Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Namna lengo la zakat linavyofikiwa.
Zakat na sadaka zinalengo la kutakasa mali na nafsi ya mtoaji na mpokeaji kama ifuatavyo;
Zakat na sadaka inavyotakasa mali ya mtoaji.
Zakat hutolewa 2.5% ya mali na kuwapa wanaostahiki, hivyo kuitakasa mali ya mtoaji kutokana na chumo la haramu na haki za watu.
Zakat na sadaka zinavyotakasa nafsi ya mtoaji.
Utoaji mali kwa wanaostahiki huitakasa nafsi ya mtoaji kutokana na ubakhili, kuabudu mali, kibri, n.k katika kumiliki mali na kuwa na upole, huruma, n.k.
Rejea Quran (61:10-12) na (9:102-103).
Zakat na sadaka inavyotakasa nafsi ya mpokeaji.
Utoaji wa zaka na sadaka kwa wanaostahiki huondoa chuki, husuda, uadui, unyonge kwa wasionacho na kuleta udugu, upendo, shukurani na ushirikiano.
Rejea Quran (9:60).
Zakat na sadakat huitakasa jamii ya waislamu.
Utoaji wa zakat na sadaka hujenga jamii yenye udugu wa kweli, kujenga uchumi wa halali na kuondoa chuki na uadui baina ya masikini na matajiri.
Rejea Quran (61:4).
Umeionaje Makala hii.. ?
Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?
Soma Zaidi...Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla.
Soma Zaidi...Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha taratibu za kuajiri, kufanya kazi na malipo.
Soma Zaidi...Huwezi kuruhusiwa kumrejea mke endapo utamuacha kwa talaka hizi mbili.
Soma Zaidi...