Bawasili usababishwa na nini?
Posti hii inahusu zaidi visababishi vya ugonjwa wa Bawasili,kuna watu wengi wanapenda kujua kabisa chanzo cha kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii na kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu visababishi vya Bawasili.
Visababishi vya ugonjwa wa Bawasili.
1. Kufunga choo au kukosa choo kwa mda mrefu.
Hii ni sababu ya kwanza kabisa kwa sababu kuna watu ambao hawapati choo au wanabana choo kwa mda mrefu na usababisha kuwepo kwa Bawasili.
2. Wakati wa ujauzito.
Wakati wa ujauzito kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Bawasili kwa sababu ya kuwepo kwa mgandamizo wa mtoto kupelekea kwenye na sehemu ya haja kubwa , na pia wakati wa kujifungua mtoto anakandamiza sana sehemu ya haja kubwa.
3. Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
Kuna kipindi watu wanapenda kufanya mapenzi kwenye sehemu ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa Bawasili.
4. Uzee.
Pia nao wana uwezekano wa kupata tatizo hili la Bawasili kwa sababu mtu akiweka na kinga za mwili zinashuka hali ambayo Usababisha kupata ugonjwa huu.
5. Pia kuna sababu za kurithi.
Kwa kawaida kuna familia ambayo upata ugonjwa huu mara kwa mara kutoka kwa babu , baba na majukumu kwa hiyo kuna uwezekano wa kupata kama ugonjwa umo kwenye familia.
6. Kuharisha sana na kwa mda mrefu.
Kuna watu ambao wanapatwa na tatizo la kuharisha sana na kwa mda mrefu nao wana uwezekano wa kupata ugonjwa huu wa Bawasili.
7. Matumizi ya vyoo vya kukalia.
Kuna uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu kwa sababu ya matumizi ya vyoo vya kukalia kwa mda mrefu ingawa sio wote wanaotumia vyoo hivi kupata Bawasili.
8. Kunyanyua vitu vizito.
Kuna wakati mwingine watu wenye tabia ya kunyanyua vitu vizito wamo hatarini kupata ugonjwa huu wa Bawasili.
9. Kuwepo kwa mfadhaiko au stress.
Kwa kuwepo kwa mfadhaiko wa mara kwa mara usababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo na Bawasili.
10. Kuwepo kwa uzito mkubwa na unene wa kupitiliza, kwa kawaida watu wanene na wenye uzito uliopitiliza usababisha kuwepo kwa magonjwa mbalimbali na wako hatarini kupata Bawasili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π2 Dua za Mitume na Manabii π3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π4 ai web app π5 Madrasa kiganjani π6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Dalili za Mimba Baada ya Ovulation
Kipindi cha baada ya yai kupevuka (ovulation) na kabla ya siku zako za hedhi kutarajiwa (drip-wait period) ni kipindi cha kusisimua kwa mwanamke anayetafuta mtoto. Makala hii inaelezea dalili za mapema ambazo mwili unaweza kuzionyesha mara baada ya yai kurutubishwa na kupandikizwa kwenye mji wa mimba, yakikusaidia kuelewa mabadiliko ya kibaolojia yanayoendelea.
Soma Zaidi...Ishara na dalili za saratani ya mdomo.
Posti hii inaonyesha dalili na mabo ya hatari kwenye ugonjwa wa saratani ya mdomon.Saratani ya mdomo inarejelea Kansa inayotokea katika sehemu zozote zinazounda mdomo. Saratani ya mdomo inaweza kutokea kwa: Midomo, Fizi, Lugha, Nd
Soma Zaidi...Dalili za VVU/UKIMWI Ni zipi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za VVU/ UKIMWI
Soma Zaidi...Matatizo ya kisaikolojia baada ya kujifungua (Postpartum Depression).
Kipindi cha baada ya kujifungua ni wakati wa mabadiliko makubwa ya kimwili na kihisia. Makala haya yanalenga kuelimisha kuhusu Postpartum Depression (PPD)βhali ya huzuni kali na msongo inayowapata akina mama wengi. Tutachambua dalili, sababu, na njia muhimu za kutafuta msaada ili kuhakikisha afya ya akili ya mama na ustawi wa mtoto.
Soma Zaidi...Kazi ya Ini: Jinsi ya kulilinda dhidi ya sumu.
Ini ni kiungo kikubwa zaidi cha ndani mwilini na kinafanya kazi kama "kiwanda cha kusafisha sumu" cha mwili wako. Kazi yake ni muhimu sana kwa uhai, kuanzia kuchuja damu hadi kuyeyusha chakula. Hata hivyo, kutokana na mtindo wa maisha wa kisasa, ini linaweza kulemewa na sumu, jambo linalopelekea maradhi kama ini la mafuta (fatty liver) au uvimbe wa ini (hepatitis). Makala haya yanachambua kazi kuu za ini na mbinu madhubuti za kulilinda dhidi ya uharibifu.
Soma Zaidi...Madhara ya ugonjwa wa madonda ya koo usipotibiwa
Posti hii inahusu zaidi madhara ya ugonjwa wa madonda ya koo usipotibiwa, ugonjwa huu usipotibiwa unaweza sababisha madhara mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...