Dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa ,kwa kawaida Ugonjwa huu utokea kuanzia kwenye wiki ya pili mpaka mwaka mmoja na hapo Ugonjwa unakuwa bado haujaonesha Dalili na Dalili zikishaonekana ni vigumu kutibika.

Dalili za Ugonjwa wa kichaga cha mbwa.

1.Dalili ya kwanza ni kuwepo kwa maumivu makali kwenye kidonda,kwa kawaida utegemea na ukubwa wa kidonda kwa hiyo kuna tabia ya watu kuanza kutibu kidonda kwa njia za kawaida na kufunika bila kuchomwa dawa inayosababisha kuzuia kichaa cha mbwa hatimaye matokeo huwa mabaya kwa hiyo jamii inapaswa kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kutibu tatizo la ugonjwa wa kichaa cha mbwa hospitalini.Na kama Maumivu ni makali kwenye kidonda dawa za kutibu maumivu zinaweza kutumika ili kupunguza maumivu kwenye kidonda.

 

2.pengine mtu akiumwa na mbwa huanza kuogopa sana akiamini kwamba labda atafariki ila tunapaswa kujua kuwa kama umengatwa nambwa na ukaenda hospitalini na kupewa dawa kuwa na matumizi ni lazima kwa sababu unakuwa umefuata masharit kwa hiyo tuachane na tabia za kuogopa ovyo ovyo, ila kuna woga mwingine utokea kwa sababu ya kuingia kwa wadufu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.

 

 

3,Kuanza kuogopa maji na kuwa na tabia kama za mbwa, kama vijidudu havijatibiwa vizuri na vikisambaa sehemu mbalimbali za mwili usababisha mgonjwa kuwa na tabia mbwa mpaka kubweka na pengine uanza kuogopa maji ambapo kwa kitaalamu huitwa fear of water.

 

4. Kuwepo kwa maumivu hasa mgonjwa anapokuwa anameza wakati wa kula chakula.

Dalili mojawapo ya mgonjwa wa kichaa cha mbwa ni maumivu wakati wa kumeza chakula, hali hii utokea kwa sababu wadudu wanakuwa wamesambaa mwili mzima kwa hiyo kwa hatua hizi uponyaji ni kwa neema ya Mungu peke yake.

 

5. Kama Mgonjwa hajapewa dawa kwa kipindi chote tangia alipongatwa na mbwa dalili zikianza kujitokeza hasa kubweka kama mbwa, kuogopa maji na Dalili zinginezo mgonjwa ni vigumu kupona kwa hiyo anaweza kuishi kwa siku kumi tangu baada ya Dalili za hatari na kumgusa ila kufa ni lazima hasa kwa wagonjwa. 

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/25/Wednesday - 05:42:10 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 955


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-