Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Bawasili

Posti hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa Bawasili, ni ugonjwa unaotokea kwenye njia ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa uvimbe au nyama ambazo uonekana hadi nje, kwa lugha ya kitaalamu ujulikana kama haemorrhoid au pokea.

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Bawasili.

1. Pamoja na kuwepo kwa Ugonjwa huu kuna aina mbili za Ugonjwa wa Bawasili kuna Bawasili ya nje ambayo uonekana kwa nje na kuna Bawasili ya ndani ambayo uonekana kwa ndani kwa hiyo tutaziona moja baada ya nyingine.

 

2. Bawasili ya nje. 

Aina hii ya Bawasili utokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa  na kuambatana na maumivu makali kwa mgonjwa na pia utokea miwasho wa ngozi katika sehemu hiyo  mara nyingi katika sehemu hiyo mishipa ya damu yaani veini upasuka  na damu kuganda  hivyo kusababisha aina hii ya Bawasili ambapo kwa kitaalamu huitwa thrombosed haemorrhoid.

 

3. Pia aina ya pili ya Bawasili ni Bawasili ya ndani.

Aina hizi ya Bawasili ni tofauti na ya kwanza hii kwa kawaida utokea ndani ya mfereji wa haja kubwa pia nayo uambatana na Maumivu ambayo Usababisha Mgonjwa kuumia sana na pengine miwasho inaweza kutokea kwa nje .

 

4. Baada ya kuona aina kuu mbili za Bawasili yaani Bawasili ya ndani na nje na matokeo yake ni hali ya kuwepo kwa maumivu makali yanayoambatana na miwasho, kwa hiyo ni vizuri kabisa kutafuta matibabu ili kuweza kuondokana na tatizo hili kwa sababu watu walio wengi wanapuuza kuwepo kwa dawa hospitalini wanakimbilia dawa mbadala ambazo kwa wakati mwingine zinaweza kusababisha madhara zaidi kuliko kuponesha .

 

5. Kwa hiyo baada ya kuona aina hizi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya na kuachana na mila potovu kabisa ambazo zinaweza kuleta madhara zaidi, kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa mbadala ambazo uaminika na walio wengi ni vizuri kuzitumia ila tahadhari ni lazima na kama hali ikiwa mbaya katika matumizi ya dawa mbadala ni vizuri kabisa kumwona mtaalamu wa afya na kumweleza kila kitu kwa ukweli ili kusaidia katika kudili na tatizo.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/09/Saturday - 02:56:13 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 753


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-