwa wenye kuzama katika maasi.

- Baadhi ya neema walizotunukiwa Mayahudi zimeainishwa katika Qur-an - Rejea (2:47-53, 60, 122),(45:16-17).



(ii) Walipewa maonyo na mazingatio ili waache makosa na watengenee, lakini hawakuonyeka wala kuzingatia bali walikaidi na kuendelea kuzama katika kumuasi Allah(s.w). Rejea Qur-an (2:54-59, 61, 63-74), (5:71), (7:138-141).



(iii)Waliwakadhibisha na kuwaua Mitume wa Allah(s.w) bila ya haki.

"Kwa yakini Tulichukuwa ahadi ya wana wa Israili (Mayahudi kuwa watafuata), na Tukawapelekea Mitume. (Lakini) kila mara alipowafikia Mtume kwa yale zisiyoyapenda nafsi zao, wengine (katika Mitume hao) waliwakadhibisha, na wengine wakawaua (khasa)" (5:70).



(iv) Walivunja ahadi mbali mbali walizowekeana na Allah(s.w).
- Rejea Qur-an (2:83-86, 93, 100), (5:12-13, 70).



(v) Walikuwa na kibri na majivuno kuwa wao ni vipenzi vya Allah (s.w) na kwamba wataingia Peponi bila ya kufanya amali stahiki. Na ikitokea waingie Motoni watakaa muda mchache tu bila ya kujali uovu wanaoufanya:


"Na walisema: Hautatugusa Moto (wa Jahannamu) isipokuwa kwa siku chache tu. Sema: Je! mmepata ahadi kwa Mwenyezi Mungu kwa hivyo hatakhalifu ahadi yake? Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua? (2:80).

- Pia rejea Qur-an (2:88, 91).



(vi) Wanazuoni wao walikuwa wakificha haki. Pia walikuwa wakichanganya haki na batili.

Mnatumaini (nyinyi Waislamu) ya kwamba watakuaminini (hao Mayahudi); na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wanayabadili baada ya kuwa wameyafahamu; na hali wanajua? (2:75)

Wala msichanganye haki na batili, na mkaficha haki, na hali mnajua. (2:42)

- Pia rejea Qur-an (2:76-79).



(vii) Walibadili vitabu vya Allah(s.w) kwa kupunguza au kuongeza au kuondoa maneno au aya ili kuvuruga maana halisi ya kile kilichokusudiwa kwa maslahi yao binafsi kwa ajili ya dunia.



(viii) Walikuwa wakiwaamrisha watu kutenda mema ambayo wenyewe walikuwa hawafanyi.

Je! Mnawaamrisha watu kutenda mema na mnajisahau nafsi zenu, hali mnasoma kitabu (cha Mwenyezi Mungu kuwa kufanya hivyo ni vibaya)? Basi je, hamfahamu? (2:44)



(ix) Walikuwa wakitekeleza baadhi ya maamrisho ya Allah(s.w) na kukufuru baadhi. Yaani walikuwa wakifuata baadhi ya kitabu na kukufuru baadhi nyingine - Rejea Qur-an (2:85)



(x) Walikuwa wakila riba na kula mali za watu kwa batili - Qur-an (4:161).



(xi) Walikuwa hawaamrishi mema na kukataza mabaya - Qur-an (5:78-79)


(xii) Walikuwa wakifanya urafiki na makafiri - Qur-an (5:80). (xiii) Walipenda sana kuishi na walikuwa wakiogopa sana kufa kutokana na yale maovu iliyotanguliza mikono yao - Qur-an (2:96), (62:6-8).



(xiv) Waligawanyika katika makundi makundi mbali mbali, kila kundi likiwa dhidi ya lingine japo wote wanasoma kitabu kimoja. Qur'an inawaonya Waislamu juu ya hili katika aya zifuatazo:

Hakika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna ukhusiano nao wowote. Bila shaka shauri yao (ya kuwaadhibu) iko kwa Mwenyezi Mungu; kisha (hapo wakati wa kuwaadhibu) atawaambia yale waliyokuwa wakitenda (6:159).

"Nyenyekeeni Kwake na mcheni, na simamisheni Sala, wala msiwe katika washirikina"
"Katika wale walioitenga Dini yao na wakawa makundi makundi; kila kikundi kinafurahia kilicho nacho" (30:31-32).



(xv) Waliofanya Viongozi wao Miungu Juu ya hili Qur'an inatufahamisha katika aya zifuatazo:


"Na Mayahudi wanasema: "Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;" na Wakristo wanasema: "Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu;: haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale walio kufuru kabla yao,Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!" (9:30).


"Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu na (wamemfanya) Masihi mwana wa Maryamu (pia Mungu), hali hawakuamrishwa isipokuwa kumuabudu Mungu Mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Yeye. Ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo" (9:31).



(xvi) Walijenga hoja za visingizio.

Mayahudi walikatazwa kufanya kazi Jumamosi. Lakini baadhi yao waliasi ima kwa ujanjaujanja au kwa wazi wazi. Miongoni mwa waliokhalifu kwa unjanja ujanja ni wavuvi wa samaki. Walikuwa wakitega mitego yao Ijumaa jioni na kuchukua samaki Jumamosi jioni au Jumapili asubuhi ili ionekane kuwa Jumamosi hawakufanya kazi. Na wengine waliasi kwa kuleta visingizio kadhaa. Allah(s.w) aliye mjuzi wa nia zao aliwajua kuwa waliamua kumuasi na akawalipa adhabu ya kudhalilisha:

"Na kwa yakini mmekwisha kujua (khabari za) wale walioasi miongoni mwenu katika (amri ya kuihishimu) Jumamosi. Basi Tukawaambia: "Kuweni manyani wadhalilifu" (2:65).



                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 813


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Kwa nini quran ilishuka kidogo kidogo?
Kuna sababu nyingi za kuonyesha umuhimu wa Quran kushuka kwa mfumo wa kidogo kidogo Soma Zaidi...

Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w)
(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat Ikhlas
Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani? Soma Zaidi...

Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili Kuwania Madaraka na Ukubwa
(x) Dai kuwa Muhammad (s. Soma Zaidi...

Quran Tafsiri kwa Kiswahili
Tafsiri ya quran kw akiswahili, imeandikw ana Shekh Ali Muhsin al-Barwani Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki katika quran
Soma Zaidi...

Qur-an Kushuka Kidogo Kidogo kwa Kipindi cha Miaka 23:
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MADD
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MADD YAANI KUVUTA HERUFI KWENYE USOMAJI WA QURAN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...