1.
1.Kuoshwa (Kukoshwa).
Mazingatio kabla ya kuosha maiti.
(a)Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake pia.
- Maiti ya mtoto yaweza kuoshwa na yeyote.
- Ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia
(b)Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa ajili ya kumpa msaada inapobidi.
(c)Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti muislamu kama vile;
1. Muoshaji awe muislamu.
2. Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
3. Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
4. Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa โglovesโ.
5. Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi, pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.
(d)Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:
1. Nia
2. Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi kwa idadi ya witiri.
Namna ya Kuosha Maiti hatua kwa hatua.
i.Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
ii.Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu unaotoka kwa maiti.
- Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye karo liliotengenezwa
kwa kazi hiyo.
iii.Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji wakati wa kuosha.
iv.Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo (ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.
v.Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.
vi.Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama ilivyo mara ya kwanza.
vii.Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi.
- Kama hapaja takata, basi na avae gloves safi na ile chafu aitupe kwenye
ufuo na asafishe tena kama mara ya kwanza mpaka patakate.
viii.Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha akitupe ufuoni.
ix.Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
x.Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.
xi.Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu za kawaida za kutia udhu (kutawadha).
xii.Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa ameinamishwa mbele kidogo.
- Kama nywele au ndevu ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na
maji mpaka zitakate.
- Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizongโoka
ziambatanishwe na sanda.
xiii.Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni na maji safi mpaka itakate.
xiv.Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyooshwa wa kulia.
xv.Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.
xvi.Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu baada ya kufa.
xvii.Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari kuvalishwa sanda (kukafiniwa).
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inakwenda kukufundisha ni kwa nini dua ya kafiri inawwza kujibiwa wakati ya muumini haijibiwi.
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua
Soma Zaidi...Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila.
Soma Zaidi..."Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu, kama mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za ndugu zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za s
Soma Zaidi...Hii ni historia ya Imamu Bukhary pamoja na kitabu chake cha sahihul Bukhari.
Soma Zaidi...