Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii, hizi ni njia za awali za kupambana na kuwepo kwa Ugonjwa wa Bawasili.
1. Njia ya kwanza ni kuhakikisha kuwa ukipata haja kubwa fanya haraka kuitoa na usisubiri mda na pia kama kuna tatizo la choo kuwa ngumu ni vizuri kutafuta matibabu ili kuweza kuepuka madhara ya uwepo wa Bawasili.
2. Kuachana na tabia ya kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
Hii ni tabia ambayo imeingia na inatumiwa na watu wengi sana hasa kwa vijana hali inayopelekea kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili na pia kuwepo kwa Maambukizi mbalimbali kwa sababu ya kulegea kwa mishipa ya haja kubwa hali inayosababisha kuwepo kwa Bawasili.
3. Kutibu magonjwa ya kuharisha endapo yametokea.
Kwa kawaida kuharisha kwa mda mrefu usababisha kuwepo kwa Ugonjwa wa Bawasili kwa kufanya hivyo tutaweza kuepuka kuwepo kwa Ugonjwa huu.
4. Kupunguza matumizi ya vyoo vya kukalia.
Kwa wale wanaotumia sana vyoo vya kukalia wanapaswa kupunguza au kutumia njia nyingine ili kuepuka kuwepo kwa Ugonjwa wa Bawasili.
5. Kupunguza tabia ya kunyanyua vitu vizito.
Kwa wale ambao kazi zao mara nyingi ni kunyanyua vitu vizito wanapaswa kupunguza ili kuepuka matatizo ya gonjwa la Bawasili.
6. Kupunguza uzito na unene wa kupitiliza.
Kwa kawaida watu wanene na wenye uzito wa kupitiliza wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.
7. Kuachana na msongo wa mawazo.
Kuna watu ambao wanaweza kila siku kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo kwenye maisha yao kwa hiyo tunapaswa kuwakwaza na kutafuta kitu chochote cha kuwafanya waachane na kukaa kwenye mawazo mda wote.
8. Kutoa elimu kwa watu kuhusu Ugonjwa huu. Maana yake, jinsi unavotokea, madhara yake na njia za kufanya ili kuweza kutokomeza kabisa ugonjwa huu kwenye jamii.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inaelezea kuhusiana na sababu zinazosababisha kinjwa au mdomo kutoa harufu mbaya?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo unapaswa kufanya kama una tatizo la kiungulia.
Soma Zaidi...HOMA YA MANJANO (yellow fever)Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na mambo hatari yanayosababisha ugonjwa wa moyo.
Soma Zaidi...VYNZO VYA MINYOO Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao.
Soma Zaidi...Saratani inahusu ugonjwa wowote kati ya idadi kubwa ya magonjwa ambayo yanaonyeshwa na ukuaji wa seli zisizo za kawaida ambazo hugawanyika bila kudhibitiwa na kuwa na uwezo wa kupenya na kuharibu tishu za kawaida za mwili. Saratani mara nyingi ina uwezo
Soma Zaidi...SABABU ZA KUTOKEA KWA VIDONDA VYA TUMBO Sababu za kawaida za vidonda vya tumbo ni maambukizo na bakteria Helicobacter pylori (H.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha matatizo yanayosababisha saratani ya mapafu .
Soma Zaidi...ugonjwa wa kisukari ni moja katika magonjwa hatari sana, na mpaka sasa bado hauna matibabu ya kuponya moja kwa moja
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya watu walio hatarini kupata fangasi
Soma Zaidi...