Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata ujauzito
SIKU YA KUPATA UJAUZITO
Swala la kupata ujauzito limekuwa likikabiliwa na imani nyingia ambazo sio sahihi. Watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha kujaribu kutatua maswali yao. Leo nitakusaidia kutatua swali hili Je..! ni zipi dalili za mimba changa. Swali hili ni la msingi kwani kuna watu wengi wamekuwa wakichanganya dalili za ujauzito na shida nyingine za kiafya. Hapa nitajaribu kukufahamisha utofauti wa dalili hizi na nyingine ili upate kufahamu vyema.
Imani potofu kuhusu dalili za ujauzito:-1.Mimba inaingia siku yeyote ile. Hii sio sahihi kabisa mimba inasiku maalumu ambazo huweza kutungwa. Kitaalamu siku hizi zinafahamika kama fertile window2.Siku yya 14 ndio siku ambayo mimba hingia. Hii pia sio sahihi, kwani wanawake sio wote wanaingia siku 28, kuna wengine ni kati ya 21 mpaka 353.Unaweza kupima mimba kwa ktumia sukari, chumvi, mafuta, sabuni, delto. Hizi zote sio sahihi kabisa.
Ni siku gani mimba huingia.Mimba huweza kuingia siku ambayo yai litakutana na mbegu ya kiume kwenye mirija ya falopia kwenye tumbo la uzazi la mama. Yai la mwanamke kuzalishwa kwenye ovari. Mwanamke ana ovari mbili, moja upande wa kulia na nyingine kushoto. Hizi mbili hupeana zamu ya kutoa mayai. Yaani kama mwezi huu limetoa hili na nyingine itatoa mwezi ujao.
Tafiti zinaonyesha kuwa yai huweza kuanza kukomaa kuanzia siku ya 10 toka kupata hedhi mpaka siku ya 14. hii ni kwa wanawake wengi. Ila si wote. Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--
1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.
2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20.
4.Mwanamke mwenye siku 28: 28-12 = 16 kisha toa siku 4 nyuma 16 - 4 = 12. hivyo siiku ambazo yai hukomaa kwa mwenye siku 28 ni kati ya 12 mpaka 16.
Sasa baada ya kuzijua siku hizi ambazo yai hukomaa, inabidi ufahamu kuwa yai la mwanamke huweza kuishi kati ya masaa 12 mpaka 24 toka kukomaa (ovulation). kwa upande mwingine mbegu za kiume huisho kati ya siku 3 mpaka 5. hivyo ujauzito unaweza kutungwa kwa mbegu ambayo ilikuwepo toka siku tatu zilizopita.
NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.
Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-
1.Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.
2.Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.
3.Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.
Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za mfuko wa kizazi kushindwa kisinyaa, ni sababu ambazo utokea kwa akina Mama wengi kadri ya wataalamu wametafuta asilimia kuwa asilimia sabini ya wanawake mifuko yao ya kizazi kushindwa kisinyaa.
Soma Zaidi...Kupata Ukimwi ama HIV hufungamana na mambo mengi. Si kila anayefanya ngono zembe nabmuathiria naye lazima aathirike. Hiivsibkweli, ila tangu kuwa hali hii ni hatari kwani kupata maambukizi ni rahisi sana.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kujaa tmgesi tumbon
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango.
Soma Zaidi...Utajifunza sababua zinazopelekea kuhisi maumivu makali ya tumbo baada ya kumaliza tendo la ndoa
Soma Zaidi...Nina swali langu:-je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi fibroids au uvimbe kwenye via vya uzazi hasa hasa utokea kwenye tumbo la uzazi ambapo kwa kitaalamu huitwa uterusi, uvimbe huu ulitokea watu wengine huwa hawawezi kutambua Dalili zake mapema kwa hiyo leo tunapaswa kujua Dalili zake
Soma Zaidi...