Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika Ili kuweza kupunguza kuwepo kwa magonjwa ya zinaa
1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kuwa ugonjwa wa zinaa uleta matatizo mengi kwenye jamii kwa hiyo tunapaswa kutumia njia mbalimbali Ili kuweza kupunguza ugonjwa huu, kwa hiyo zifuatazo ni mbinu za kupunguza ugonjwa wa zinaa.
2 . kutumia kinga wakati wa kujamiiana na kuwa na mpenzi mmoja.
Kwa kutumia kinga kwa mtu ambaye haumfahamu kama ana maambukizi ni jambo zuri na la busara kwa sababu katika kufanya hivyo maambukizi hayawezi kuwepo, pia kuwa na desturi ya kuwa na mpenzi mmoja na kupima mara kwa mara Ili kuangalia kama Kuna maambukizi yoyote walau kila mwezi kama inawezekana.na pia ikitokea kuna maambukizi ni vizuri kupima nyote na kuhaidi kuwa waaminifu katika mahusiano.
3. Kuachana na Mila na desturi zinazochangia
kuwepo na kuenea kwa magonjwa ya zinaa.
Jamii inapaswa kuachana kabisa na Mila na desturi za zamani ambazo usababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa, kwa mfano kukeketa wasichana kwa kutumia wembe mmoja na pia kitendo cha kurithisha wanawake au wanaume ikitokea mmoja amefariki, kwa hiyo hali hii inapaswa kukoma kabisa na jamii za hivi zipatiwe elimu Ili kuweza kuokoa maisha ya watu na kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa haya kama vile ugumba na vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa na kaswende.
4. Kutoa elimu kwa wakimbizi na vijana walio kwenye umri wa kubarehe.
Kwa kawaida katika makazi ya wakimbizi Kuna hattari kubwa ya kuwepo kwa magonjwa ya zinaa kwa sababu ya kuwepo kwa watu mbalimbali na waliokusanyika kwa pamoja kwa hiyo wanapaswa kupewa elimu kuhusu madhara ya magonjwa ya zinaa na njia za kuepuka Nazo ambazo ni kuwa na mpenzi mmoja pamoja na kutumia kondom.
5. Vile vina na vijana wanapaswa kuwa na mipaka na kuepukana na matendo ya zinaa katika umri mdogo kwa hiyo wanapaswa kusubiri au hali ikiwa vibaya watumie kinga Ili kuepuka na kuwepo kwa magonjwa ya zinaa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV
Soma Zaidi...MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Matibabu ya vidonda vya tumbo inategemea sababu.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa bakteria unaoambukizwa na kupe ambao husababisha dalili kama za mafua. Dalili na ishara za Ugonjwa huu ni kati ya kuumwa na mwili kidogo hadi homa kali na kwa kawaida huonekana ndani ya wiki moja au mbili baada ya kuumwa na kupe. Njia bora ya
Soma Zaidi...Mrija wa mkojo hutoa mkojo nje ya mwili lakini mrija huu unapoziba hufanya utoaji wa mkojo kutoka kwa shida au maumivu
Soma Zaidi...ugonjwa wa kisukari ni moja katika magonjwa hatari sana, na mpaka sasa bado hauna matibabu ya kuponya moja kwa moja
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia dalili na namna ya kujikinga tusipate mafua .mafua kwa jina lingine hujulikana Kama baridi ya kawaida (common cold).baridi ya kawaida husababishwa na virusi kwenye pua na hutoa makamasi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kufanya usafi wa sikio, sikio ni mojawapo ya ogani ambayo usaidia kusikia,kwa hiyo sikio linapaswa kusafishwa kwa uangalifu kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Tetekuwanga (varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, upele kama vile malengelenge. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya kawaida ya tetekuwanga, karibu watu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia Watu wale ambao wana Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vitu ambavyo vinasababisha kuongezeka kwa Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na baada ya watu kujua Ugonjwa huu na matokeo ila bado ugonjwa unazidi kuongezeka.
Soma Zaidi...