Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi ambayo kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili inashuka.
Magonjwa nyemelezi
1.Ugonjwa wa kifua kikuu
Ni mojawapo ya magonjwa nyemelezi kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili ikishuka huu ugonjwa unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au endapo mgonjwa hajaanza kutumia dawa na pengine uambukizwa pale mtu akishika makohozi ya mgonjwa wa kifua kikuu na kama hajanawa mikono anaweza kushika kitu chochote Cha kula akajiambukiza, zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kifua kikuu.
_ kukohoa ndani ya wiki mbili na zaidi
_ kupungua uzito
_ kuwa na joto hasa wakati wa usiku
_ Homa za mara kwa mara
_ makohozi kuwa na damu
2. Magonjwa ya ngozi
Huu ni ugonjwa ambao pia ni nyemelezi kwa mtu ambaye kinga yake Iko chini, ambapo ngozi ya mgonjwa ushambulia sana na bakteria na kufanya mwili uwe na maupele upele ambayo hayaponi au uchukua mda mrefu kupona na pengine vidonda uweza kusababisha maambukizi mengine kama vile Homa kupanda zaidi na kusababisha madhara makubwa hasa kwa watoto kama vile degedege kwa hiyo tunapaswa kuwa macho iwapo kinga ya mwili ikishuka na kutafuta njia ya kuipandisha.
3.Kandidiasisi
Ni ugonjwa nyemelezi ambao utokea ikiwa kinga ya mwili ikishuka na hasahasa ushambulia sehemu za Siri na kusababisha maupele na kumfanya mtu aanze kujikinga , huu ugonjwa usababishwa na fangasi ambazo ushambulia sehemu za Siri,kwahiyo unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana kwa mtu Mwenye ugonjwa na ambaye Hana,kwa hiyo mtu akiwa na huu ugonjwa anapaswa kwenda hospitalini Ili akapatiwe dawa maana ugonjwa huu upo na unatibika
4. Mkanda wa jeshi.
Huu ni ugonjwa ambao utokea Baada ya kinga ya mwili kushuka, ugonjwa huu usababishwa na virusi ambaye ushambulia kulingana na sehemu ya nevu zinapopita kwa hiyo maambukizi uendana na nevu ya sehemu ndo maana utakuta mtu amishambuliwa sehemu fulani, Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa kutokea, maumivu kwenye sehemu ya maambukizi. Mgonjwa wa mkanda wa jeshi anaweza kupatiwa dawa kwa kufuata nadalili na hali ya maumivu na vidonda vilivyopo.
Magonjwa nyemelezi yakitokea ni lazima mgonjwa apelekwe hospitali mara moja Ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwa sababu iwapo kinga imeshuka sana magonjwa zaidi ya mawili yanaweza kutokea kwa wakati mmoja, kwa hiyo tuwe makini kulinda afya nzetu na kutumia dawa zinazohitajika .
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
UGONJWA WA GONORIA NA DALILI ZAKE (GONORRHEA)Gonoria (gonorrhea) ni katika maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.
Soma Zaidi...Kama una tatizo la midomo kuchubuka na kuwa myeupe ama kuwa na vidonda. Post hii inakwenda kuangalia swala hili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali,za miguu kufa ganzi,ni tatizo ambalo uwakumba watu wengi na walio wengi hawafahamu kabisa ni sababu zipi ambazo uleta tatizo hili.
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi aina za ajali kwenye kifua,pamoja na kifua kuwa na sehemu mbalimbali na pia na ajali ambazo utokea Huwa za aina mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Post yetu inaenda kuzungumzia kuhusiana na Saratani ya Matiti ni Saratani ambayo hutokea katika seli za matiti. Baada ya Saratani ya Ngozi, Saratani ya matiti ndiyo Saratani inayojulikana zaidi hugunduliwa kwa wanawake Mara nyingi. Saratani yaÂ
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Bawasiri. Bawasiri ni mishipa iliyovimba kwenye njia yako ya haja kubwa na sehemu ya chini ya puru. Bawasiri inaweza kutokana na kukaza mwendo wakati wa kwenda haja ndogo au kutokana na shinikizo la kuongeze
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi ya tishu ya matiti ambayo husababisha maumivu ya matiti, uvimbe, joto na uwekundu. Pia unaweza kuwa na Homa na baridi. Ugonjwa huu huwapata zaidi wanawake wanaonyonyesha ingawa wakati mwingine hali hi
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia ishara na dalili za SELIMUDU ambao kitaalamu huitwa Sickle cell Anemia.selimudu ni aina ya kurithi ya Anemia — hali ambayo hakuna chembechembe nyekundu za damu zenye afya za kutosha kubeba oksijeni ya kutos
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa ,kwa kawaida Ugonjwa huu utokea kuanzia kwenye wiki ya pili mpaka mwaka mmoja na hapo Ugonjwa unakuwa bado haujaonesha Dalili na Dalili zikishaonekana ni vigumu kutibika.
Soma Zaidi...