Menu



Quran si maneno ya shetani

Quran si maneno ya shetani

(v) Dai kuwa Qur-an ni aya za Shetani



Katika mwaka 1988 Salman Rushdie, Muingereza mwenye asili ya kihindi, aliandika kitabu chake alichokiita "Satanic Verses" (yaani aya za Shetani) ambamo amemtukana Mtume (s.a.w), Uislamu na Qur-an kwa kuiita "aya za Shetani."



Katika kitabu chake hicho, Rushdie amedai kuwa hapakuwa na wahy wowote uliomshukia Muhammad (s.a.w) bali alikuwa akidai tu kuwa anashushiwa Wahy. Aidha Rushdie anadai kuwa Muhammad (s.a.w) alikuwa ni mtu aliyekuwa akifuata matashi yake mwenyewe akiongozwa na shetani na kwa hiyo yote yaliyomo ndani ya Qur-an ni maneno ya shetani.



Pia Rushdie katika kitabu chake hicho amedai kuwa Mtume (s.a.w) hakuwa na uwezo wa kutofautisha wahy kutoka kwa Malaika au wahy kutoka kwa shetani.

Vile vile Salman Rushdie amedai kuwa Mtume (s.a.w) hakuwa na kumbukumbu ya kile alichowasomea waandishi wake na wala hakuweza kutambua hata kile ambacho waandishi hao wamekiongeza kichini-chini. Amepiga mfano wa mwandishi mmoja wa Kifursi kuwa alisomewa na Mtume aandike "Mwenye kusikia, mwenye kujua kila kitu" lakini yeye akaandika "Mwenye kujua na Mwenye hikma" na Mtume hakung'amua mabadiliko hayo!



Udhaifu wa madai ya Salman Rushdie
Kwanza,
ujumbe wa Qur-an umeteremshwa ili kumtoa binaadamu kutokana na hadaa zote za shetani. Shetani katika Qur-an ameelezwa wazi pamoja na vitimbi vyake na watu anaowatumia ili wanaadamu wasiweze kupotezwa naye. Hebu turejee aya chache zifuatazo:


"Na namna hii tumemfanyia kila Nabii maadui, (nao ni) mashetani katika watu na (mashetani) katika majini. Baadhi yao wanawafunulia wenzao maneno ya kupamba pamba ili kuwadanganya. Na Mola wako angelipenda wasingelifanya hayo. Basi waache na uongo wao." (6:112)


"Enyi wanaadamu! Shetani (Iblisi) asikutieni katika matata, kama alivyowatoa wazee wenu katika Pepo akawavua nguo zao ili kuwaonesha tupu zao. Hakika yeye pamoja na kabila yake wanakuoneni na hali ya kuwa hamuwaoni." Bila shaka sisi tumewajaalia mashetani kuwa marafiki wa wale wasioamini." (7:2 7)



"Kwa yakini Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni adui (yenu; kwa hivyo msimtii) kwani anaita (analiita) kundi lake liwe katika watu wa Motoni." (35:6)
Kama Qur-an ni maneno ya Shetani, inakuwaje tena shetani mwenyewe ajidhihirishe kiasi hicho ili watu wamkimbie?



Pili, Allah (s.w) anasema kuwa laiti ingelikuwa hii Qur-an inatoka kwa mwingine asiye kuwa Yeye au kama ingekuwa ina waandishi wawili tofauti ambao wana malengo yanayopingana mmoja anavutia kwenye mema na mwingine kwenye uovu pangelikuwa na khitilafu nyingi (Qur-an 4:82). Je, uko mgongano wowote katika maneno ya Qur-an? Haupo, bali maneno yote ya Qur-an ni yenye kusadikishana. Hivyo haiwezekani Qur-an kuwa na mchanganyiko wa maneno ya shetani na ya Allah (s.w) kwa pamoja.



Tatu, Qur-an yenyewe imekataa kuwa Qur-an si maneno ya shetani."Wala hii si kauli ya shetani aliyefukuzwa (katika rehma za Mwenyezi Mungu.) (81:25)



Nne, Sote tunamfahamu shetani kuwa ni kiumbe dhaifu pamoja na kuwa hatumuoni. Sasa ikiwa shetani ameleta maneno na ujumbe mzito uliomo ndani ya Qur-an, kwanini na mashetani wengine nao hawakai pamoja kujibu zile changamoto zilizotolewa? "Mahound" kama alivyomwita Rushdie ni shetani mmoja tu, je pamekuwa na uzito gani kwa wanaadamu pamoja na majini wakichanganyika kuleta mfano wa angalau sura moja ya Qur-an? Qur-an imetoa changamoto hiyo tangu kuanza kushuka kwake:


"Sema "Hata wakijikusanya watu (wote) na majini kuleta mfano wa hii Qur-an basi hawangaliweza kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao." (17:88)




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views 1148

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Amri ya Kuchinja Ng'ombe

Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr.

Soma Zaidi...
Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w)

(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.

Soma Zaidi...
Aina saba za Viraa vya usomaji wa Quran

Post hii inakwenda kukuorodheshea aina saba za viraka vya usomaji wa Quran.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat at Takaathur

Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi

Soma Zaidi...
quran na sayansi

YALIYOMONENO LA AWALI1.

Soma Zaidi...
Aina za Madd far-iy

Mada zipo katika makundi mawili ambayo ni madda far-iy na mdada twab-iy.

Soma Zaidi...