Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti

2.

Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti

Kuandaa sanda na kumvalisha maiti wa kiume na kike

2. Kumkafini (Kumvisha Sanda) Maiti.
Mazingatio juu ya Sanda.
- Ni sunnah kutumia nguo nyeupe.
โ€˜Ibn Abbas amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema:
โ€œVaeni nguo nyeupe, kwa sababu hili ni vazi lenu lililo bora kuliko yote, na wakafinini maiti wenu kwa nguo (nyeupe)โ€
(Abu Daud, Tirmidh na Ibn Majah)



- Pia sanda isiwe nguo ya gharama.
โ€˜Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema:
โ€œMsigharamie sana nguo za sanda, kwani inakwenda kuozeana (kaburini)โ€
(Abu Daud)



- Hajji akifa akiwa katika vazi la Ihram (Hija), vazi hilo ndio litakuwa sanda yake.
โ€˜Abdullah bin Abbas amesimulia kuwa mtu mmoja alikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) ngamia wake alimkanyaga, wakati akiwa anahiji mpaka akafa, Mtume wa Allah akasema:
โ€œMuosheni na maji na majani ya mkunazi na mumkafini kwa hayo mashuka yake mawili, msimpake manukato na msimfunike kichwa chake โ€ฆโ€ฆ.โ€
(Bukhari na Muslim )



- Ukubwa wa sanda unategemeana na ukubwa wa maiti.



Sanda ya Mwanamume na namna ya kumkafini (kumvika).
- Sanda ya mwanamume ina vipande (majavi) vitatu.

1. Utaratibu wa kutayarisha sanda ya mwanamume.
i.Weka kipande cha kwanza juu ya mkeka kisha cha pili na cha tatu na vyote kushikizwa kwa uzi katikati, na kila kipande kipakwe marashi na ubani.



ii.Pasua kamba katika pembe mbili za jamvi la kwanza, moja kwa ajili ya kufungia kichwani na nyingine kwa ajili ya kufungia miguuni.
Kamba moja itachanwa kutoka jamvi la pili, ili kumfunika (kufungia) maiti katikati. Na kamba tatu zitachanwa jamvi la tatu na la pili kwa ajili ya kufungia juu ya mkeka.



iii.Maiti italazwa juu ya majavi yote matatu. Ichukuliwe pamba iwekwe manukato kisha iwekwe juu ya viungo vyote vya sijda; paji la uso, viganja vya mikono, magotini na vidole vya miguu. Pamba itumike pia kuziba tundu zote mwilini; mdomo, masikio, pua na makalio.



iv.Maiti itatizwe (ifunikwe) mwili wote, kwa kuanza kipande cha kwanza, kisha cha pili na cha tatu ukitanguliza kunjo la kushoto kisha la kulia linafuata. Zile kamba zilizochanwa zitatumika kufungia vitanzi maiti kichwani, tumboni na miguuni. Baada ya hapo maiti inaweza kuwekwa kwenye jeneza baada ya kuzungushiwa kwa mkeka tayari kwa kuswaliwa.



Sanda ya mwanamke na namna ya kumvika.
- Sanda ya mwanamke ina vipande vitano;
1. Majamvi 2
2. Shuka (Gagulo) au Underskirt 1
3. Kanzu (Blause) 1
4. Shungi (Ukaya) 1.



- Taratibu za kutayarisha sanda na kukafini:
i.Majamvi mawili yatatandikwa moja baada ya nyingine.
ii.Kikatwe kitambaa cha ukubwa wa shuka ya kujifunga kiunoni (shuka/gagulo) na iwekwe juu ya majamvi mawili ili ije kutumika kumfungia kiunoni.



iii.Kisha ikatwe kanzu (blause) isiyoshonwa vizuri kwa kukunja kitambaa na kukitoboa katikati kwa ajili ya kuingizia kichwa cha maiti (kumvalisha) na kisha kushikiza pembeni kwa uzi mfano wa kanzu kata mikono na kuwekwa juu ya gagulo sehemu ya chini (kiunoni) na itakuwa juu ya majamvi 2 sehemu ya juu (kifuani).



iv. Kitambaa (ukaya/shungi) ya kutosha kuweza kufunika kichwa na uso kitaingizwa ndani ya shingo ya kanzu na kunyooshwa kwa juu.



v.Maiti itaanza kuvalishwa kanzu, kisha kufungwa shuka (gagulo) juu yake. Kisha maiti itawekewa pamba viungo vyote vya sijda na kuziba sehemu za matundu kama ilivyokuwa kuwa kwa maiti mwanamume. Kisha maiti itatizwa (itafungwa) na majamvi mawili, moja baada ya jingine kwa kuanza kunjo la kushoto na kumalizia la kulia juu yake, na kisha kufungwa na kamba tatu juu yake- kichwani, tumboni na miguuni na kuwa tayari kuingizwa kwenye jeneza na kuswaliwa.


Sanda ya mtoto.
- Sanda ya mtoto mdogo, wa kike au kiume wasiofikia baleghe ni majamvi matatu, kama ilivyo sanda ya mwanamume.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 4833

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 web hosting    ๐Ÿ‘‰2 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰3 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    ๐Ÿ‘‰6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu

Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?

Soma Zaidi...
TOFAUTI KATI YA MAKATOZO NA MAAMRISHO KATIKA SUNNAH

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ู‡ูุฑูŽูŠู’ุฑูŽุฉูŽ ุนูŽุจู’ุฏู ุงู„ุฑูŽู‘ุญู’ู…ูŽู†ู ุจู’ู†ู ุตูŽุฎู’ุฑู ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ู‚ูŽุงู„ูŽ: ุณูŽู…ูุนู’ุช ุฑูŽุณููˆู„ูŽ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ูŠูŽู‚ููˆู„ู: "ู…...

Soma Zaidi...
Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?

Soma Zaidi...
Haki za raia katika dola ya kiislamu

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuswali swala ya kuoatwa kwa juwa ama swala ya kuoatwa kwa mwezi.

Post hii itakufundisha kuhusu swala ya kupatwa yaani kupatwa kwa juwa na kupatwa kwa mwezi swalat kusuf na swalat khusuf

Soma Zaidi...
Nafasi ya serikali katika ugawaji

Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi.

Soma Zaidi...
maana ya Eda na aina zake

Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.

Soma Zaidi...
Sunnah za udhu

Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu sunah za udhu

Soma Zaidi...