- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na
ubinaadamu wao.
- Watumwa walimilikiwa kwa kuuzwa na kununuliwa kama bidhaa za biashara
au kwa matumizi mengineyo pia.
- Watumwa walikuwa wakitumika kama sehemu ya starehe na kiburudisho kwa
wakubwa zao.
- Mateso, unyama na ukatili ilikuwa desturi ya kufanyiwa watumwa na mabwana
zao katika kutimiza matashi yao.
- Watumwa walikuwa hawana uhuru wa kufanya na kufuata mila, desturi au dini
waitakayo na waipendayo wao wenyewe bila ruhusa ya wakubwa wao.
- Watumwa walikuwa wakitumikishwa kama wanyama au hata zaidi ya wanyama
kwa kufanyishwa kazi ngumu zilizozidi uwezo wao.
- Kila jaribio la ubaya lilifanywa kupitia watumwa, mfano makali ya kisu, mkuki,
mshale, n.k yalijaribiwa kwa watumwa.
- Watumwa ndio ilikuwa nyenzo pekee ya kufanyia kazi, kubebea na kusafirishia
mizigo mikubwa kwa masafa ya mbali.
- Hadhi na nafasi kati ya mabwa na watumwa ilikuwa na utofauti mkubwa mno,
kiasi kwamba bwana anaweza kumdhalilisha mtumwa kwa namna apendavyo.
- Huduma na misaada ya kiutu kwa watumwa ilikuwa hafifu mno, kiasi kwamba
mtumwa akiugua au kukosa uwezo wa kuzalisha mali alikuwa hana faida tena
kwa bwana.